Aliyemuiba mtoto na kukaa naye siku nne, aachiwa huru kituo cha polisi Kiomboi, Iramba

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,230
6,469
Wadau wa JF poleni na pilika zetu hizi za kila siku,

Hivi karibuni limetokea tukio la kuibwa mtoto wa miaka miwili ktk mji mdogo wa Kiomboi wilayani Iramba. Tukio hili lilitokea eneo la Soweto lenye watu wengi mjini hapo.

Aliyemuiba mtoto ni jirani ambaye ni mstaafu serikalini. Baada ya kumuiba mtoto huyo alimfungia kwake na inadaiwa Mzee huyu na Mkewe wana imani za kishirikina hivyo huenda ilikuwa kwa mambo ya makafara. Mzee huyu alishiriki vikao vyote vya mwano kama jirani ili kupanga namna ya kumpata mtoto huyu aliyepotea.

Za mwizi arobaini, wenye mtoto walimleta Mganga na mganga alisema mtoto kashikiliwa na jirani. Lahaulaaahh!!! Watu wakaivamia nyumba na kumkuta mtoto kafichwa akiwa na sufuria kubwa la wali. Mzee alipigwa kidogo na nyumba kuvunjwa vioo kabla polisi kufika na kumchukua na mtoto na pia wazazi wa mtoto.

Ajabu mzee huyu yupo mtaani anapeta kama kawaida. Hivi makosa ya utekaji watoto yamekaaje?
 
Kamati ya ufundi imehusika mzee kuachiwa mkuu.. mafaili yamepotezwa na watu(polisi) kichwani kumbukumbu zimefutwa
 
Ujinga mtupu huu.

Eti Mganga akaja akamtoa Mtoto, na mngemuua huyo Mzee wa watu kwa ujinga wenu.

Hii vita ya adui Ujinga, Maradhi na Umasikini haijafanikiwa kabisa.

Serikali ipige marufuku hii kada ya Waganga wa kienyeji maana wanafarakanisha sana jamii kwa utapeli wao.
 
Wadau wa JF poleni na pilika zetu hizi za kila siku,

Hivi karibuni limetokea tukio la kuibwa mtoto wa miaka miwili ktk mji mdogo wa Kiomboi wilayani Iramba. Tukio hili lilitokea eneo la Soweto lenye watu wengi mjini hapo.

Aliyemuiba mtoto ni jirani ambaye ni mstaafu serikalini. Baada ya kumuiba mtoto huyo alimfungia kwake na inadaiwa Mzee huyu na Mkewe wana imani za kishirikina hivyo huenda ilikuwa kwa mambo ya makafara. Mzee huyu alishiriki vikao vyote vya mwano kama jirani ili kupanga namna ya kumpata mtoto huyu aliyepotea.

Za mwizi arobaini, wenye mtoto walimleta Mganga na mganga alisema mtoto kashikiliwa na jirani. Lahaulaaahh!!! Watu wakaivamia nyumba na kumkuta mtoto kafichwa akiwa na sufuria kubwa la wali. Mzee alipigwa kidogo na nyumba kuvunjwa vioo kabla polisi kufika na kumchukua na mtoto na pia wazazi wa mtoto.

Ajabu mzee huyu yupo mtaani anapeta kama kawaida. Hivi makosa ya utekaji watoto yamekaaje?

Minyiramba na Minyaturu ni Michawi sana!
 
Ujinga mtupu huu.

Eti Mganga akaja akamtoa Mtoto, na mngemuua huyo Mzee wa watu kwa ujinga wenu.

Hii vita ya adui Ujinga, Maradhi na Umasikini haijafanikiwa kabisa.

Serikali ipige marufuku hii kada ya Waganga wa kienyeji maana wanafarakanisha sana jamii kwa utapeli wao.
Mkuu mganga kaonesha alipo mtoto baada ya muda mrefu wa kumsaka. Mwenye mtoto alileta mganga akafanikiwa
 
Hakuna chochote, huyo Mganga ana nini cha ziada kufanya hayo?

Ni Watu wanapumbazwa tu na Mjanja mmoja...na athari zake ni kufarakanisha Wanajamii kwa manufaa yake binafsi.
 
Sasa mtoto kapatikana kwake, huko pia kupumbazwa?
 
Oops! Hata sikusoma miaka eti..Ila yote yaliyofanyika hapo ni maigizo tu ya huyo mganga ..mtekaji na wazazi wa mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ongezea na baadhi ya watu waliokuwepo ambao jukumu lao lilikuwa ni kuhakikisha mtekaji haumizwi sana kwa kipigo na pia mleta mada mwenyewe maana ukiangalia comments zako zote ni kama anatetea nguvu ya mganga.
 
Back
Top Bottom