Moshi: Aliyepigwa kwa kudaiwa kufumaniwa amliza Mkuu wa Mkoa

Basi tufanye ni kweli.
Sasa, mnadhani basi hata kama ni kweli.... Je, ule udhalilishaji alio fanyiwa ni adhabu sahihi?
Hata basi Kama ni adhabu sahihi, je huyo mwalimu anahaki ya kumuhukumu ama kuadhibu mwenye makosa?
Mkuu naomba link ya video
 
Huyu mwanamke nilikataa kumuamini tangu naiona ile vidio haya ona sasa kabadirisha alichokiri mwenyewe

Acheni kutembea na wake/waume za watu mtapigwa sana

Hongera Agnes kwa kumshughulikia huyo mwizi
Hongera zake na sasa ni muda wake kushuhulikiwa. Sijui na mumewe alimshuhulikia? Agness ajiandae kula ugali wa bure.
 
Mwanaharakati wa Haki za Wanawake hapa nchini Joyce Kiria the super woman pamoja na Juma Raibu diwani wa Boma Mbuzi Manispaa Moshi wamsaidia mwanamke aliye daiwa kufumaniwa na mume wa mtu kupata matibabu

Akizungumza Mara baada kutembelewa nyumbani kwake Msaranga wilani Moshi Mkoani Kilimanjaro mwanamke Huyo Venna Esau Kimaro amesema kwamba Kwa jitihada za Joyce na Raibu zimefanikisha yeye kupata matibabu Mara baada kufuatilia jambo hilo kwa umakini na ukaribu zaidi

Amesema kwamba Joyce na Diwani huyo walifika kwa mwenyekiti wa kamati ya ulizi na usalama Mkoa kilimanjaro ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira na kumtembelea nyumbani kwako eneo la Msaranga Moshi Kilimanjaro kwa lengo la kumjulia hali na baadae kuagiza kupelekwa hospital ya Rufaa Mawezi kupata matibabu ambapo ameagiza mganga mkuu kumuhudumia mpaka apone

Venna alikanusha mbele ya mkuu wa mkoa na kamanda wa polisi wa mkoa wa kilimanjaro kwamba akufumaniwa na mume wa mtu Bali kilicho jitokeza Kwa mwanamke Huyo ni kumvamia wakati akiwa eneo la nyumba ya Biashara Bar akiwa na mwanaume uyo wakipanga biashara ya kumpangishia eneo la kufanyia biashara ya vinywaji bar

Amesema kwamba bila kuulizwa chochote alivamiwa na mwanamke alijulikana kwa jina la Agnes Mushi ambaye pia ni Mwalimu wa Shule binafsi itwayo Norther Highland iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro

Wakati naendelea kuongea na mwanamke huyo alinivamia na kuanza kunipiga huku akishirikiana na mwezie walinipiga na kunivua Nguo zote na kubaki uchi na kunipigia Picha za video nikauliza kosa langu nini na kusema kwamba natembea na mwanaume wake jambo ambalo sio kweli nilikua na mazungumzo na Huyo bwana Juu ya kufungua Biashara ya bar na kusema kwamba mwalimu huyo pia alimwibia fedha kiasi cha shilingi laki Tisa na elfu saba alisema Venna

Mara baada ya kueleza tukio hilo alipelekwa hospital na gari la Polisi huku kamanda Polisi Mkoa Kilimanjaro aliwataka watuhumiwa kujitokeza kwani tuko hilo ni la jinai na msako wa kuwatafuta walipo kimbilia mwanamke Huyo na mumewe unaendelea

Amesema walio husika katika tuko hilo kumdhalilisha mwanamke huyo na kumpiga video wote watakamatwa na kuwaonya wananchi kujichukulia Sheria mkononi

Kwa upande wa mkuu wa mkoa amewataka Wanawake kuacha tabia ya kuisi Wanawake mwezao kwamba muda wote wakiwa na wanaume wanaendekeza mapenzi kwani kilicho tokea Kwa Mwananchi Huyo sio fumanisi Bali ni mazungumzo ya kibiashara

Mkuu wa Mkoa ameagiza Polisi kuwatafuta watuhumiwa wote wawili usiku namchana na kufikishwa mahakamani na kujibu tuhuma za kumpiga na kuzalilishaji ktk mitandao ya kijamii



View attachment 1459485View attachment 1459486View attachment 1459487View attachment 1459488View attachment 1459489

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni movie inachezwa hamna jipya hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BI DADA Atajitetea vizuri tu kwamba alikubali ana uhusiano na yule jamaa ili asiendele kupigwa..Kitendo cha kumpiga kimewafunga hawa kama wangemhoji tu akakiri ingekua sawa kabisa.

