Hu
Huwezi kumtoa lowasa kwenye ujenzi wa shule za kata yeye ndie aliyesimamia mpango huo, kubuni mpango ni kitu kimoja na kuufanikisha ni kitu kingine, tuliona kwa macho mchaka mchaka wa ujenzi was shule hizi .Makamanda tuache kujipendekeza. Mfumo wa Elim ya Sekondari kwa kila kata ulinuniwa na Utawala wa Benjamin Mkapa. Walianza na Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM). Baada ya kukamilika kwa mpango huo ndipo ulipoanza Mpango wa Maendeleo ya Shule za Sekondari (MMES) ambao ulianza kutekelezwa awamu ya mwisho ya Utawala wa Mkapa.
Ni upunguwani na uhayawani kudhani kuwa ni Lowasa ndiye aliyebuni shule za Kata. Kilichotokea ni kwamba kwa vile utawala wa Mkapa ulimaliza muda wake na Utawala wa Kikwete kuanza, kama ilivyo ada ya kupokezana kijiti, Kikwete na Serikali yake wakaanza kutekeleza MMES iliyobuniwa na Mkapa na serikali yake. Kwa Ujumla ni kwamba MMES ni jitihada za serikali ya CCM kufikisha elimu ya sekondari kwa kila mtoto. Sisi kazi yetu ni kujipendekeza tu na kuchukua yale mazuri ya CCM kuwa yetu na mabaya ya CCM kuwa yao