Aliyepiga picha na Simba akalia kuti kavu,Mamlaka za uhifadhi zatishia kumnyang'anya leseni

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,828
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg

Hii picha imezua utata sana kwenye mitandao ya Kijamii...Huyu jamaa anaweza kupokwa leseni ya kuongoza Watalii huko Afrika Kusini,sababu huyo Simba ni hayawani sio timamu kwamba unajenga nae urafiki.Kampuni na Hotel anayofanyia kazi imejitahidi sana kuomba radhi....Jamaa ni mfanyakazi wa Lodge iliyopo kwenye hifadhi inaitwa Tintswalo Safari Lodge

.Maana picha hii inaweza kusababisha watu wengi na hasa watalii wanaopenda kuweka kumbukumbu wadhani nao wanaweza kupiga picha ya namna hiyo...Hii ndio ilitokea kule Marekani mtoto akabebwa na Gorilla matokeo yake mnyama akauwawa,Leo China Tiger kauwa bibi mmoja na kujeruhi wanafamilia....Huyu si "temed lioness" kwamba amefunzwa kukaa na binadamu.

Huyo jamaa anaitwa Eric!!Kakalia kuti kavu kwa picha hii,Mamlaka za Uhifadhi wa Wanyama wametoa karipio kali sana na kuchukuwa hatua za kiuchunguzi kabla ya kuchukua hatua dhidi ya jamaa.Maana imeonekana kama jamaa alifanya hivyo ili "kuwapendeza watalii".Tukio hili lilitokea katika sehemu ya "Manyaleti Game Reserve" iliyo katika eneo la Kruger National Park,Afrika Kusini.

Tintswalo Safari Lodge imetoa Press Release wanasema

"Eric (the tracker) comments that he "enjoyed the experience and knew the lion was going to walk past without harming him - he knows the lion is relaxed he has been watching him since he was a baby and knows his behavior"

Eric has been watching these cubs since they were born and there is a bond between them. These lions are viewed everyday as they are our resident pride at Tintswalo Safari.Thank you all for the comments on social networks.Eric is a wonderful tracker and as mentioned above, TSL is not a zoo. We adhere to the highest standards of safety and respect of wildlife. Be rest assured that our staff and guests are never put into danger, nor is the wildlife ever compromised.

This was a well timed photograph - which can either tell a story or start one!"
Cc: Matola mxyo16
 
mbona Tanzania wanawauwa lakini serikali ya ccm inapiga makofi badala ya hatua?
 
View attachment 370917 View attachment 370915 View attachment 370916

Hapa nahisi colour inamponza. Though kiuhalisia atakua amevunja kanuni za kazi.....asa je anaweza ku prove ni bahati mbaya hakujua, au huwa wanafanya hako kamchezo kakuvunja hizo kanuni ila picha ime leak-ishwa na imemponza. ni sad story.
Kwahiyo imegeuka kua kesi ya kumchezea mnyama mkali dah! hizi rangi zetu hizi
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Kwanini wasingempa motivation kwa ujasiri aliouonesha?
Na tahadhari ingeendelea tu kuwekwa,DONT TRY THIS AT HOME.!
 
aahh mkuu, tatizo ni jamaa kuvunja kanuni za kazi na kujipatia umashuhuri kwenye kijiwe cha mzungu....angekua white ungeiona tu as a breaking news CNN
Kumbe huyu Simba anamfahamu tangu anazaliwa? Kuna tofauti gani na Simba wa kufuga?
 
Mkuu mnyama wa porini hata afugwe vipi huwa asili yake haipotei. Kuna watu wamewafuga hawa simba, tiger , chatu , sokwe, au yule mu australia aliekua anakamata mamba, wooote huwa wanabadilikiwa na kujeruhiwa au kuuawa.
Tafuta mikasa iliyowapata watu kama siegfried & roy, au steve Irwin..............wote hao walizijua tabia za wanyama vizuri tu ila walidhuriwa
 
Hovyo kweli hao jamaa, walitaka awe mzungu ili waseme watu weusi wajinga wanachokoza mnyama halafu wanasema ni mkali hatari. Ukoloni kuisha Afrika bado sana.
 
Maonevu tu
Nani asiejua simba hatari!
kama aliamua kufanya hivyo niyeye ns ujasiri wake tatizo nini!!
 
Umasaini kawaida. Simba mkazie macho,mwangalie moja kwa moja machoni. Ukicheka au kutabasamu,kuchezesha midomo,anajihami.
 
Nini Simba kijibwa chako koko tu kuna siku kinakubadilishia rangi mpaka unamwona israili anaku beep!
 
Back
Top Bottom