Aliyeongoza kidato cha Sita ni zao la shule za Kata

Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,793
1,083
1.jpg

Mwanafunzi aliyeongoza katika matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Hassan Gwaay ameonesha moja kati ya tunda bora lililodhihirisha faida ya kuanzishwa kwa shule za kata na Serikali ya awamu ya nne iliyoongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.

Gwaay mwenye umri wa miaka 19 ameeleza kuwa alisoma katika shule ya kata ya Mirerani Benjamin W. Mkapa mkoani Manyara alipopata elimu ya kidato cha nne na kupata ufaulu mzuri uliomuwezesha kuchaguliwa kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora (Tabora Boys) kuendelea na elimu yake ya kidato cha tano.

Amesema kuwa alipokuwa akisoma katika shule hiyo ya kata, wanafunzi waliokuwa wanasoma katika shule za watu binafsi zenye mazingira bora zaidi ya walikuwa wakimuonesha dharau lakini alitaka kuwadhihirishia kuwa hata katika shule hiyo anaweza kufanya vizuri zaidi yao.

“Sikujali kelele na dharau za watoto waliosoma kwenye shule za kulipia, ambao mara kwa mara walikuwa wakiibeza shule yetu. Nilopomaliza kidato cha nne, nilipata daraja la kwanza alama 10 (Division 1 ya point 10). Ndipo nilipowadhihirishia kuwa hata kwenye shule za kata watu wanafaulu,” Gwaay anakaririwa na gazeti la Jambo Leo.

Mwanafunzi huyo ambaye amelelewa na bibi yake kwa muda mrefu baada ya mama yake kufariki huku akiishi mbali na baba yake (anamsapoti), alisema kuwa baada ya kujiunga na shule ya wavulana ya Tabora kusoma masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), aliweka bidii zaidi hasa baada ya kugundua kuwa wanafunzi aliokutana nao hapo wote walikuwa na akili sana.

Alisema kuwa alipofanya mtihani wa ‘Mock’ alipata Fizikia (A), Kemia (A) na Hesabu (B) na kwaba aliumia sana kuona amepata B. Aliongeza bidi hadi kuibuka na alama A kwenye mitihani yote katika Mtihani wa Taifa na kutangazwa kuwa mwanafunzi aliyeongoza.

Changamoto ya upungufu wa walimu hususan wa Sayansi katika shule nyingi za umma nchini lilimkumba pia Gwaay katika shule ya wavulana ya Tabora, lakini aliipanda ngazi hiyo ndefu kwa nguvu ya ziada bila kukata tamaa.

“Hakuwa na Mwalimu wa Fizikia pale. Tangu najiunga sikuwahi kumwona zaidi ya wakuazimwa ambaye alikuwa akija jioni na mwisho mwa wiki tu na alikuwa akija mara chache. Muda mwingi tulitumia kujisome wenyewe lakini hatukukata tamaa,” alisema.

Shule ya wavulana ya Tabora mwaka huu imerudi kwenye nafasi yake ya ubora ulioaminika miaka mingi iliyopita. Imeshika nafasi ya 5 kati ya shule zote.

Kwa hisani ya MPEKUZI
 
Kijana pambana......chuo kikuu kinakusubir....na taifa lako hongera mwanaapolo.....
 
Nimeanza kufikiria labda kuna waliokuwa wameweka matumbo mbele kufelisha shule za kata, ili wao na wenzao waingize pesa zaidi ktk shule za binafsi

Nami naandika kama mwananchi ambaye nachokumbuka tu kwa miaka hii ya karibuni ni kusifika kwa watoto wa shule binafsi tu.
Jambo lipo...hata ile listi wow
 
Sipati picha kama angekuwa anatokea kanda ya Ziwa
Kuna kanda nyingi lakini umeona tu ya Ziwa. Hii inaonyesha unafahamu vichwa vya huko. Leo zamu yenu kutoa, kesho itakuwa yao, na kanda hiyo imeshazoea kutoa watu wa namna hiyo mara nyingi na ndiyo maana hata kiongozi wa nchi smart alitokea huko na sasa mnamuona aliyepo sasa hivi anafanana na yule wa kwanza kwa mambo mengi. Chezea Ziwa wewe?
 
wewe ndo mjinga,Lowasa ndio alibuni na kusimamia shule za kata.waulize wanaokutumia
Makamanda tuache kujipendekeza. Mfumo wa Elim ya Sekondari kwa kila kata ulinuniwa na Utawala wa Benjamin Mkapa. Walianza na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Baada ya kukamilika kwa mpango huo ndipo ulipoanza Mpango wa Maendeleo ya Shule za Sekondari (MMES) ambao ulianza kutekelezwa awamu ya mwisho ya Utawala wa Mkapa.

Ni upunguwani na uhayawani kudhani kuwa ni Lowasa ndiye aliyebuni shule za Kata. Kilichotokea ni kwamba kwa vile utawala wa Mkapa ulimaliza muda wake na Utawala wa Kikwete kuanza, kama ilivyo ada ya kupokezana kijiti, Kikwete na Serikali yake wakaanza kutekeleza MMES iliyobuniwa na Mkapa na serikali yake. Kwa Ujumla ni kwamba MMES ni jitihada za serikali ya CCM kufikisha elimu ya sekondari kwa kila mtoto. Sisi kazi yetu ni kujipendekeza tu na kuchukua yale mazuri ya CCM kuwa yetu na mabaya ya CCM kuwa yao
 
Back
Top Bottom