Aliyeshinda kura za maoni CHADEMA Kalenga awekwa kiporo, Grace Tendega kupambana na CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
February 14, 2014

index.jpg

Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi jimbo la Kalenga walivyompongeza Sinkala Mwenda siku ya kura za maoni baada ya kushinda wenzake 13.

KAMATI kuu ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imemteua aliyekuwa mshindi wa pili wa kura za maoni katika zoezi la kura za maoni Bi Grace Tendega kupeperusha bendela ya Chadema katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kamati kuu ya Chadema iliyoketi jijini Dar es Salaam leo zinadai kuwa aliyekuwa mshindi wa kura za maoni mwanasheria Sinkala Mwenda hajateuliwa na kamati kuu hiyo mbali ya kuongoza kwa kura kura 132 dhidi ya kura 122 alizopata mpinzani wake wa karibu Grace Tendega

Katibu wa Chadema wilaya ya Iringa vijijini Felix Nyondo amethibitisha kuwa amepata taarifa hizo za kuteuliwa Bi Grace Tendega kuwa mgombea wa Chadema jimbo hilo la Kalenga .

Hata hivyo alisema anapongeza maamuzi ya kamati kuu na kuwataka wana Chadema Kalenga kujiandaa kwa kampeni za uchaguzi huo na kuanza kumnadi mgombea wao ili kuweza kushinda uchaguzi huo mdogo.

Kutokana na uteuzi sasa Tendega atavaana Godfrey Mgimwa wa CCM katika uchaguzi huo ili kuziba nafasi iliyoachwa waziri na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kalenga marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyefariki mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo duru za kisiasa kutoka ndani ya Chadema zinadokeza kuwa sababu ya kuachwa kwa mgombea huyo aliyeshinda kura za maoni mwanasheria Mwenda ni kutokuwa na mtaji wa watu kwa maana ya kutokubalika ndani na nje ya chama hicho hivyo Chadema kuona kumsimamisha Mwenda ni kulipoteza jimbo hilo.

Huku kwa upande wa mteule wao Bi Tendega amekuwa na sifa ya kugombea katika jimbo hilo kupitia chama cha Jahazi Asilia na kufanya vema japo si kwa kushinda hivyo nin imani yao kupitia Chadema anaweza kufanikiwa kushinda.

Muda mfupi uliopita, Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe amemaliza kuzungumza na waandishi wa habari, akitoa tamko la maamuzi ya Kamati Kuu iliyoketi kwa dharura jana jijini Dar es Salaam, kujadili agenda moja kuu; Uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, ambapo kikao hicho kimefanya uteuzi wa jina la mgombea wa CHADEMA, ambaye ni;

Ndugu Grace Tendenga Mvanda

attachment.php

Mpambanaji huyu ni Mwalimu kitaaluma, akibobea katika Elimu ya Saikolojia ya Jamii pia na masuala ya ukuzaji mitaala.
 
huu ni ubakaji wa demokrasia...
wamedharau sauti ya wanachadema kalenga
hawatapata kitu
 
Napenda kuishukuru kamati kuu kwa kufanya maamuzi magumu ya kumteua mama Grace Tendega licha ya mama huyo kushika nafasi ya pili kwenye kura za maoni.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya jimbo la Kalenga toka uhuru wa nchi hii litatoa mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza haijawahi kutokea ni aibu kwa nchi inayodai kupigania usawa.

Nashukuru chadema kwa kusikia ushauri wangu kuwa CCM inamwogopa yule mama kutokana na historia yake ya kupambana na ccm akiwa kwy chama dhaifu cha jahazi asilia na huku akiwa ni mkulima na hana resources kabisa lakini alikuwa na msimamo na roho ya ujasiri ya kutembea jimbo zima na baskeli za mashabiki wake na watu waliimpenda sio kwa elimu yake wala nini bali ni misimamo na ujasiri wake pamoja na kwamba yeye ni mkulima tu wa kawaida na niliwaambia chadema msitishwe cv ya mtu kwani mama ana reflect cv za watanzania walio wengi vijijini.
 
