Aliyepigwa risasi ya muro atoboa siri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyepigwa risasi ya muro atoboa siri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bujibuji, Mar 23, 2010.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,359
  Likes Received: 22,221
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  YADHIHIRIKA MURO ANATEMBEA NA KIFO MKONONI, ALAZIMIKA KUISHI MAFICHONI
  Yule Daktari aliyepigwa risasi iliyomkosa mtangazaji wa habari za uchunguzi wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC1) Jerry Muro, Dk. Paul Andrew ametoboa siri kwa kusema kuwa kitendo chake cha kujeruhiwa mguuni kwa risasi ni njama za wazi zilizofanywa na wabaya wao...
  Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Dk. Andrew alitoboa siri kuwa ana undugu na Jerry, na kuongeza kwamba amekuwa akijijengea maadui na wafanyakazi wa taasisi moja (jina tunalihifadhi) ambao wamekuwa wakikiuka maadili ya kazi ya udaktari na kila anapowaonya, anageuka kuwa adui kwao.
  [​IMG]

  “Naweza kusema wazi kwamba wafanyakazi hao ambao wana kawaida ya kufanya kazi kinyume cha maadili, huniona adui yao kila ninapokwenda kuwaonya, naweza kusema wanahusika na njama za kutaka kuniua na kunizushia mambo ya hatari katika jamii, japokuwa pia inawezekana nia ya wadunguaji ilikuwa kumpata Jerry,” alisema Dk. Andrew.

  Akifafanua zaidi Daktari huyo ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya binadamu alisema siku ya tukio Machi 12, mwaka huu akiwa na Jerry, alishangazwa kuona gari moja dogo lenye rangi ya fedha (Silver) likiwapita kwa kasi wakiwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu alikokwenda kwenye kesi ya ndugu yake huyo (Jerry Muro).
  Alisema walikuwa nje ya mahakama na wakati huo walikuwa wakipanga kwenda kumuona mwanasheria, lakini ghafla gari lilipita na tukio hilo likatokea.

  “Lile gari tuliligutukia baada ya mimi kupigwa risasi mguuni na kuanguka, tukaliona linakwenda kwa kasi huku nikiachwa nikivuja damu nyingi sana na wakati huo huo risasi ikiwa imetoboa kiatu na kuingia mwilini mwangu, mguu wa kushoto,” alisema Dk. Andrew.

  Alisema mara baada ya kitendo kile na kujikuta akiwa chini, watu walikusanyika lakini ndugu zake wakamkimbiza Hospitali ya Marie Stopes anakofanyia kazi kwa gari alilokuwa akiendesha Jerry na baada ya kufika na kufanyiwa uchunguzi, madaktari walisema mshipa wa damu ulikatika ndiyo maana alikuwa akivuja damu nyingi.
  Alifafanua kwamba madaktari hao walimshona jeraha na akalazwa hapo, hivyo huwa analitafakari tukio hilo ambalo hadi sasa linamtia hofu na woga mkubwa.

  Hata hivyo, baadhi ya ndugu wa Andrew na Jerry Muro waliozungumza na gazeti hili kwa masharti ya kuhifadhi majina yao walisema kuna kila dalili kwamba aliyekuwa akiwindwa siku hiyo kumalizwa ni Jerry na sasa anatembea na kifo mkononi.

  “Tuna wasi wasi mkubwa na ndugu yetu kwa sababu waandishi wengi duniani wanaofanya kazi za uchunguzi huishia pabaya, hapa nchini tulikuwa na Bw. Stan Katabalo ambaye alifichua kashfa ya Loliondo, kifo chake kilikuwa ni cha kutatanisha, tuna mashaka Jerry wanaweza kumfanya hivyo hivyo,” alisema mmoja wa ndugu hao.

  Aidha, ndugu huyo alionesha wasiwasi wake kwa jeshi la polisi kuwa hata kesi ambazo Jerry aliwahi kuziripoti polisi kwa kufungua majalada, hakuna kilichofanyika hadi sasa, hali wanayoitafsiri kuwa wanasusa masuala ya ndugu yao kwa kuwa tu alianika uozo wa polisi wa usalama barabarani.

  Jerry aliwahi kufungua kesi tatu tofauti katika Kituo cha Oysterbay na Kituo Kikuu cha Polisi kutokana na kushambuliwa na kuibiwa laptop iliyokuwa na kumbukumbu muhimu lakini kesi zote ‘zimeganda’ katika vituo hivyo vya usalama wa raia.

