Aliyemwahidi Lowassa mvua afungwa kwa rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyemwahidi Lowassa mvua afungwa kwa rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, Oct 25, 2008.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Source: Tanzania Daima

  THAKSIN Shinawatra, Waziri Mkuu wa zamani wa Thailand, aliyeahidi kutuletea mvua ya kutengeneza nchini mwetu, baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, kumtembelea, amehukukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa makosa ya rushwa.

  Shinawatra kama ilivyo kwa Lowassa, wote walipata kuwa mawaziri wakuu katika nchi zao na wote waliondoka madarakani kwa tuhuma za rushwa.

  Tofauti ni kwamba Shinawatra ndiye aliyeanza kuondoka madarakani wiki chache baada ya Lowassa kurejea nchini, kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika Septemba mwaka 2006 dhidi ya serikali ya Thailand.

  Sababu kubwa iliyomfanya waziri mkuu huyo apinduliwe na ndiyo iliyompeleka jela, ni matumizi mabaya ya madaraka na rushwa.

  Shinawatra anatuhumiwa kumsaidia mke wake kununua ardhi kwa bei ya kutupwa, tena kwa kutumia wakala wa serikali mwaka 2003 alipokuwa waziri mkuu.

  Kiongozi huyo wa Thailand mwenye miaka 59 aliruka dhamana na kukimbilia nchini Uingereza anakoishi uhamishoni akiwa na mkewe Pojaman (51), ambaye naye awali alishitakiwa lakini Mahakama Kuu wakati ikimhukumu mume wake wiki hii ilibaini kuwa hana hatia.

  Hukumu hiyo ni ya kwanza dhidi ya kiongozi huyo wa zamani nchini Thailand tangu alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi.

  Kupinduliwa kwake pamoja na Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo, Sonthi Boonyaratglin, kulivuruga mpango ulioombwa na Lowassa wakati Tanzania ilipokabiliwa na ukame uliosababisha kukauka kwa mabwawa ya kuzalisha umeme.

  Wachambuzi wa masuala mbalimbali nchini Thailand, wanasema kitendo cha mahakama kutoa hukumu hiyo ni upepo mwingine wa kudhoofisha tatizo la kisiasa ambalo bado upepo wake unaonekana kuvuma vibaya.

  Shinawatra mwenyewe anapinga madai hayo, alipozungumza na Shirika la Habari la Associated Press mara baada ya jopo la majaji wanane waliokuwa wakiongozwa na Jaji Thongloh Chomngam, anasema hana hatia na kwamba hukumu hiyo ilichochewa na siasa ili kuendeleza mapinduzi dhidi yake.

  “Mshitakiwa alikuwa waziri mkuu kipindi hicho, ilibidi awe mkweli na muwazi lakini pia mwenye kufuata maadili kwa kutokiuka sheria zinakokataza rushwa,” anakaririwa jaji huyo aliposoma hukumu ndefu dhidi ya Shinawatra.

  Hatua ya Mahakama Kuu ya Thailand imemfanya Shinawatra kuwa mwanasiasa wa kwanza kupatikana na makosa ya rushwa aliyoyafanya akiwa Waziri Mkuu, lakini wachambuzi wanadai kuwa hatua hiyo haitaondoa tatizo la kisiasa lililopo nchini humo kwa sasa wakati serikali ya nchi hiyo inaongozwa na shemeji yake, Somchai Wongsawat (61) ambaye ni Waziri Mkuu mpya.

  Somchai, alithibitishwa na Bunge baada ya mahakama kumtimua Samak Sundaravej, aliyerithi madaraka kutoka kwa Shinawatra, kwa madai ya kumkingia kifua waziri mkuu huyo wa zamani.

  Mbali na hilo, sababu nyingine iliyomfanya atimuliwe ni kulipwa fedha nyingi baada ya kutokea kwenye onyesho la upishi ambapo ni kinyume cha sheria za nchi yake.

  Waziri Mkuu huyo mpya amemuoa dada wa Shinawatra, achilia mbali sifa na uzoefu wa muda mrefu aliokuwa nao katika uongozi wa serikali, lakini amewahi kuwa jaji, waziri wa elimu katika baraza la mawaziri lililokuwa likiongozwa na Samak.

  Hata hivyo, doa alilonalo na pengine kwa sababu serikali yake inakabiliwa na upinzani mkali ni hili la kuwa na uhusiano na Shinawatra, mtu aliyepatikana na hatia kwa makosa ya rushwa.