Yale yale ya Mbega na Mwakalebela

hapana yule mama anapendwa jimbo zima kwa ajili ya ujasiri na misimamo yake na hasa ukizingatia tofauti yao kura mama bado ana nguvu na hasa ukingatia yeye ni mama mkulima tu lakini walipishana na mwanasheria kwa kura kumi na chadema ilishatuma timu yake ya investigation kwy ground kwahiyo chadema wako makini sana kumteua huyu mama na watashinda kwani ccm ndiye mtu pekee ilikuwa inamwogopa. ccm ita panic na kuanza kumpiga mabomu huyu mama na ndiyo kitachoizamisha ccm kalenga na anakwenda kuwa mbunge wa kwanza mwanamke toka uhuru kutoka jimbo la kalenga
 
wameanza mambo ya magamba!

Huyu mama ni pandikizi la akina Slaa. Kilichomponza Sinkala ni misimamo yake isiyotetereka na usomi wake. Hakika chadema haiwapendi wasomi
 
Napenda kuishukuru kamati kuu kwa kufanya maamuzi magumu ya kumteua mama Grace Tendega licha ya mama huyo kushika nafasi ya pili kwenye kura za maoni.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya jimbo la Kalenga toka uhuru wa nchi hii litatoa mbunge mwanamke kwa mara ya kwanza haijawahi kutokea ni aibu kwa nchi inayodai kupigania usawa.

Nashukuru chadema kwa kusikia ushauri wangu kuwa CCM inamwogopa yule mama kutokana na historia yake ya kupambana na ccm akiwa kwy chama dhaifu cha jahazi asilia na huku akiwa ni mkulima na hana resources kabisa lakini alikuwa na msimamo na roho ya ujasiri ya kutembea jimbo zima na baskeli za mashabiki wake na watu waliimpenda sio kwa elimu yake wala nini bali ni misimamo na ujasiri wake pamoja na kwamba yeye ni mkulima tu wa kawaida na niliwaambia chadema msitishwe cv ya mtu kwani mama ana reflect cv za watanzania walio wengi vijijini.
Hivi jimbo la Moshi mjini liliwahi kutoa mbunge wa kuchaguliwa mwanamke?
 
Huyu mama ni pandikizi la akina Slaa. Kilichomponza Sinkala ni misimamo yake isiyotetereka na usomi wake. Hakika chadema haiwapendi wasomi

naona chiku abwao kashamtafutia mshefa maana nasikia ni mashosti sana
 
Tofauti ya kura 10 tu? Thats insignificant

jerry, CCM ilikuwa inamwogopa sana huyu mama Tendega na tuna wasiwasi hata hizo kura alizopata mwanasheria zinaweza kuwa na mkono wa ccm(speculation) ili kumwezesha ashinde. chadema ninahisi wameliona hilo na kulifanyia kazi na huyu mama anakwenda kuvunja historia ya kalenga kwa kuwa mbunge wa kwanza mwanamke kutoka jimbo kitu ambachi ccm walikuwa wakikiofia sana kwani wapiga kura wengi ni wakina mama vijijini na yeye ni mkulima mwenzao matatizo yao anayatambua kwani kila siku anaishi nao
 
ha ha ha

chadema mnaota sana tutaona mtakavyoangukia pua
 
Hakuna demokrasia ndani ya chadema huu ni uhuni mwingine kufanywa na chadema kwa kuipanda panda demokrasia.
 
Kwani huyu grace yupo karibu na kigogo gani ndani ya chadema au na yeye anatoka kwa wenye chama.

ni shoga yake na yule chiku abwao

chiku abwao ana ukaribu binafsi na wakubwa wa chama

hivyo?.......................
 
Back
Top Bottom