Aliyeolewa na Imam Uganda, asema alifanya hivyo kwa sababu ya maisha magumu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Bwana Richard Tumushabe, mtu aliyejifanya mwanamke na kuolewa na Imam Mohammed Mutumba, amewaomba Waganda wasimhukumu kwa matendo hayo

Tumushabe alisema alilazimika kuuza mwili wake kwenye mitaa ya Kampala baada ya kukosa kazi. "Ninakubali nilichofanya ilikuwa kosa. Nilikosea familia yangu na wengine wanaohusika na ninajuta”

Alifafanua kuwa yeye na marafiki wake walipofika Kampala kutafuta kazi, walazimika kulala mitaani.

Wanaume walikuja na gari zao usiku na kuomba walale na wawalipe pesa. Walikubali kwa kuwa walihitaji pesa.
Madai ya Tumushabe ni kielelezo cha mapambano ya vijana wengi wa Uganda wanavyotafuta ridhiki kutokana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira nchini humo.

Sheikh Mutumba, imamu wa Msikiti wa Kyampisi Masjid Noor wilayani Kayunga, alisema alifunga ndoa na mtu aliyejulikana kama 'Swabullah Nabukeera' na alikaa wiki mbili bila kujua jinsia yake.

Ukweli ulijulikana baadaye baada ya polisi kumkamata 'Nabukeera' kwa madai ya wizi na wakati wa uchunguzi wa mwili wa polisi wa kike kabla ya kupelekwa kwenye selo.

Tumushabe anatuhumiwa kwa kuiba seti ya runinga na nguo zenye thamani ya Zaidi ya shilling millioni mbili za kitanzania mali ya Bw Eryazi Jimmy wa Kijiji cha Kyampisi katika kaunti ndogo ya Kayunga
 
Yaani kama kuna kitu kigumu mwanaume kuweza kufanya hata kama ni shida ambayo ingegharimu maisha yake ni kuuza mwili wake,sasa huyu nashindwa hata kumtafakari ni mwanaume wa aina gani...
 
wiki mbili bila kumfanya......wote mashoga
mimi wangu kwa wiki mbili bila kumpa patachimbika huko chumbani labda nilale chumba cha watoto
 
Back
Top Bottom