Walimpompa kichapo hapo ndio amejichukulia point 3 zote.. Joyce kiria ameshapata kanafasi amesafiri mpaka Moshi duh...
Mkuu ulitaka asisafiri wakati nauli ni yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanavyomtetea sasa wakati hapo mke anasota na watoto wake huko unazani mkewe anakuwa kwenye hali gani mme anatamba huko na mahawala mke unalala njaa, ndiyo hao kina Baba watoto akikua na kuwa na maisha yao mazuri wanaanza shenzi kabisa, wanao msaidia wenyewe ndoa zao zilishazikwa zamani wanataka na mwenzao ndoa yake isambaratike Mwl tafuta nawewe mawakili wakusaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muonekano tu wa huyo wanaemtetea unatia mashaka haya kaiba bwana wa mtu leo anakuja na drama ya kumuibia tena hela Agnes kupitia visheria koko

Na ukiangalia wengi wanaotetea hapa ni wachepukaji na inabidi wajue ukikamatwa na AGNES either utatinduliwa mtaro ikiwezekana mtungo kabisa au kipigo heavy

Hatuhalalishi uzinzi hongera AGNES we ni shujaa
 
Hongera zake na sasa ni muda wake kushuhulikiwa. Sijui na mumewe alimshuhulikia? Agness ajiandae kula ugali wa bure.
Bado haifuti kuwa Agnes ni shujaa, unakuta mke/mm3 wako anapiga/anapigwa mambo halafu utulie tu huo ni ubwege kiwango cha SGR mzee na alichokifanya AGNES si chaajabu hivyo ndio wachepukaji huwa wanatendewa huku kitaa


Jela hata mashujaa hukaa rejea kwa MANDELA sasa ni shujaa AGNES
 
Mwenyewe kasema mwanaume huyo kamwambia hana.mke, na walifika pale usiku, na kama sio hawala yake kwanini huyo mwanaume alikimbia? Kama alikuwa ni mbia mwenzie kwenye biashara kwanini alikimbia msituchoshe kama walishatifuana atulie tu

Sent using Jamii Forums mobile app
May be alkua anaokoa nafsi yake, kipigo kilikua kikali ili asije hata kuuliwa ilibidi ajitetee vile, mwanaume alikimbia sababu walipanga na mke wake wamwibie huyu dada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siungi mkono udhalilishaji alofanyiwa.Nataka kuamini huyu dada ni kweli amechukua Mme wa mtu.Kulingana na ile clip.Japo kwenye mahojiano ana kana.Sasa kama ni kweli walikua wanafanya issue za biashara alikua anamuuliza huyo mwanaume kama ana mke ili agundue nini.Kuna kitu hakijakaa Sawa hapa.Au labda aina ya biashara walotaka wafanye ilikua haihitaji mtu aliepo kwenye ndoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyovyote vile lakini haimoi uhalali wa mwenye mke kumpiga na kumjeruhi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha sheria ichukue mkondo wake alifumaniwa hakufumaniwa haijalishi kwa namna walivyompiga na kumdhalilisha waende wakapambane magereza kwa walioazima akili maana watawatenda kweli

Mwanaume akicheat tambua kuna mahali unakosea kama Mama Mwenye Nyumba
Ona sasa wawili hao wanaishi kama digidigi

Kucheat ni uamuzi wa mtu sio lazima mwenza wako awe anakosea kitu fulani. Unaweza kuwa malaika na bado mtu akacheat.
 
Kweli duniani inakimbia, wachaga mnaanza kugombea wanaume and not money

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli ni kwamba Mwanaume/Mme ndiyo kila kitu kwenye familia, ila wanawake hawataki kukiri tu, infact naona mtuhumiwa ana bahati sana, nisingeshangaa kama angetolewa maisha kabisa, wanawake hatari sana wakichukuliwa utamu wao...
 
Jitu linalobadiri badiri maneno kama kinyonga linastahili kabisa kibano

Kutetea jitu linalolala na mke/mme wa mtu ni kuhalalisha uzinzi

Yeye si wa kwanza kutendewa hivyo vitu na ndio mfumo wa maisha yetu watizedi yani hivi vihuruma huruma vya hawa wakina KIRIA ambao ndoa zimewashinda tutaharibu jamii... Aachwe augulie kwasababu hayo ndio malipo ya uzinzi


Huyoo dada alimbaka huyoo mume wa mtu??? Yani mwanaume amtongoze huyoo dada ampeleke adi nyumbani anapoishi walale alafu ujee usemee huyoo mfumaniwa ndo anamakosa??? Kwanini asingemdhalilisha na mumewe??
 
Back
Top Bottom