aliyeng'olewa na madiwani aukwaa uenyekiti wa mkoa wa geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

aliyeng'olewa na madiwani aukwaa uenyekiti wa mkoa wa geita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by WABHEJASANA, Oct 14, 2012.

 1. WABHEJASANA

  WABHEJASANA JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 4,225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  MKUTANO Mkuu wa kwanza wa CCM katika Mkoa wa Geita janaumemchagua Mwenyekiti wake wa kwanza wa CCM ambaye atakiongoza chama hichokatika kipindi cha miaka mitano ijayo ambapo Joseph Msukuma alipata ushindi wakishindo dhidi ya wapinzani wake wawili.
  Msukuma anaukwaa uwenyekiti CCM Mkoa wa Geita na kuingiakwenye rekodi ya kuwa mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho katika mkoa wa Geita,ikiwa ni takribani Miezi 10 tangu ang'olewe kwenye nafasi ya Uenyekiti waHalmashauri ya wilaya ya Geita na madiwani wenzake kwa tuhuma mbalimbaliikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
  Hata hivyo kung'olewa kwake kwenye kiti hicho kulipingwa nawananchi wa kawaida ambao walikuwa wakimuona kama mtetezi wa wanyonge,haliambayo imethibitishwa na ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi huo na kuwakielelezo kwamba ni mtu anayekubalika kwa jamii ya mkoa huo.
  Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa GEDECO Msukuma alifanikiwa kupata jumla ya kura 565Kati ya 698 ikiwa ni ushindi wa zaidi ya asilimia 80 ya kura zote zilizopigwakatika uchaguzi huo uliozishirikisha wilaya tano za Nyang'hwale,Geita,Chato,Mbogwe,naBukombe.
  Alifuatiwa na Jeremiah Ikangala ambaye alipata kura 130ikiwa ni asilimia 18,huku aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo katikakipini cha miaka mitano iliyopita na kuhakikisha kwamba Mkoa wa Geitaunapatikana John Luhemeja akipata kura 5 kati ya kura 698.
  Luhemeja aliamua kuacha kutetea kiti chake katika wilaya nakwenda kugombea nafasi hiyo katika mkoa kwa madai kuwa anao uwezo mkubwa wakukiongoza chama hicho katika mkoa kwa vile ameshiriki katika mchakato mzima wakuhakikisha kwamba Geita inapata mkoa huku akijisifia uzoefu na elimu ya chuokikuu aliyonayo.
  Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa uchaguzi huo WilliamLukuvi ambaye ni mjumbe wa Kamati kuu ya CCM alisema Msukuma huenda akawamwenyekiti wa kwanza kushinda kwa ushindi mkubwa katika chaguzi za CCMzinazoendelea nchini zilizoshirikisha washindani watatu.
  "Sehemu nyingine wanapokuwa wagombea watatu mara nyingikura hurudiwa kwa washindani wawili ili kumpata mshindi,lakini huyu Msukumaametia fora kwa kupa ushindi wa moja kwa moja tena ushindi wa zaidi ya asilimia80...hii ni kuonyesha ni namna gani ambavyo anakubalika kwa wanachama wa ccmkwenye mkoa huu....'' alisema Lukuvi.

  Haya wadau huyu jamaa ambaye alionekana kupingana na UFISADI akiwa ndani ya CCM wakati akiwa Mwenyekiti wa Halmashauri na baadaye katika mazingira ya KIFISADI akang'olewa na Madiwani wenzake sasa amekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa Mzima wa Geita na madiwani wote wa ccm katika mkoa huo wakiwemo waliomng'oa wako chini yake,na kibaya zaidi tayari ametangaza vita na MAFISADI walioko ndani ya CCM sipati picha itakuwaje!!!!


   
 2. M

  Mwapa Member

  #2
  Oct 14, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ni mtu niliyemfahamu korogwe tanga his a fighter hata kama hana elimu hivyo ila kiuongozi yupo vizuri sana.
   
Loading...