Moshi: Aliyepigwa kwa kudaiwa kufumaniwa amliza Mkuu wa Mkoa

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Mwanaharakati wa Haki za Wanawake hapa nchini Joyce Kiria the super woman pamoja na Juma Raibu diwani wa Boma Mbuzi Manispaa Moshi wamsaidia mwanamke aliye daiwa kufumaniwa na mume wa mtu kupata matibabu

Akizungumza Mara baada kutembelewa nyumbani kwake Msaranga wilani Moshi Mkoani Kilimanjaro mwanamke Huyo Venna Esau Kimaro amesema kwamba Kwa jitihada za Joyce na Raibu zimefanikisha yeye kupata matibabu Mara baada kufuatilia jambo hilo kwa umakini na ukaribu zaidi

Amesema kwamba Joyce na Diwani huyo walifika kwa mwenyekiti wa kamati ya ulizi na usalama Mkoa kilimanjaro ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mama Anna Mghwira na kumtembelea nyumbani kwako eneo la Msaranga Moshi Kilimanjaro kwa lengo la kumjulia hali na baadae kuagiza kupelekwa hospital ya Rufaa Mawezi kupata matibabu ambapo ameagiza mganga mkuu kumuhudumia mpaka apone

Venna alikanusha mbele ya mkuu wa mkoa na kamanda wa polisi wa mkoa wa kilimanjaro kwamba akufumaniwa na mume wa mtu Bali kilicho jitokeza Kwa mwanamke Huyo ni kumvamia wakati akiwa eneo la nyumba ya Biashara Bar akiwa na mwanaume uyo wakipanga biashara ya kumpangishia eneo la kufanyia biashara ya vinywaji bar

Amesema kwamba bila kuulizwa chochote alivamiwa na mwanamke alijulikana kwa jina la Agnes Mushi ambaye pia ni Mwalimu wa Shule binafsi itwayo Norther Highland iliyopo Moshi Mkoani Kilimanjaro

Wakati naendelea kuongea na mwanamke huyo alinivamia na kuanza kunipiga huku akishirikiana na mwezie walinipiga na kunivua Nguo zote na kubaki uchi na kunipigia Picha za video nikauliza kosa langu nini na kusema kwamba natembea na mwanaume wake jambo ambalo sio kweli nilikua na mazungumzo na Huyo bwana Juu ya kufungua Biashara ya bar na kusema kwamba mwalimu huyo pia alimwibia fedha kiasi cha shilingi laki Tisa na elfu saba alisema Venna

Mara baada ya kueleza tukio hilo alipelekwa hospital na gari la Polisi huku kamanda Polisi Mkoa Kilimanjaro aliwataka watuhumiwa kujitokeza kwani tuko hilo ni la jinai na msako wa kuwatafuta walipo kimbilia mwanamke Huyo na mumewe unaendelea

Amesema walio husika katika tuko hilo kumdhalilisha mwanamke huyo na kumpiga video wote watakamatwa na kuwaonya wananchi kujichukulia Sheria mkononi

Kwa upande wa mkuu wa mkoa amewataka Wanawake kuacha tabia ya kuisi Wanawake mwezao kwamba muda wote wakiwa na wanaume wanaendekeza mapenzi kwani kilicho tokea Kwa Mwananchi Huyo sio fumanisi Bali ni mazungumzo ya kibiashara

Mkuu wa Mkoa ameagiza Polisi kuwatafuta watuhumiwa wote wawili usiku namchana na kufikishwa mahakamani na kujibu tuhuma za kumpiga na kuzalilishaji ktk mitandao ya kijamii


IMG_20200525_134350_9.jpg
P1100213.JPG
IMG_20200525_145230_7.jpg
IMG_20200525_145442_2.jpg
Screenshot_20200525-180359.jpg


Pia soma hapa

VIDEO: Fumanizi na kipigo kikali sana

Kilimanjaro: Mwanamke aliemfumania mwanamke mwenzake na kumpiga azungumza mazito
 
Mbona kwenye video yeye mwenyewe anakiri kuwa huyo Mwanaume alimwambia kuwa hajaoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nami nilipo soma nimeona kajichanganya, na inavyoonesha katika zile video za vipigo yeye mwenyewe alikiri kuwa na mahusiano na yule mume wa mtu ila alidanganywa hajaoa..

Huyu Dada ni mwongo kwa haraka haraka inavyoonekana, na katika video alikuwa katika nyumba ya huyo bwana ambayo anaishi na mke ambaye alifanya fumanizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha sheria ichukue mkondo wake alifumaniwa hakufumaniwa haijalishi kwa namna walivyompiga na kumdhalilisha waende wakapambane magereza kwa walioazima akili maana watawatenda kweli

Mwanaume akicheat tambua kuna mahali unakosea kama Mama Mwenye Nyumba
Ona sasa wawili hao wanaishi kama digidigi
 
Nami nilipo soma nimeona kajichanganya, na inavyoonesha katika zile video za vipigo yeye mwenyewe alikiri kuwa na mahusiano na yule mume wa mtu ila alidanganywa hajaoa.. Huyu Dada ni mwongo kwa haraka haraka inavyoonekana, na katika video alikuwa katika nyumba ya huyo bwana ambayo anaishi na mke ambaye alifanya fumanizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bwawa limeshaingia luba...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nami nilipo soma nimeona kajichanganya, na inavyoonesha katika zile video za vipigo yeye mwenyewe alikiri kuwa na mahusiano na yule mume wa mtu ila alidanganywa hajaoa.. Huyu Dada ni mwongo kwa haraka haraka inavyoonekana, na katika video alikuwa katika nyumba ya huyo bwana ambayo anaishi na mke ambaye alifanya fumanizi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio tu muongo, hapo ameshauriwa amkomeshe yule aliyemdharirisha, hapo inatengenezwa mazingira alipwe


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nami nilipo soma nimeona kajichanganya, na inavyoonesha katika zile video za vipigo yeye mwenyewe alikiri kuwa na mahusiano na yule mume wa mtu ila alidanganywa hajaoa.. Huyu Dada ni mwongo kwa haraka haraka inavyoonekana, na katika video alikuwa katika nyumba ya huyo bwana ambayo anaishi na mke ambaye alifanya fumanizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna ukili wa mtu akiwa ndani ya pressure huo hatuuhesabu kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom