Aliyeshauri ofisi za mabasi ya mwendokasi (UDART) zijengwe Jangwani akamatwe mara moja

Binadamu tunaposhindwa kuyatawala mazingira yetu, inadhihirisha ni kiasi gani hatujaelimika.
 
Kutokana na uharibifu wa miundombinu serikali ya mkoa ama uongozi wa kampuni uzihamishe hizo ofisi hapo jangwani. Ni aibu kubwa kwa serikali na taifa letu, kama ni uzembe ulishafanyika, na hii wapembunzi wa mradi walitanguliza rushwa ktk serikali ilo pita. Miaka mingi inajulikana kuwa eneo hilo mafuriko hayaishi. Tuwe na akili timamu hatuwezi kuendelea kutumia ofisi kubwa kama hiyo katika eneo hilo. Uongozi wa jiji uchukue hatua haraka kuhamisha ofisi kama ni hasara ya ujenzi tuikubali tu. Meya wa jiji kazi kwako na maamuzi sahihi asante.
Mkuu,kipekee nilivyoona wanaishia level ile ya tuta na kwa kumbukumbu za mvua katili zile za mwaka 2012,ni dhahiri kabisa kilichotokea kitaendelea mwaka hadi mwaka. Tuta lililowekwa ni dogo mno kulingana na eneo oevu lilivyo. Pale ili kuweka majengo,reference point ilikua ni level iliyoko pale fire mataa ya Muhimbili. Yaani ujaze tuta angalau linalokaribia au sawa na level za mataa ya Muhimbi pale fire. Lakini kwa tuta lililopo sasa,hali ile itakua kila mwaka. Ni jambo lililo dhahiri kabisa kuwa ili kujaza tuta(road embankment) kwa level ya mataa ya fire-Muhimbili Junction,ili takiwa fill material nyingi kuwa imported ambayo ni gharama kubwa sana.
 
Nayasikitikia magari Yale, halafu migari ya umeme kwa karibu system yote hasara,walioifikisha kampuni kujenga pale watafutwe na kushughulikiwa, hasara tupu
 
Jana nimejiuliza sana ,nani alishauri kujenga ofisi na karakana ya mabasi ya mwendo kasi pale jangwani?
Eneo ambalo sote tunajua huwa hatarishi wakati wa mvua.
Eneo ambalo watu waliondolewa kwa ajiri hiyo hiyo ya kuhatarisha maisha na mali zao.
Ina maana hakukuwa na maeneo mengine?
Vipi kama itafikia wakati watalazimika kuhamisha ofisi.....ghara hizo hasara ya nani?
Vipi kama mvua zitanyesha mfululizo wiki nzima ?
NI MASWALI MENGI YA KUJIULIZA.
................NAJIULIZA TU NIKIWA NAPITA NAENDA ZANGU KARIAKOO.......
 
Hilo eneo likiendelezwa vizuri wala sio korofi..niliwahi kufanya mazungumzo na kijana Fulani ambaye kwa sasa ni mkuu Wa mkoa Fulani ..akanipa idea njema sana za kuboresha eneo lile in comparison to Libya...
 
Ofisi zimejengwa kwenye bonde la mto msimbazi eneo linalojulikana kama jangwani. Ofisi hazijajengwa jangwani. Shida siyo wapi zilipojengwa hizo ofisi, shida ni namna zilivyojengwa. Wenzentu kwenye nchi zilizoendelea nyumba zinajengwa mitoni au baharini ambapo maji ndipo yanapooishi sembuse bondeni ambapo maji yanakuja mara moja moja. Shida ni kwamba hazijajengwa kwa namna ya kupambana na hali ya pale.
 
kwa wenzetu hata pembeni ya bahari wanauwezo wa kujenga,lakini kwengi ni mara ngapi watalamu na watawala wetu wamekuwa na maono hayo?, ofisi za DAWASCO basihaya huwa mvua zikinyesha kubwa wanakimbia ofisi.
 
Ofisi zimejengwa kwenye bonde la mto msimbazi eneo linalojulikana kama jangwani. Ofisi hazijajengwa jangwani. Shida siyo wapi zilipojengwa hizo ofisi, shida ni namna zilivyojengwa. Wenzentu kwenye nchi zilizoendelea nyumba zinajengwa mitoni au baharini ambapo maji ndipo yanapooishi sembuse bondeni ambapo maji yanakuja mara moja moja. Shida ni kwamba hazijajengwa kwa namna ya kupambana na hali ya pale.
Sahihi kabisa
 
Mafuriko jangwani jana tarehe 08/01
 
Attachments

  • VID-20180108-WA0026.mp4
    12.7 MB · Views: 26
Si kwamba ofisi za UDART zilijengwa kwenye mkondo wa maji maarufu Dar na TZ, ila barabara iliyojengwa kwa akili za ULAFI.

Kabla ya kuweka hiyo lami mpya na lane ya BRT, mvua ikinyesha kila mtu aliona barabara ilivyokuwa ikifunikwa na maji eneo lile, AJABU; unachimba mtaro ili kupitisha barabara, kweli??? Kulikuwa na haja gani kutokea magomeni kuchimba vile na kujenga kingo pembeni? Daraja la maana na USEFUL lingejengwa pale na chini wakaacha maji yapite mvua inyeshapo.

Kwani waziri wa barabara alikuwa nani kipindi kile??? Mkinitajia hata alipokea mradi ule inatosha!
ingependeza kama ingejengwa flyover au daraja kutoka fire mpaka mapipa chini yapite maji
 
Cha kushangaza miaka yote wamekuwa wakiwatoa watu jangwani kwa kuwa ni hatari kwa maisha yao,ajabu wao wanaenda kujenga pale.ona sasa kama jana imebidi watolewe ofisini na boti.
Heeh!! walitolewa ofisini kwa boti? ... Hivi wao walidhani ni samaki.. unawahamisha wenzako halafu unaenda kuweka makazi
 
Back
Top Bottom