Aliyepika data za UVCCM achukuliwe hatua za Kisheria ndani ya chama chetu

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,774
2,000
Huyu aliyehusika kupika data za wanachama halisi wa uvccm anapaswa kuadhibiwa chino ya sheria na kanuni za chama. Anapaswa kuhojiwa na chama aeleze alikuwa ana nia gani kufanya hivo.
Nawasilisha
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,894
2,000
Amesifiwa na Sizo kawajibu waliobeza kuhusu kuwaachia huru waliohukumiwa kunyongwa!!! Anasema hajamtuma ila amejiongeza
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
37,351
2,000
Msando kaingia na kuwaumbua..... sidhani uccm wanamwangalia vizuri.

Halafu nadhani Msando na wenzake wa upinzani hawajaambiwa sio kila kitu kinachosemwa jukwaani ukweli. Wakati Msando anasema hivyo kama uliangalia vizuri alizua taharuki kuanzia meza kuu mpaka wajumbe wote. Kwa ujumla kile alichosema hakikuwafurahisha, wengi wameona analeta mambo ya upinzani kuongea kila kitu hadharani. Akumbuke juzi Polepole alikuwa anaongea kwa madaha kwamba ccm sasa hivi ina wanachama 12,000,000 nchi nzima. Sasa kwa haraka haraka hiyo idadi aliyosema ya milioni 6 kwamba sio kweli toa kwenye ile 12m utaona zaidi ya nusu haipo. Hapo ni jumuiya moja imepika idadi kubwa hivyo. Kiuhalisia ccm sidhani kama ina wanachama hai zaidi ya milioni 3 nchi nzima.

Machali naye alitoa angalizo kwamba vijana wa ccm wajue siasa sasa hivi imehamia kwenye mitandao ya kijamii lakini hawaoni vijana wa ccm wakijibu hoja. Sasa tujiandae kuwaona vijana wa ccm wakiingia humu jukwaani kama nyuki. Si vibaya wakija lakini watakuja na hoja hapo ndio ngoma. Kuanzia kesho j3 na kuendelea tutegemee kuona id mpya nyingi zikishusha mashambulizi na nyingine za zamani zikianza kazi tena.. Ni kwa muda gani watajibu hoja ni muda utaamua. Na vile mwenyekiti wa ccm kasema wasiogope kujibu hoja za wapinzani tunatarajia kuona mikutano ya siasa ikiruhusiwa ili tuone ushindani wa siasa.
 
ZILLAHENDER MPEMA

JF-Expert Member
Apr 4, 2015
2,059
2,000
Huyu aliyehusika kupika data za wanachama halisi wa uvccm anapaswa kuadhibiwa chino ya sheria na kanuni za chama. Anapaswa kuhojiwa na chama aeleze alikuwa ana nia gani kufanya hivo.
Nawasilisha

Kupika data ni moja ya sifa za msingi za ccm na serikali yake na serikali na taasisi zake zote.Kama NEC ilipika data ili kuipa ccm ushindi,unashangaa nini uvccm kupika data?

FB_IMG_1506492005604.jpg
 
Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,774
2,000
Halafu nadhani Msando na wenzake wa upinzani hawajaambiwa sio kila kitu kinachosemwa jukwaani ukweli. Wakati Msando anasema hivyo kama uliangalia vizuri alizua taharuki kuanzia meza kuu mpaka wajumbe wote. Kwa ujumla kile alichosema hakikuwafurahisha, wengi wameona analeta mambo ya upinzani kuongea kila kitu hadharani. Akumbuke juzi Polepole alikuwa anaongea kwa madaha kwamba ccm sasa hivi ina wanachama 12,000,000 nchi nzima. Sasa kwa haraka haraka hiyo idadi aliyosema ya milioni 6 kwamba sio kweli toa kwenye ile 12m utaona zaidi ya nusu haipo. Hapo ni jumuiya moja imepika idadi kubwa hivyo. Kiuhalisia ccm sidhani kama ina wanachama hai zaidi ya milioni 3 nchi nzima.

Machali naye alitoa angalizo kwamba vijana wa ccm wajue siasa sasa hivi imehamia kwenye mitandao ya kijamii lakini hawaoni vijana wa ccm wakijibu hoja. Sasa tujiandae kuwaona vijana wa ccm wakiingia humu jukwaani kama nyuki. Si vibaya wakija lakini watakuja na hoja hapo ndio ngoma. Kuanzia kesho j3 na kuendelea tutegemee kuona id mpya nyingi zikishusha mashambulizi na nyingine za zamani zikianza kazi tena.. Ni kwa muda gani watajibu hoja ni muda utaamua. Na vile mwenyekiti wa ccm kasema wasiogope kujibu hoja za wapinzani tunatarajia kuona mikutano ya siasa ikiruhusiwa ili tuone ushindani wa siasa.
Kweli tupu
 
Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,250

Nani kasema vijana wa ccm hawapo kwenye mitandao?? Tunao humu siku zote ila hawawez jibu hoja za wapinzani.

Unamuuliza Kijana wa ccm, nyie mlimtukana Lowassa aliposema akiwa Rais atawaachia hutu akina Babu Seya, Leo JPM kawaachia huru je yale matusi yenu yamhusu pia JPM? Hapo unataka Kijana wa ccm ajibu nini?

Unamuuliza mnajinasibu mnapambana na Rushwa. Je ni kina nani waliochota fedha za escrow kwenye sandarusi pale standbic?? Hapa Kijana wa ccm unataka ajibu nini?? Vijana wa ccm wapo kimya kwa sababu hawana majibu ya maswali magumu toka kwa wananchi/wapinzani.

Kama mwenyekiti taifa wa chama hana majibu, atajibu mwanachama wa umoja wa vijama wa ccm?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom