Aliyeshauri ofisi za mabasi ya mwendokasi (UDART) zijengwe Jangwani akamatwe mara moja

Inawezekana mzembe namba 1 ni yule aliyepaita JANGWANI eneo linalopata mafuriko makubwa kiasi kile, labda ndo aliwapumbaza makandarasi walifikiri wanajenga sehemu yenye jangwa. Anyway I'm kidding

Japo kinachonihuzunisha kwenye huu usafiri ni dana dana zinazopigwa kila uchwao! Tatizo la msongamano kwenye vituo linazidi kuongezeka kila siku, then mawaziri wanaenda kukagua na kudanganywa eti sababu kubwa ni traffic police kuongoza magari badala ya taa wamesahau kuwa mradi ulikuwa designed kuoperate mabasi 300 na UDART(operators) wana jumla ya mabasi 140 and probably mengine hayafanyi kazi (kutokana na kuwa over used) then waziri unaenda kusikiliza kero na unakuja na recommendation kuu eti kuwaondoa traffic police badala ya kuja na mbadala halisi KUONGEZA IDADI YA MABASI. kweli nchi hii kazi ipo
 
Hivi haya maji ya jangwani hatuwezi kuweka mtambo wowote wa kuyavuna na kuyatumia japo yanakuja kwa msimu, maana yake kila msimu yanakuja na uharibifu. Sasa kila msimu yangekuwa yanakuja kwa manufaa ingekuwa poa sana. Alafu unajua jangwani sio user friends kabisa lakini watu mate yanawadondoka kila siku, yaani ubongo unawaza miradi miradi tu! sababu jografia ya jangwani wanailazimisha kimiradi wakati pale ni basin ya kupokea maji ya mji na kutupa bahari ya hindi, hivi hii nchi inawasomi kweli au?
 
Una level gani ya utaalamu kwenye mambo ya ujenzi? Pendekeza ambapo kwako pangefaa uje na sababu 5 za pendekezo lako.
Nchi imekwama kwa akili ya kudhani wanataaluma ndio kila kitu kwenye kusongesha nchi mbele kimaendeleo.

Huhitaji hizo levo zako za elimu kujua pale ni mkondo wa maji! Si bora hata ungedesa au ungepata digirii ya pichu mkononi ukajua kuibia kuliko kujifanya mweledi na kuzamisha rasilimali fedha kivile.

Samahani kama unatumia CHAMA kuwaza.
 
Kwa namna yoyote ile huyu mtu hakuwa na nia njema , Jangwani kwa miaka kadhaa imefahamika kama mkondo wa Bahari , sasa kwa mtu yeyote mwenye akili timamu ama mwenye nia njema asingeleta ushauri duni wa kiwango kile .

Nasema akamatwe ahojiwe na nina hakika mengi yatafumuka .
Unaujua mkondo wa bahari? Hapo jangwani ni flood plain wakati wanataka kujenga hayo majengo walitakiwa wasome kwa umakini level ya maji wakati mvua nyingi inaponyesha
 
Una level gani ya utaalamu kwenye mambo ya ujenzi? Pendekeza ambapo kwako pangefaa uje na sababu 5 za pendekezo lako.
Mnapenda kutafuniwa.
Mkiachiwa mtafune mnameza bila kutafuna! kivumbi mkifika 'toileti' usicheze na makukulu.

Ona sasa muundombinu unavyobuma!
 
Kutokana na uharibifu wa miundombinu serikali ya mkoa ama uongozi wa kampuni uzihamishe hizo ofisi hapo jangwani. Ni aibu kubwa kwa serikali na taifa letu, kama ni uzembe ulishafanyika, na hii wapembunzi wa mradi walitanguliza rushwa ktk serikali ilo pita. Miaka mingi inajulikana kuwa eneo hilo mafuriko hayaishi. Tuwe na akili timamu hatuwezi kuendelea kutumia ofisi kubwa kama hiyo katika eneo hilo. Uongozi wa jiji uchukue hatua haraka kuhamisha ofisi kama ni hasara ya ujenzi tuikubali tu. Meya wa jiji kazi kwako na maamuzi sahihi asante.
 
Waliofanikiwa kupata picha tuoneshane ili comment ziwe na mashiko
 
Back
Top Bottom