Aliyemuua mkewe kwa shoka anaswa kwa 'Dog Style' akitorokea nchini Kenya

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Hatimaye jeshi la polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumnasa mtuhumiwa wa mauaji ya Mkewe, Moses Palangyo mkazi wa kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru ambaye siku ya sherehe za Christmas Desemba 25 alimuua mkewe Mary Mushi ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kwa kumkata na shoka kichwani.

Kamanda wa polisi Mkoani hapa, Jonathan Shana amethibitisha kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa na kueleza kuwa mbinu ya Dog Style ndio iliyofanikisha kupatikana kwa mtuhumiwa huyo akiwa mafichoni eneo la Ngaramtoni wilayani humo wakati akijiandaa kukimbilia nchi jirani ya Kenya.

Amesema mtuhumiwa mara baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa alipitiwa na shetani na kufikia hatua ya kufanya mauaji hayo, hivyo jeshi la polisi litamfikisha mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Kamanda Shana amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa Jana majira ya saa 11 jioni baada kuwekewa mtego uliofanikisha kumnasa akiwa mafichoni nyumbani kwa mtu.

Tukio hilo mbali na kuwasikitisha ndugu na jamaa pia limewaacha vinywa wazi wakazi wa kijiji hicho ukizingatia kuwa muuaji alikuwa mwokovu na mwimbaji wa nyimbo za injili.

Kamanda Shana ameeleza kuwa baada ya kumhoji mtuhumiwa alikiri kutenda kosa akidai shetani alimpitia na hapakuwa na sababu nyingine iliyopelekea kutenda kosa hilo la kinyama.

Baadhi ya majirani na eneo la tukio wamedai kuwa mtuhumiwa alimpeleka marehemu nyumbani kwa wazazi wake kwa lengo na kumtambulisha na waliishi nyumbani hapo kwa muda wa wiki tatu kabla ya kutekeleza tukio hilo, Desemba 25 mwaka 2019.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa na mkewe walikuwa wakiishi pamoja eneo la Shangarai wilayani humo na baadae walikubaliana kwenda kwa wazazi kwa ajili marehemu kutambulishwa.

"Wakiwa nyumbani kwa baba yake na mtuhumiwa ,kulitokea kutoelewana kwa mtuhumiwa aliyekuwa akidai apatiwe funguo ya chumba cha marehemu ili aende mara moja lakini marehemu alikataa akidai kuwa alikuwa akidaiwa kodi ya nyumba hivyo kitendo cha kuonekana hapo ingeleta usumbufu kwa mwenye nyumbani" alisema jirani ambaye aliomba jina lake lisiandikwe

Amesema hatua hiyo haikumpendeza mtuhumiwa ambapo siku ya tukio wakati akiandaliwa chai alionekana akinoa shoka na baadae aliingia ndani kunywa chai akiwa na shoka lake.

Taarifa zinadai kuwa mara baada ya kumaliza kunywa chai alimwita marehemu ndani ya chumba walichokuwa wakilala na baadae alianza kumshambulia kwa kumkata na shoka mara mbili kichwani lililopelekea kifo chake.

Akiongelea tukio hilo baba mzazi wa mtuhumiwa Mzee Latiaeli Palangyo amesema kuwa hapo awali hapakuwa na ugomvi wowote na walitarajia kusherehekea vema sikukuu ya Krismasi kwani muda mfupi marehemu aliwapikia chai.

Naye mwimbaji wa nyimbo za injili, Emmanuel Mbasha ambaye alifika kituo cha polisi wilani Arumeru kuzungumzia tukio hilo amesema kitendo hicho kimewasikitisha sana kwani kimekatisha ndoto ya mwimbaji mwenzao Mary Mushi ambaye alikuwa ndio kwanza ameanza kuchipukia.

Amesema wao kama waimbaji wa nyimbo za injili wanajipanga kuangalia jinsi ya kumuenzi marehemu.

Kwa upande wake Rais wa umoja wa waimbaji wa Nyimbo za Injili, Dkt Donald Kisanga amesema kuwa tukio hilo limewasikitisha sana ila analishukuru jeshi la polisi kwa kulishughulikia kwa makini na kufanikisha kumtia mbaroni mtuhumiwa akiwa hai na kuitaka sheria ichukue mkondo wake.

Kwa mujibu wa Shana mtuhumiwa ambaye anashikiliwa katika kituo cha polisi, atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

Ends.

IMG_20191229_105946.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatimaye jeshi la polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kumnasa mtuhumiwa wa mauaji ya Mkewe ,Moses Palangyo mkazi wa kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru ambaye siku ya sherehe za xmass desemba 25 alimuua mkewe Mary Mushi ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili kwa kumkata na shoka kichwani.


Kamanda wa polisi Mkoani hapa,Jonathan Shana amethibitisha kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa na kueleza kuwa mbinu ya Dog Style ndio iliyofanikisha kupatikana kwa mtuhumiwa huyo akiwa mafichoni eneo la Ngaramtoni wilayani humo wakati akijiandaa kukimbilia nchi jirani ya Kenya.


Amesema mtuhumiwa Mara baada ya kuhojiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na kueleza kuwa alipitiwa na shetani na kufikia hatua ya kufanya mauaji hayo ,hivyo jeshi la polisi litamfikisha mahakamani Mara baada ya upelelezi kukamilika.


Kamanda Shana amesema kuwa mtuhumiwa alikamatwa Jana majira ya SAA 11 jioni baada kuwekewa mtego uliofanikisha kumnasa akiwa mafichoni nyumbani kwa mtu


Tukio hilo mbali na kuwasikitisha ndugu na jamaa pia limewaacha vinywa wazi wakazi wa kijiji hicho ukizingatia kuwa muuaji alikuwa mwokovu na mwimbaji wa nyimbo za injili.


Kamanda Shana ameeleza kuwa baada ya kumhoji mtuhumiwa alikiri kutenda kosa akidai shetani alimpitia na hapakuwa na sababu nyingine iliyopelekea kutenda kosa hilo la kinyama.


Baadhi ya majirani na eneo la tukio wamedai kuwa mtuhumiwa alimpeleka marehemu nyumbani kwa wazazi wake kwa lengo na kumtambulisha na waliishi nyumbani hapo kwa muda wa wiki tatu kabla ya kutekeleza tukio hilo,desemba 25 mwaka 2018.


Inadaiwa kuwa mtuhumiwa na mkewe walikuwa wakiishi pamoja eneo la Shangarai wilayani humo na baadae walikubaliana kwenda kwa wazazi kwa ajili marehemu kutambulishwa.


"Wakiwa nyumbani kwa baba yake na mtuhumiwa ,kulitokea kutoelewana kwa mtuhumiwa aliyekuwa akidai apatiwe funguo ya chumba cha marehemu ili aende Mara moja lakini marehemu alikataa akidai kuwa alikuwa akidaiwa kodi ya nyumba hivyo kitendo cha kuonekana hapo ingeleta usumbufu kwa mwenye nyumbani" alisema jirani ambaye aliomba jina lake lisiandikwe


Amesema hatua hiyo haikumpendez mtuhumiwa ambapo siku ya tukio wakati akiandaliwa chai alionekana akinoa shoka na baadae aliingia ndani kunywa chai akiwa na choka lake.


Taarifa zinadai kuwa Mara baada ya kumaliza kunywa chai alimwita marehemu ndani ya chumba walichokuwa wakilala na baadae alianza kumshambulika kwa kumkata na shoka Mara mbili kichwani lililopelekea kifo chake.


Akiongelea tukio hilo baba mzazi wa mtuhumiwa mzee Latiaeli Palangyo amesema kuwa hapo awali hapakuwa na ugomvi wowote na walitarajia kusherehekea vema sikukuu ya Krisimas kwani muda mfupi marehemu aliwapikia chai .


Naye mwimbaji wa nyimbo za injili ,Emanuel Mbasha ambaye alifika kituo cha polisi wilani Arumeru kuzungumzia tukio hilo amesema kitendo hicho kimewasikitisha sana kwani kimekatisha ndoto ya mwimbaji mwenzao Mary Mushi ambaye alikuwa ndio kwanza ameanza kuchipukia.


Amesema wao kama waimbaji wa nyimbo za injili wanajipanga kuangalia jinsi ya kumuenzi marehemu.


Kwa upande wake rais wa umoja wa waimbaji wa Nyimbo za Injili,dkt Donald kisanga amesema kuwa tukio hilo limewasikitisha sana ila analishukuru jeshi la polisi kwa kulishughulikia kwa makini na kufanikisha kumtia mbaroni mtuhumiwa akiwa hai na kuitaka sheria ichukue mkondo wake.


Kwa mujibu wa Shana mtuhumiwa ambaye anashikiliwa katika kituo cha polisi ,atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.


Ends.....



View attachment 1306455

Sent using Jamii Forums mobile app
Inshallah afande amenenepa kisawasawa
 
Hichi kifo kilichotokea sijui nyuma yake kuna infuence gani!

Huyu mtuhumiwa alienda kunoa shoka kisha akaenda kukaa nalo ndani akisubir amalize chai aanze kutekeleza alichokua anawaza!

Ugomvi ni ufunguo tu ndy uliopelekea kifo cha huyo dada!

Kweli kifo hakina mwaliko!
 
Back
Top Bottom