Aliyeshindwa kura za maoni CCM Antony Msami ahamia CHADEMA achukua fomu za ubunge

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
Mgombea wa ubunge ccm aliyeshindwa kura za maoni Bw Anthony msami amehamia na ameomba kugombea ubunge kupitia chadema. Katibu wa chadema wa Wilaya ya Meru bw Totian Ndonde amethibitisha kuwa Msami amechukua fomu na anatarijiwa kuirudisha leo.

Bwana Msami amesema ana siri nzito ya rushwa ndani ya CCM ambapo kila mgombea alileta watu wake na kwa namna moja au nyingine wote wametoa rushwa. Anthony amekuwa akishutumiwa kuwa ni mamluki ndani ya CCM aliyetumwa na chadema kwenda kugawa kura na kufanya upelelezi amekanusha habari hiyo na kusema kuwa kimsingi watu wawili ambao watakuwa wamekiharibu chama katika kipindi hiki ni James Milya ambaye kundi la rafiki ya EL linataka SIOI apitishwe. Kundi lingine ni la BM ambalo linataka mtu wao apitishwe. Hata hivyo SIOI kama hana shida ni kajina anayeonekana ana uwezo isipokuwa anabebwa na kundi baya na chafu. Makundi yote haya mawili yamemwaga hela ya kutosha.

Msami ameulelezea kukerwa na mpango wa kuwatumia washili ambao anasema ni mambo yalipangwa kipropaganda. NI aibu kwa wazee wa CCM kukubali kubebeshwa jambo zito kama hili kuwa WAMEPANGA KUMCHINJA MBUNGE LEMA halafu inaonekana kuwa ni WASHILI wa meru.

Source: Arusha.
 
CDM mmeshazoea kupokea makapi, wapo wengi na huwa mnawapokea lakini wakija huko ndiyo wanakuwa SHIBUDA style.
 
CDM kuweni makini! Watu wa dizaini hii watakuwa mizigo. Shibuda ni mfano hai anavosumbua CDM. Msikubali mamluki hawa
 
Back
Top Bottom