Aliyesema Waziri Ummy kafungua duka la dawa za nguvu za kiume akamatwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Serikali imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa zinazotangazwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa hazijadhibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Akizungumza Jijini Dodoma mara baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kumekuwa na wimbi la watu mbalimbali wanaotoa kiholela matangazo ya kuuza dawa za aina mbalimbali kupitia mitandao husika.

"Jamii itambue kuwa kuuza dawa ambazo hazijazidhitishwa ni kosa kisheria na niwatake wahusika kuacha mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao,”Alisisitiza Mhe Ummy.

Akifafanua, Ummy amesema kuwa ifahamike kuwa dawa siyo kama nguo,viatu ama bidhaa nyingine kama hizo ambazo mtumiaji anaweza kununua kadiri utakavyo kutokana na mahitaji au uwezo wake, lakini dawa isiyothibitishwa na mamlaka ni sumu na kwamba inaweza kumgharimu maisha mtumiaji anayetumia bila maelekezo ama ushauri wa daktari.

Aliongeza kuwa, Kamati hiyo imeitaka Wizara yake kuongeza jitihada katika kuzuia matangazo yanayotolewa kupitia mitandao ya kijamii yakinadi dawa za aina mbalimbali ikiwemo kuhusu masuala ya uzazi na magonjwa mengine.

Aidha Ummy Mwalimu,amesema, tayari Wizara yake imeshaanza kuchukua hatua kupambana na vitendo vya kutangaza dawa na chakula mitandaoni bila kusajiliwa na kwamba tayari mtu mmoja ameshakamatwa na wakati wowote anatarajiwa kufikishwa mahakamani kufutia kitendo chake cha kutangaza dawa ya kuongeza viungo vya wanaume na kudai kuwa Waziri Ummy,alifungua duka husika lililoko Kariakoo,jijini Dar Es Salaam wakati taarifa hizo zikiwa si za kweli.

Katika hatua nyingine, aliwataka wale wote wanaotaka kuuza dawa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria kuepuka kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Chanzo: Maelezo Blog
 
Kwani hizo nguvu za kiume ni za nini? Si usipokuwa nazo zinakusaidia kutuliza na kuendelea na mipango ya maendeleo? Mi nataka nimuombe Mungu anipunguzie hizi nilizonazo kusudi nifanye mambo mengine ya maendeleo. kwani kipapuchi changu kinanizingua kusimama simama na kudai vitafunio
 
Mkuu unapapuchi na wewe?
 
Nguvu za kiume kwaajili ya kutafuta pesa
Kwani hizo nguvu za kiume ni za nini? Si usipokuwa nazo zinakusaidia kutuliza na kuendelea na mipango ya maendeleo? Mi nataka nimuombe Mungu anipunguzie hizi nilizonazo kusudi nifanye mambo mengine ya maendeleo. kwani kipapuchi changu kinanizingua kusimama simama na kudai vitafunio
 
Kwani hizo nguvu za kiume ni za nini? Si usipokuwa nazo zinakusaidia kutuliza na kuendelea na mipango ya maendeleo? Mi nataka nimuombe Mungu anipunguzie hizi nilizonazo kusudi nifanye mambo mengine ya maendeleo. kwani kipapuchi changu kinanizingua kusimama simama na kudai vitafunio
Kumbe una papuchi?
 
Mwanaume huna hela nguvu za kiume unazitolea wapi?

mantiki ilopo wanaume wengi sasa hivi hawana nguvu za kiume kwa sababu hawana hela, kipnd cha utawala wa kikwete pesa ilikua nje nje ikpatkana kwa urahic na matumiz yake kuwa ya kizembe haikui kuckika kama sasa hiv kuhusu nguv za kiume

Na weng wanaovumisha n wanawake wakichukulia kama sababu za kuwaacha wapenz wao wasiokuw na hela

Nirud kwenye mada hapo juu hii mada inahusu uuzwaji wa daw kiholela
Wale wazee wa alliance in global motion nao wamo au?
 
Kwani hizo nguvu za kiume ni za nini? Si usipokuwa nazo zinakusaidia kutuliza na kuendelea na mipango ya maendeleo? Mi nataka nimuombe Mungu anipunguzie hizi nilizonazo kusudi nifanye mambo mengine ya maendeleo. kwani kipapuchi changu kinanizingua kusimama simama na kudai vitafunio
Kipapuchii kinasimama tena?? Ohoo! Hatari basi.
 
Serikali imewataka wananchi kuepuka matumizi ya dawa zinazotangazwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kuwa hazijadhibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Akizungumza Jijini Dodoma mara baada ya kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kumekuwa na wimbi la watu mbalimbali wanaotoa kiholela matangazo ya kuuza dawa za aina mbalimbali kupitia mitandao husika.

"Jamii itambue kuwa kuuza dawa ambazo hazijazidhitishwa ni kosa kisheria na niwatake wahusika kuacha mara moja kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao,”Alisisitiza Mhe Ummy.

Akifafanua, Ummy amesema kuwa ifahamike kuwa dawa siyo kama nguo,viatu ama bidhaa nyingine kama hizo ambazo mtumiaji anaweza kununua kadiri utakavyo kutokana na mahitaji au uwezo wake, lakini dawa isiyothibitishwa na mamlaka ni sumu na kwamba inaweza kumgharimu maisha mtumiaji anayetumia bila maelekezo ama ushauri wa daktari.

Aliongeza kuwa, Kamati hiyo imeitaka Wizara yake kuongeza jitihada katika kuzuia matangazo yanayotolewa kupitia mitandao ya kijamii yakinadi dawa za aina mbalimbali ikiwemo kuhusu masuala ya uzazi na magonjwa mengine.

Aidha Ummy Mwalimu,amesema, tayari Wizara yake imeshaanza kuchukua hatua kupambana na vitendo vya kutangaza dawa na chakula mitandaoni bila kusajiliwa na kwamba tayari mtu mmoja ameshakamatwa na wakati wowote anatarajiwa kufikishwa mahakamani kufutia kitendo chake cha kutangaza dawa ya kuongeza viungo vya wanaume na kudai kuwa Waziri Ummy,alifungua duka husika lililoko Kariakoo,jijini Dar Es Salaam wakati taarifa hizo zikiwa si za kweli.

Katika hatua nyingine, aliwataka wale wote wanaotaka kuuza dawa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria kuepuka kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii leo Oktoba 23, 2019 Bungeni Jijini Dodoma imepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA).

Chanzo: Maelezo Blog
kigogo au?
 
Back
Top Bottom