Aliyeshauri ofisi za mabasi ya mwendokasi (UDART) zijengwe Jangwani akamatwe mara moja

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,383
217,464
Kwa namna yoyote ile huyu mtu hakuwa na nia njema. Jangwani kwa miaka kadhaa imefahamika kama mkondo wa bahari, sasa kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ama mwenye nia njema asingeleta ushauri duni wa kiwango kile.

Nasema akamatwe ahojiwe na nina hakika mengi yatafumuka.

===
1576657002217.png


Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Udart) umeamua kuhamisha ofisi zake kwa muda ili kuepusha uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.

Ofisi hizo zilizopo eneo la Jangwani, wilaya ya Ilala, kwa sasa hazitatumika na mabasi yote yaendayo haraka yatalazwa katika vituo vikuu vya mabasi hayo.

Akizungumza leo Machi 16 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Udart, Deus Bugaywa amesema wamehamisha ofisi hizo ili shughuli zinazofanywa na mradi huo zisiweze kutetereka kutokana na mvua zinazoendelea.

"Maji yalianza kujaa saa nane usiku, tulianza kuhamisha magari yetu yote na kuyapeleka katika vituo vikubwa vya mabasi yetu, licha ya mabasi pia tumehamisha vitu vingi vya ofisi kwa sasa hatutaitumia kwa muda," amesema Bugaywa.

Amesema wameamua kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, kutokana na maji kujaa eneo la jangwani na hivyo barabara hiyo ilifungwua tangu saa kumi alfajiri na imefunguliwa saa tatu asubuhi baada ya trafiki kujiridhisha kwamba inafaa kupitika.


Pia Soma:
 
Si kwamba ofisi za UDART zilijengwa kwenye mkondo wa maji maarufu Dar na Tanzania, ila barabara iliyojengwa kwa akili za ulafi.

Kabla ya kuweka hiyo lami mpya na lane ya BRT, mvua ikinyesha kila mtu aliona barabara ilivyokuwa ikifunikwa na maji eneo lile, Ajabu; unachimba mtaro ili kupitisha barabara, kweli? Kulikuwa na haja gani kutokea Magomeni kuchimba vile na kujenga kingo pembeni? Daraja la maana na useful lingejengwa pale na chini wakaacha maji yapite mvua inyeshapo.

Kwani Waziri wa barabara alikuwa nani kipindi kile? Mkinitajia hata alipokea mradi ule inatosha!
 
Kwa namna yoyote ile huyu mtu hakuwa na nia njema. Jangwani kwa miaka kadhaa imefahamika kama mkondo wa bahari, sasa kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ama mwenye nia njema asingeleta ushauri duni wa kiwango kile.

Nasema akamatwe ahojiwe na nina hakika mengi yatafumuka.
Unamaanisha kuwa Rais Magufuli akamatwe na kushtakiwa au? Maana ndo alikuwa the boss wa huo mradi na alikuwa anaukeshea site kikamilifu. Kama ni yeye unataka akamatwe basi tunaomba uongoze kikosi sisi tuko nyuma
 
Labda mradi ulitengenezwa kipind cha kiangazi mkuu.

Si unajua akili zetu hazifikirii mbali.
Hii haiwezi kuwa sababu ya kujitetea wahandisi waliotoka ujerumani au hata Juba kule South Sudan.
Ule ni uzembe na matumizi mabaya ya rasilimali za umma(pesa).

Kwa hivyo madaraja yote yaliyojengwa kiangazi yalitakiwa yawe ya ovyo wakati wa mvua?
 
Back
Top Bottom