  Maelfu ya wafuasi wa chama cha People’s Alliance for Democracy ambao ni wapinzani wa serikali waliokuwa wamezingira ofisi ya Waziri Mkuu tangu Agosti mwaka jana, walikuwa wakiimba: “Nenda jela…nenda jela Shinawatra na mke wako…mla rushwa wewe una tumia madaraka vibaya.”

  “Bado hatutaiacha serikali, tutaendelea kusisitiza juu ya mabadiliko ya kisiasa ili kuwa huru kutoka katika utawala wa Shinawatra, ambaye amezidi kuishikilia serikali na mfumo wa sasa wa kisiasa uliojaa maadili potofu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka,” anasema kiongozi mmoja wa upinzani aliyetambulika kwa jina la Pipob Thongchai.

  Kuondoka madarakani kwa Shinawatra na hata Lowassa aliyekuwa ameiomba taasisi ya mfalme wa Thailand inayosimamia utafiti wa kutengeneza mvua, itume wataalamu wake Tanzania kuangalia uwezekano wa kutumia teknolojia hiyo ili kujaza bwawa la Mtera, kumehitimisha ndoto hiyo.

  Septemba 3 mwaka 2006 mara baada ya kutembelea Chuo Kikuu cha Kasetsart, ambacho kinafanya utafiti wa kutengeneza mvua kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Ushirika ya nchi hiyo, Lowassa alikaririwa na vyombo vya habari akisema Serikali ya Thailand imekubali kuisaidia Tanzania kutengeneza mvua baada ya kupokea maombi rasmi ya kufanya hivyo.

  Juhudi za Lowassa hazikuzaa matunda, licha ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo wa Thailand, Dk. Suthiporn Chirapanda, kumhakikishia kuwa suala hilo linawezekana na sasa wana utaalamu wa kuifanya mvua kunyesha juu ya bwawa tu ilimradi hewa iwe na unyevu unaotakiwa.

  Alimthibitishia kuwa taasisi hiyo ilipokea maombi kutoka nchi za Mashariki ya Kati na baadhi ya nchi za Asia Kusini, zikiwemo Indonesia, Philippines, Malaysia, Bangladesh na Srilanka.

  Katika mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mfalme ambaye pia ni mtaalamu wa teknolojia ya kutengeneza mvua, Wathana Sukanchanaset, imebainika kuwa kwa kutumia kemikali nane tofauti na hatua (stages) tatu tofauti, wataalamu hao wanaweza kutengeneza mvua endapo angani kuna unyevu wa kutosha na wakalenga inyeshe mahali wanapotaka.

  Baada ya kufanya utafiti na kupata kiwango cha unyevu na mwelekeo wa upepo, kazi ya kutengeneza huchukua wastani wa saa tano na kufuata hatua tatu ambazo ni kufanya mawingu yatokee (triggering), yawe mazito (fattening) na kuchokoza mvua inyeshe (attacking).

  Juhudi za Lowassa hazikuishia hapo, ujumbe wa Serikali ya Thailand ulifika nchini ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Ushirika ya Thailand, Theera Wongsamut na kukawa na taarifa kuwa mkataba wa kuanza kazi hiyo ungetiwa saini Septemba mwaka 2006.

  Lakini mpango huo baadaye haukusikika tena ukiendelea baada ya Shinawatra kuondolewa madarakani kinguvu na Lowassa pia kuachia ngazi Februari mwaka huu, kwa tuhuma za ofisi yake kuhusika kwenye mkataba wa zabuni ya kufua umeme wa megawati 100 kutoka Kampuni hewa ya Richmond.

  Hatua ya Lowassa kuachia ngazi ilitokana na taarifa ya kamati teule ya Bunge iliyopewa kazi ya kuchunguza uhalali wa mkataba huo, chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyemb
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Oct 25, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  Waarabu wa Pemba........ ....

  waberoya
   
 3. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Siyo kama wa unguja.
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwani ahadi ya mvua ilikuwa ya kiserikali au Lowassa kama Lowassa?
   
 5. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  hapa napo pana stori ?
   
 6. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Stori ipo, TUMEPONEA TUNDU LA SINDANO kwani hujui kuwa ndege wafananao huruka pamoja?
   
 7. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2008
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yeye EL alienda kujifunza namna ya kula rushwa au alikwenda kumfundisha namna ya kula rushwa?
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Birds of the same feather flock together!
   
 9. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2016
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
   
 10. m

  m2020 JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2016
  Joined: Jul 10, 2016
  Messages: 754
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 180
  MUNGU MKUBWA ALITUEPUSHA NA MTU YULEE. KWA HAPA NAMSIFU SANA MZEE KIKWETE NA MZEE SITA KWA WELEDI WAO KUSIMAMIA AKAE KANDO YA SERIKALI. TUNGEUMIAAA.
   
Loading...