Aliyesababisha kifo cha Salome Mbatia akamatwa

Acheni conspiracy theories hapa. Hiyo ajali, imetokea, imetokea. Huyo mbatia siku yake ndio ilikuwa imefika. Wote tutakufa, na hatujui tutakufa kwa jinsi gani na tutakutana wapi na ziraeli.

Kwani watanzania wangapi wanakufa kila siku kwa ajali za barabarani?? Kwani huyo marehemu ana tofauti gani na za kibanadamu na mwanakijiji wa chole samvula???

Kwani kuna watanzania wangapi wanauawa kwa makusudi mithili ya yule mtangazaji wa zamani wa RTD au marehemu Minde?
 
Kifo cha Mbatia chadaiwa kusabishwa na mwendo kasi wa dereva wake

Na Hakimu Mwafongo, Njombe


CHANZO cha ajali mbaya iliyotokea eneo la Factory

wilayani Njombe na kusababisha kifo cha Naibu Waziri wa Maendeleo ya Wanawake, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia, wiki iliyopita inadaiwa kusababshwa na mwendo kasi wa dereva wa gari lake ambaye alikosa mwelekeo na kisha kugongana uso kwa uso na lori aina ya Mitsubishi Fuso.


Katika ajali hiyo gari la Waziri huyo aina ya Nissan Patrol liligongana uso kwa uso lori hilo lililokuwa limesheni mbao kutoka Lupembe

kwenda makambako.


Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo ambao

hawakutaka kutaja majina yao walisema lori hilo

lilikuwa limetoka kusimama umbali mfupi kutoka eneo la ajali hiyo, hivyo halikuwa kwenye mwendo kasi.


Waliongeza kuwa eneo hilo lina mwinuko kidogo hivyo lori lenye mzigo mzito haliwezi kupandisha kwa kasi.


Kijana mwingine ambaye alikuwepo eneo ambalo lori hilo lilisimama, alisema wao walikuwa wanatengeneza lori jingine na kwamba lori lililopata ajali lilipofika mahali hapo

lilisimama na baadaye kuendelea na safari.


Aliongeza kuwa muda mfupi baada ya kukata kona

iliyokuwajirani yao walisikia mshindo mkubwa na

baada ya kwenda wakakuta ajaliiliyohusisha lori hilo na Nissan ilimokuwemo Marehemu Salome.


Wengine walisema dereva wa Nissan hiyo alikosa

mwelekeo baada ya kumkwepa mwendesha baiskeli na

kugongana uso kwa uso na lori hilo.


?Unajua kutokana na kasi aliyokuwa nayo dereva wa

Nissan, mara baada ya kumkwepa mwendesha baiskeli

alikosa mwelekeo na kukutana uso kwa uso na lori?, walisema.


Majeruhi wa ajali hiyo Dastani Gonza (26) ambaye nifundi wa kupasua mbao na mkazi wa Mufindi ambaye amelazwa wodi namba nne katika Hospitali ya Kibena wilayani Njombe, alisema walisimama lilipokuwa lori lililoharibika na mara baada ya kuanza safari, walipofika katika mwinuko walikutana na Nissan iliyokuwaimehama upande wake.


Aliongeza kuwa Nissan hiyo ilikuwa kwenye mwendo kasi na katika jitihada za kukwepana ziligongana uso kwa uso.


Alisema kuanzi majira ya saa kumi walipoata ajali hakujitambua mpaka alipopata fahamu akiwa wodini yeye na mwenzake.


Gonza aliumia kichwani mkononi na mguu wa kushoto

wakati fundi mwenzake Nicolas Lubuva aliumia shingoni, mbavu na kichwani.


Matroni wa Hospitali hiyo, Asia Mlimbila, alisema

majeruhi hao wanaendelea vizuri na kufahamisha kuwa Gonza anaweza kuinuka na kukaa kwa muda

lakini Lubuva hawezi kutokana na kuumia mbavuni.


Katika ajali hiyo Dereva wa roli hilo, Peter Mangula aliyenusurika katika ajali hiyo alitoroka na jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta.
 
Watu wamekimbilia kumlaumu dereva wa Fuso bila hata ushahidi.

Kama nilivyoandika mwanzoni, baadhi yamadereva wanaendesha upande wa pili kwenye zile barabara nzuri kama ya Kwenda Njombe.
 
madereva wenye magari madhubuti nao tanzania wamekuwa wanajiona wafalme wa barabara..........wanaendesha kwa kasi na kusababisha ajali kwa gari ndogo ndogo au kwa wenye baskeli
 
Hii habari inasikitisha sana. Na kuwa nasikia huyu dereva wa mheshimiwa alikuwa houseboy aliyepandishwa cheo kuwa dereva, na kwa kuwa hata mashuhuda wa ajali wanathibitisha yeye ndiye aliyekuwa akiendesha kimakosa, naanza pia kupata wasiwasi juu ya umakini uliotumika katika kumpatia leseni ya udereva. Labda alijifunzia gari nyumbani kwa bosi wake, halafu kwa influence ya bosi huyohuyo akapatiwa leseni. Ni wasiwasi wangu tu, sina uthibitisho, lakini mazingira ya tukio na background ya dereva yananifanya niwe na mawazo hayo.
 
The whole thing still very suspicious!

Kuna kitu hapa na bado naamini hii ni assassination attempt that went wrong, kill me if you dont like it!
 
The Absence Of Evidence Is Not The Evidence Of Absence? Are Theren't Any Evidence? Are There Any Evidence? If.....then.... And Ifnot.....then....., Finnish!
 
Hivi taarifa ya Kikosi cha Usalama barabarani (Traffic police) imeshatoka au ndio kaputi? Wanasema nini kuhusu hii ajali? Jinsi wanavochelewa ndio ushahidi unavyopotea, nani anayeshughulikia?
 
Hata mie najiuliza swali bado kama dereva wa lori amepatikana au bado! hivi vifo vya kutatanisha vinazidi sasa Tanzania!
 
Yule dereva aliyehusika katika ajali ya Bi. Salome Mbatia na ambaye alikuwa ameajiriwa muda si mrefu kabla ya ajali ile na kutoweka kama mvuke na kutokomea kama "night crawler" wa matrix hakuacha hata vumbi? Hivi jina lake la kweli lilikuwa lile?

Huyu bwana alihusika na ajali ya Waziri ambaye kabla ya hapo aliwahi kushikilia nafasi ya Mweka Hazina Mkuu wa CCM wakati ufisadi wa EPA unatokea...

that is all sir, I was just thinking...

sorry to bother you.
 
Yule dereva aliyehusika katika ajali ya Bi. Salome Mbatia na ambaye alikuwa ameajiriwa muda si mrefu kabla ya ajali ile na kutoweka kama mvuke na kutokomea kama "night crawler" wa matrix hakuacha hata vumbi? Hivi jina lake la kweli lilikuwa lile?

Huyu bwana alihusika na ajali ya Waziri ambaye kabla ya hapo aliwahi kushikilia nafasi ya Mweka Hazina Mkuu wa CCM wakati ufisadi wa EPA unatokea...

that is all sir, I was just thinking...

sorry to bother you.

Hahahahahah,

M. M. M kuna msg hapo. Unadhani asingekufa mama Mbatia leo Ikulu ingekalika?
 
Yule dereva aliyehusika katika ajali ya Bi. Salome Mbatia na ambaye alikuwa ameajiriwa muda si mrefu kabla ya ajali ile na kutoweka kama mvuke na kutokomea kama "night crawler" wa matrix hakuacha hata vumbi? Hivi jina lake la kweli lilikuwa lile?

Huyu bwana alihusika na ajali ya Waziri ambaye kabla ya hapo aliwahi kushikilia nafasi ya Mweka Hazina Mkuu wa CCM wakati ufisadi wa EPA unatokea...

that is all sir, I was just thinking...

sorry to bother you.

is just thinking? No forgive us!
 
ni yule yule dereva yule ambae alikuwa ana drive mbele ya zito na FS ndio huyo huyo aliesababisha ajali mbaya kiasi kile.........
 
yeah.. ndiyo huyo huyo ambaye aliweza kutokomea hewani na hadi hivi sasa haijulikani anaishi kwenye msitu gani....
 
Na ni nani aliyesema kulikuwemo sh. 200 million kwenye gari lile? Zilisalimika hizo!

Oooh! tulivyo wasahaulifu waTanzania, na wala hatuulizi jambo!
 
Back
Top Bottom