Aliyemuua Mkewe wa kwanza, Amuua Mke pili Tena na kufungwa miaka minne

Bravo snr

Senior Member
Aug 16, 2020
182
472

Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka minne Lameck Essau Meza mkazi wa Sikonge mwenye umri wa miaka 38 baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumuua bila kukusudia mkewe Dafroza Paul.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, Amour Khamis amesema baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili katika shauri hilo la mauaji namba 19 la mwaka 2017, mahakama imejiridhisha pasina shaka yoyote kwamba mshtakiwa Lameck alifanya tukio hilo la kumpiga mkewe na kusababisha kifo chake kinyume na kifungu cha 196 Disemba 24 mwaka 2012 huko Kijiji cha Mwenge wilayani Sikonge.

Hata hivyo kabla ya kutolewa hukumu Upande wa Jamhuri ulidai kuwa mshtakiwa hii ni mara yake ya pili kufanya mauaji ya aina hiyo ambapo awali alimuua mke wake wa kwanza na kufikishwa mahakamani akahukumiwa kwenda jela miaka minne baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na hii ilikuwa ni mara yake ya pili kurejea kosa la aina hiyo baada ya kumuua mkewe huyu mwingine.

“Hii ni mara ya pili alishawahi kumuua bila kukusudia Mkewe wa kwanza (kwa kumpiga) na alihukumiwa kifungo cha miaka minne pia,” ilielezwa mahakama hiyo.

Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo kuu kanda ya Tabora alidai kuwa mauaji hayo ameyafanya tena bila kukusudia kutokana na hasira za ghafla za mshtakiwa zilizotokana na mwanamke huyo kuchelewa kurudi nyumbani na ndipo akawa anamuonya kwa kumpiga mateke, ngumi na vipande vya tofali.

Lameck Meza amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka minne Jela huku mahakama ikiacha milango wazi ya kukata rufaa.
 
Sasa hapo mnamsaidiaje? Ingekuwa nchi zilizoendelea hapo kifungo chake kingeongezwa na kuhudhuria darasa maalum la psychology. Maana huyo tatizo lake ni kushindwa kudhibiti hasira zake na kwa magereza ya bongo hakuna kitakacho msaidia zaidi ya kuja kumrudisha mtaa baada ya kifungo chake kuisha akiwa bado na tatizo lile lile linalo msababisha kuua
 
Ndoa za siku hizi lazima uishi kwa timing, hawa wanaume wa kupiga akakuua haazi siku moja,leo atakupiga kofi unachukulia kawaida,kesho anakupiga vichwa unapotezea keshokutwa anakumalizia kabisa inapigwa parapada!!.please ladies be carefully oohooooo
 
HII SIO SAWA PANA WALAKINI HAPA,JE ANATATIZO KWENYE AKILI YAKE?,NA ENDAPO HANA TATIZO NASHAURI HAYA SEREKALI IKATE RUFAA YA HUKUMU NA MASHTAKA YABADILISHWE YAWE MAUAJI,HAKUNA JAMBO LA AINA HII
 
Yaani mtu unaambiwa huyu aliua mkewe wa kwanza bila kukusudia halafu na wewe unajipeleka hapo hapo kuolewa!!!
 
Back
Top Bottom