Aliyesababisha kifo cha Danhi Makanga aliyewahi kuwa Mbunge na DC, jela miezi 6

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Misungwi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Misungwi leo Ijumaa Julai 27, 2018 imemhukumu kifungo cha miezi sita jela, Samwel Kawiche (24) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la uzembe uliosababisha kifo cha mkuu wa wilaya wa zamani, Danhi Makanga.

Kawiche aliyekuwa akiendesha gari lililogonga pikipiki aliyokuwa amepanda marehemu ambaye pia amewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bariadi, pia leseni yake imefungiwa kwa miaka miwili.

Katika ajali hiyo dereva wa pikipiki hiyo, Marco Hamisi mkazi wa Kijiji cha Nyang’omango pia alifariki dunia.

Akitoa hukumu hiyo leo hakimu mkuu mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Marley amesema mahakama imefikia uamuzi huo baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo katika tukio lililotokea Juni 23, 2018 katika barabara kuu ya Mwanza Shinyanga eneo la Nyashishi kijiji cha Nyang’omango.

“Kutokana na kukiri kosa mahakama imekuhumu kwenda jela miezi sita na kuifungia leseni yako kwa miaka miwili ili iwe fundisho kwako na madareva wengine wanaoendesha magari kwa uzembe na kusababisha ajali zinazosababisha vifo na watu kupata majeraha,” amesema.

Awali, mwendesha mashtaka wa polisi, Ramsoney Salehe ameileza Mahakama kuwa mshtakiwa aliendesha gari kwa uzembe akitokea kijiji cha Usagara kwenda jijini Mwanza kwa kuigonga pikipiki na kusababisha kifo cha abiria na mwendesha pikipiki.

“Kosa hili ni kinyume cha kifungu cha 40 na 63 (2) (27) cha sheria ya usalama Barabarani sura ya 163 Iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002,”amesema Salehe.

Akijtetea kabla ya hukumu katika shauri hilo la jinai namba 19/ 2018 mshitakiwa ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa hilo ni kosa lake la kwanza.

Chanzo: Mwananchi
 
Miezi sita mbona michache hapo kwenye leseni hakitoka, huo mwaka mmoja na nusu sijuhi atafanya shughuli gani? kama lazoea kuendesha gari
 
Kweli kifo cha ajali barabarani utadhani haki haikutendeka !
 
Hivi alikuwa anaendesha mwenyewe?
Ndio alikuwa anaendesha mwenyewe usiku wa manane akitoka maisha club nasikia wale wadada walikuwa machangu na walimwacha kwenye mataa ndipo alipowafuatilia na kuwaona wamepanda bajaj kwa hasira akaigonga hiyo bajaj na kibaya zaidi gari lake halikuwa na hata bima,lakini kwa kuwa ni alikuwa mwenyenchi akaishia kulipa faini.Pia kuna mwingine baba yake (babu)alikuwa ndio wenye TANU na CCM kabla hajamfuata mamvi na hatimae kufariki mwaka huu,mtoto wake nae alikuwa zama zile msichana akimkataa basi aidha atamgonga na gari au kuwazaba vibao demu na jamaa yake,kwa mara ya mwisho aliachwa solemba na mrembo mpenda matajiri huyu mlimbwende alikuwa amevishwa kabisa pete lakini akaingia mitini na mzungu kutoka nchi zilizokuwa za kijamaa ambaye alikuwa mmiliki wa kamari,jamaa akikaa wakati wote anapepesa pepesa macho. na anahela chafu kwa sasa mrembo wake huyo aliyevishwa pete kaolewa na babu tycoon
 
Ndugu Mbona unaandika kwa uoga hivyo..!?

Maana umeandika kwa mifano kama masihi kwenye biblia
 
Ndio alikuwa anaendesha mwenyewe usiku wa manane akitoka maisha club nasikia wale wadada walikuwa machangu na walimwacha kwenye mataa ndipo alipowafuatilia na kuwaona wamepanda bajaj kwa hasira akaigonga hiyo bajaj na kibaya zaidi gari lake halikuwa na hata bima,lakini kwa kuwa ni alikuwa mwenyenchi akaishia kulipa faini.Pia kuna mwingine baba yake (babu)alikuwa ndio wenye TANU na CCM kabla hajamfuata mamvi na hatimae kufariki mwaka huu,mtoto wake nae alikuwa zama zile msichana akimkataa basi aidha atamgonga na gari au kuwazaba vibao demu na jamaa yake,kwa mara ya mwisho aliachwa solemba na mrembo mpenda matajiri huyu mlimbwende alikuwa amevishwa kabisa pete lakini akaingia mitini na mzungu kutoka nchi zilizokuwa za kijamaa ambaye alikuwa mmiliki wa kamari,jamaa akikaa wakati wote anapepesa pepesa macho. na anahela chafu kwa sasa mrembo wake huyo aliyevishwa pete kaolewa na babu tycoon
Nimeshamjua huyo nasikia aliwahi kumuua mwanamke mzungu,nasikia pia zamani alikuwa anamgegeda huyu mke wa saizi wa mzee machache bosi wa pipi midia na ayitivi,eti anapepesa macho haaaa
 
Ndio alikuwa anaendesha mwenyewe usiku wa manane akitoka maisha club nasikia wale wadada walikuwa machangu na walimwacha kwenye mataa ndipo alipowafuatilia na kuwaona wamepanda bajaj kwa hasira akaigonga hiyo bajaj na kibaya zaidi gari lake halikuwa na hata bima,lakini kwa kuwa ni alikuwa mwenyenchi akaishia kulipa faini.Pia kuna mwingine baba yake (babu)alikuwa ndio wenye TANU na CCM kabla hajamfuata mamvi na hatimae kufariki mwaka huu,mtoto wake nae alikuwa zama zile msichana akimkataa basi aidha atamgonga na gari au kuwazaba vibao demu na jamaa yake,kwa mara ya mwisho aliachwa solemba na mrembo mpenda matajiri huyu mlimbwende alikuwa amevishwa kabisa pete lakini akaingia mitini na mzungu kutoka nchi zilizokuwa za kijamaa ambaye alikuwa mmiliki wa kamari,jamaa akikaa wakati wote anapepesa pepesa macho. na anahela chafu kwa sasa mrembo wake huyo aliyevishwa pete kaolewa na babu tycoon
Hivi umuhimu wa gari kuwa na bima ni nini?
 
Kesi za matajiri zinatembea kwa kasi sana 23 juni 2018.Imekwisha 27/8/2018
Walala hoi wanaozea jela kwa uchunguzi baaaaaaaado hujakamilika mwaka wa kumi sasa. Reference ANORD KILINDO.
 
Back
Top Bottom