Aliyesema CHADEMA mwaka huu itapata wabunge tu anaota mchana kweupe

Prof Koboko

Senior Member
Aug 15, 2020
126
1,000
Hivi unawezaje kusema CHADEMA kitapata wabunge 10 tu mwaka huu? Sababu hasa ya msingi ni ipi mpaka hivyo? Hivi kwa hali unayoiona, kitapata wabunge 10 tu au kitaongeza maradufu?

CHADEMA kinafanya mikutano yake hakuna mwaliko wa msanii hata mmoja lakini maelfu ya wananchi wanahudhuria mikutano yao kwa wingi kuliko hata ya CCM,CCM wamekusanya wasanii wote wakubwa na maarufu wa nchii, TV stations zote zinaipa Coverage CCM tu lakini bado mikutano yao iko sawa au inashindwa na ya CHADEMA. Sasa CCM wakiacha kutumia media nyingi kwa nguvu na wasanii nani atahudhuria mikutano yao? Wakamsikilize nami mwenye jipya lipi?

Magu si amezunguka nchi nzima huku aligawa pesa miaka yote 5 akidai kua yupo kwenye ziara anakagua miradi yake?

Nimeangalia Mikutano ya Tundu Lissu mikoa ya MARA, ARUSHA, MBEYA, MWANZA, MBEYA, IRINGA, MOROGORO, KATAVI, KIGOMA, TABORA, RUKWA, KAGERA maeneo mengine alikopita siamini kama ndio huyu Lissu ana nini kumshinda Magu ambaye yupo na dola miaka yote 5. Hawa wananchi wamechoka na nini aisee?
 

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
2,173
2,000
Chadema kama kweli watafikisha wabunge kumi (10) katika uchaguzi huu watastahili pongezi, upinzani kwa ujumla wake watapata wabunge zaidi ya 20 kwakua wengine watachaguliwa kutoka Zanzibar.
 

Leonardo Harold

JF-Expert Member
May 13, 2019
272
500
Huu ni mwaka wa maajabu.

Kama ambavyo hawakutegemea kama lissu angetoka hai baada ya risasi za kutisha ndivyo hawatategemea jinsi wanavyoenda kumkabidhi ikulu.
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,321
2,000
Watu hawaelew kwanini kila mgombea anajaza watu.

Watu walimiss kuona shughuli za siasa ila moyoni wanajua ni yupi wa kumchagua
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
2,902
2,000
Upinzani hata kupata mbunge mmoja ni ndoto za alinacha.

Watu wengi wanaenda kumshangaa mtu aliyrnusulika kufa kwa lisasi huwa anafananaje tu sio Sera. Maana wameona CCM ikitenda na kuwatendea makubwa wanasubiri kuirudisha tu kwa kishindo
 

AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
953
1,000
CCM haijaanza jana wala juzi kutumia wasanii. Jidanganye tu, kwani wananchi wapo smart kuliko wewe. Nani anapenda awe na mwakilishi asiyemwakilisha?. Bajeti mnapinga, bungeni mnatoka, Sasa wananchi wawachague ili iweje?. Magufuli yuko sahihi, wananchi wasichague gunzi.
 

AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
953
1,000
Chadema kama kweli watafikisha wabunge kumi (10) katika uchaguzi huu watastahili pongezi, upinzani kwa ujumla wake watapata wabunge zaidi ya 20 kwakua wengine watachaguliwa kutoka Zanzibar.
Chadema saccos Ltd, ilipigwa tafu na ukawa 2015. Safari hii mtakula wa chuya. Wabunge wengi hasa wa Chadema, huko majimboni mwao hakuna walichofanya. Mwaka huu lazima mpate mkwaju, Oct 28.Tunataka maendeleo sie, wala sio porojo.
 

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
5,277
2,000
Chadema kama kweli watafikisha wabunge kumi (10) katika uchaguzi huu watastahili pongezi, upinzani kwa ujumla wake watapata wabunge zaidi ya 20 kwakua wengine watachaguliwa kutoka Zanzibar.
CCM mjiandae tu kwa wapinzani mwaka huu
 

Ney Aziz

Member
Sep 21, 2020
47
125
Kwani wasanii wameanza kuperform kwenye majukwaa ya Siasa mwaka huu...Si walikuwepo na hata kabla ya Uchaguzi walikua wanashiriki kwenye shughuli za Vyama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom