Aliyemuua askari Arusha adaiwa kufa akijaribu kuwatoroka polisi

Siku ilipotoka habari ya huyo askari kuuawa mimi nilisema hapa ni bora ajiue kabla hajakamatwa kwani akikamatwa atakufa kifo cha mateso sana. Inaonekana jamaa aliteswa polepole mpaka akafa.
alijua labda ataweza kujificha huku akiwa anachat na hawala yake, teknolojia imemkamatisha
 
Alifungwa akatoroka na akaendelea na maisha bila kutafutwa? Taarifa za polisi wa Tanzania ni za kusikiliza kwa makini waongo waongo sana. Askari wa Arusha wapiga dili vibaya mno mzee huwajui tu. Kesi ya Zombe ilikuwa hivi hivi.
Tena wakati mwingine askari mwanamke anachukua mumewe ambaye si askari wanaenda kupiga dili kitaa.
Huyo askari ilikuwaje akaenda kumkata mhalifu aliyetoroka jela pekeyake? Hili swali halijibiwi sijui kwa nini.
Lakini yote hayo yanasimamia kwenye mauaji ya yule askari awe ameenda peke yake au na wenzake.

Shahidi aliyekuwapo kwenye tukio kamtambua huyu jambazi aliyefanya tukio.
 
Huu ni uongo uliowazi kabisa..

Ni kama wale wafungwa waliouliwa mafia kwa kupigwa then baadhi ya Askari waliandika vivohivyo kwamba wameruka kwenye gari.

Na wengine wakaandika ukweli wa kilichotokea.
Nusu ya Askari wakaenda mahabusu na nusu wakabaki.

Hilo jambazi wameliua kwa makusudi na linastahiri hicho kifo.
Unajua tatizo kubwa la kuruhusu au kufurahia polisi kufanya mauaji kama haya ni kuwa itazoeleka na kuwa tabia. (au sahihi zaidi niseme imeshazoeleka na kuwa tabia) Na ikishakuwa tabia ni lazima siku moja atakuja kuuawa mtu/watu wasio na hatia. Hii ni kanuni na ni lazima itokee. Leo kweli wanaweza kuua jambazi la kweli kabisa (kama hilo lililouawa) lakini kesho kuna uwezakano wakaua mtu asiye na hatia kwa makosa au makusudi.
 
Unajua tatizo kubwa la kuruhusu au kufurahia polisi kufanya mauaji kama haya ni kuwa itazoeleka na kuwa tabia. (au sahihi zaidi niseme imeshazoeleka na kuwa tabia) Na ikishakuwa tabia ni lazima siku moja atakuja kuuawa mtu/watu wasio na hatia. Hii ni kanuni na ni lazima itokee. Leo kweli wanaweza kuua jambazi la kweli kabisa (kama hilo lililouawa) lakini kesho kuna uwezakano wakaua mtu asiye na hatia kwa makosa au makusudi.
Wasio na hatia waliisha uwawa, lakini sio kweli askari wote ni waovu kiasi cha kuuwa kila mshukiwa wa ujambazi.

Mara nyingi ukiona jambazi anauwawa ujue hata askari waliisha choka nae, anakamatwa akifugwa muda mfupi yupo uraiani na akiendeleza matukio hayo hayo.

Hakuna haja ya kumkamata kila mara ni risasi tu ndo jawabu.
 
"Ukiuwa kwa upanga utaondoka kwa upanga"

IGP. Simon Sirro -
Kibiti
August 12 , 2017


Atawalaye kwa upanga , atakufa kwa upanga- biblia


Nafikiri kila mtu ameelewa sasa.
 
Huyo marehemu anayeitwa jambazi ukute hakuwahi iba hata ufagio.

1. Nani anaweza prove kwamba alifungwa miaka 16 pale Kisongo kisha akatoroka ila akaendelea kuishi palepale Arusha
2. Kilichomfanya amuue askari kwa mapanga usiku kwa jirani yake aliyetakiwa kukamatwa ni nini. Hii kesi anayodaiwa kuvamia wala hakumuhusu
3. Huyo askari namna gani ameenda peke yake usiku kumkamata mtuhumiwa nyumbani kwake
4. Marehemu jambazi aliwezaje kuruka kwenye gari wakati yuko chini ya ulinzi na kafungwa pingu. Ina maana askari wetu ni wazembe kiasi hiki

Hii kesi bila hata kutumia akili ina ukakasi mwingi
Ukiishaua huna utetezi mkuu.
 
Wasio na hatia waliisha uwawa, lakini sio kweli askari wote ni waovu kiasi cha kuuwa kila mshukiwa wa ujambazi.

Mara nyingi ukiona jambazi anauwawa ujue hata askari waliisha choka nae, anakamatwa akifugwa muda mfupi yupo uraiani na akiendeleza matukio hayo hayo.

Hakuna haja ya kumkamata kila mara ni risasi tu ndo jawabu.
Unajua kusoma kwa ufahamu? Nani kasema askari wote ni waovu kiasi cha kuua kila mshukiwa? Sasa kama unajua kuna wasio na hatia walishaua huoni ni vizuri watuhumiwa wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kufanya wale wasio na hatia wasiuawe?
 
Kumbe hawa jamaa wanaelewa uchungu wa kimpoteza mwenzao, na wale wa Akwilina na Mwangosi Mungu atawasimamia.
 
Polisi ni kazi ya heshima Duniani kote ila hapa Tz ni laana kutokana tu na matendo ya baadhi yao.
 
Duh! we mtu wa wapi?
Yaani niwe na ndugu jambazi au gaidi halafu niwe na huruma nae!!

Sasa hao ndugu wa huyo askari wenyewe hawana uchungu na ndugu yao ?
Huyu aliisha wahi fungwa na akatoroka, hapo ujue kuna askari magereza alifukuzwa kazi.

HAKUNA HURUMA YA KINAFIKI KWANGU KWA WATU WA NAMNA YAKE.
Mahakama zipo kwa ajili ya nini hasa kama watu wanaopaswa kusimamia sheria wanazivunja wazi wazi alafu mazuzu kama wewe mnashangilia
 
Enzi hizo bado niko huko kwenye hiyo taasisi ndio ilikuwa michezo yetu hiyo kwa wahalifu sugu...wengine tulikuwa tunawakamata wakiwa hai tunawapeleka msituni tunawapiga risasi then tunautangazia umma kuwa wameuwawa katika fierce gun battle.
 
Jambazi aliyemuua kwa kumkata mapanga Askari polisi, H.2407 Constable Damasi Magoti wa kituo Cha polisi Mbughuni wilayani Arumeru, Jacob Kideko au Ramadhani Kichwa(43) Mkazi wa Makiba amefariki dunia katika jaribio la kuwatoroka polisi alipokuwa akisafirishwa jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda was polisi mkoa wa Arusha, Justine Masejo,jambazi huyo alikamatwa julai 27 mwaka huu Mkoani Morogoro alikokuwa amejificha kukwepa polisi na walipofika eneo la Kisongo jijini Arusha akiwa kwenye gari amefungwa pingu mkononi alijaribu kuruka kuwakimbia polisi.

Taarifa hiyo inadai kwamba mtuhumiwa alipata majeraha kichwani na michubuko kwenye mwili wake, Hata hivyo polisi walijaribu kuokoa Maisha yake kwa kumpeleke katika hospital ya Mkoa Mount Meru ,lakini alipoteza Maisha akiwa njiani.

Inadaiwa kuwa jambazi huyo alikuwa akisakwa na Askari wa gereza kuu la Arusha baada ya kufungwa miaka 16 ,Septembe 10 ,2008 lakini alitoroka mnamo April 1, 2017 akiwa chini ya ulinzi wa askari wa Magereza.

Marehemu Magoti aliuawa usiku Julai 23 mwaka huu wakati akitekeleza majukumu yake katika Kijiji Cha Makiba akijaribu kumkamata mtuhumiwa wa wizi nyumbani kwake, ndipo jambazi huyo alitokea jirani na eneo la tukio na kumshambulia kwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali na kupoteza Maisha.
Tumeelewa.
 
Back
Top Bottom