  Gazeti hili liliwahi kuzungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile kuhusiana na kesi hizo lakini akasema RB namba OB/RB/1855/2009 (Wizi wa Laptop) ipo Kituo cha Oysterbay hivyo hawezi kujua kinachoendelea huko wakati shauri namba CD/ IR/148171 (shambulio) na CD /RB/ 15133/2009 zipo Kituo Kikuu cha Polisi, akaahidi kufuatilia.

  SOURCE:- SHIGONGO'S WEBSITE
   
 2. E

  Elson Makaye Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salam wanafamilia

  Ukweli jamani haya mambo yanasikitisha sana. Kuna wakati najiuliza, hivi tunakoelekea ni wapi? na wajibu wetu ni nini?

  Sote tunapaswa kutambua kuwa, Muro yamemkumba haya leo, kesho yamkini itakuwa kwa mwingine miongoni mwetu kwa namna ya tofauti, then what is our role to play in this corrupt country to make things move in the right direction?
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,359
  Likes Received: 22,221
  Trophy Points: 280
  Kwani huyu jerry muro ana siri gani nzito mpaka roho yake iwe bei juu kiasi hiki??
   
 4. Soulbrother

  Soulbrother JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 408
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Now this is the right QUESTION!!!!!!
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  MMMH hii kesi iishe tutajione mambo na kusikia mengi
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Lakini inasemekana Shigongo huwa anaandika habari za uongo sijui anazitoa wapi?
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamaa Jerry ni Kainzi, ana siri nzito sana pengine za kutikisa baadhi ya taasisi na taifa!!! Ndiyo maana waliiba ile laptop na sijui kama alikuwa na back up!! I hope kwa usalama wa taarifa zake ni lazima awe na back up!!

  Pia ni kwamba kwa jinsi alivyokuwa anafanya kazi angepaswa zaidi kuajiriwa private media na si hii ya Taifa kwani masuala mengi ya kijamii yanagusa zaidi viongozi wake au uzembe fulani na wahusika hawatakubali kupoteza unga wao!!! Including mwajiri wake kwani naye atakuwa anatumikia interest fulani. Nasisitiza, Jerry ulifanya makosa sana kuingia ajira ya serikali/utumishi wa umma!! Take it from me!!
   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  POLICE WANA HABARI HII AU NI MURO, DAKTARI NA ShIGONGO TU?
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  yetu macho tu! only the strongest will survive (Darwin)
   
 10. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mbona hiyo risasi iliyomkosa ilikuwa ni mchana kweupe..
  Saa hizi jamaa hasikilizwi tena na polisi..
  Bhita ni bhita.....
   
 11. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tunakwenda wapi wa-tz
   
 12. domokrasi

  domokrasi Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 27, 2006
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Picha ya pili kama iko photoshopped vile!
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,853
  Trophy Points: 280
  Mbona magazeti mengine hayaandiki hii khabari?
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Habari nina wasiwasi nayo, mbona umereportiwa kwenye gazeti Moja?? ina mana waandishi wa Shigongo ndo walikuwa pale??

  I support you huku amekosea njia, ushauri wako mzuri najua Jerry yuko humu humu atakuwa amekupata

  Mimi nina wasiwasi na habari hii ni ya kupika
   
 15. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani kweli tumefikia kiasi huku. Mchana kweupe risasi pu! Halafu hakuna hata taarifa za kufuatilia hilo gari na foleni za hapa Dar?
  Sitaki kudoubt hili tukio lakini uchunguzi makini unatakiwa isijekuwa mzee alijifyatua mwenyewe (si kwa makusudi lakini bahati mbaya - ajali). Huwa inatokea ingawa si kawaida pia.
   
 16. N

  Nanu JF-Expert Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Lakini, mbona hawajasema kama imeripotiwa polisi na jalada kufunguliwa?
  Hii habari ya Shigongo in ukweli?
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli mkuu kishindo cha silaha pale mahakama ya kisutu na waandishi wa habari tele kweli wasiripoti tukio hilo. Tena hapa jamii ingekuwa breaking news instantly. I also doubt the source of this sijui tuiite tetesi au uvumi au udaku au nini tena.....!!! Au hiyo silaha ni silencer!!!!! Sina hakika jamani, du!!!

  Halafu break ya kwanza unakimbiza victim Marie Stopes badala ya Muhimbili ni karibu na kwa case zile ni muafaka kabisa!!! Anyway, nachangia tu ila kwa kweli magazeti ya global publishers nilishayapiga chini!!!
   
 18. kisasangwe

  kisasangwe JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 294
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ukweli ni upi jamani????
  mbona hili tukio sijalisikia hata kwa magazeti mengine,au kwa vile sisomi magazeti sana?
   
Loading...