Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Mzee Mkinga alitumia muda mwingi kuwashambulia viongozi wa dini na hasa maaskofu,yapo mengi mazuri aliyasema lakini kwenye tuhuma dhidi ya viongozi wa dini Mzee Mkinga nadhani alikosa taarifa sahihi kuhusu Maaskofu.
Aliwatuhumu kwa uamuzi wao wa kutoka waraka wa kwaresm(TEC), na ule wa Pasaka(KKKT),tuhuma kubwa ilikuwa eti maaskofu hawa hawakuwahi kuandika waraka wala kutoa tamko lolote wakati madini na rasilimali za nchi hii zikiibiwa.
Nilistushwa sana na tuhuma hizi za uongo za Mkinga kwa maaskofu,Mzee Mkinga pamoja na mwendeshaji wa kipindi hawakuwa na taarifa za kutosha kuhusu walichokifanya viongozi wa dini wakati nchi hii madini yake yakiondoka na watu wake wakuawa pembezoni mwa migodi.
Viongozi wa dini tangu mwaka 1999 wakati nchi ilipoanza karibisha uwekezaji mkubwa kutoka nje ,walioiga kelele bila kuchoka.
Kati ya mwaka 2005 na 2012,viongozi wa Dini wakishirikiana na mashirika kama Norwegian Church walizunguka nchi nzima kwenye migodi ya dhahabu ,almasi na tanzanite,viongozi wa dini hawa walizunguka wenye na kwenda "FIELD"kuusaka ukweli.\Nakumbuka viongizi hawa wa dini walifukuzwa GGM na kuzuiwa kuingia,wkt huo serikali ilikuwa ukisema baya kuhusu wawekezaji unaitwa mchochezi.
Binafsi nilishawahi ambatana nao kwenda Geita ambapo walifukuzwa kama wakimbizi na wawekezaji,walikwenda Nzega,binafsi nikalishukuhia chozi la Shehe Fereji,nililiona chozi la Askofu mkuu Ruzoka na Askofu Munga,viongozi hawa walipiga kelele lakini Serikali ilikaa kimya na kuwatetetea wawekezaji.
Mwaka 2008,baadhi ya wananchi wa Nyamongo huko Tarime,waliungua ngozi kwa kile kilichoitwa sumu kutoka Mgodini,Serikali ilikataa,bunge lilikataa lakini maaskofu na mashehe walisimama kidete na kusema mto Tigite una sumu kutoka mgodin.
Viongozi wa dini(mashehe na maaskofu) walipiga kelele kuhusu wizi kwenye sekta ya madini,walilazimika kusaka wataalamu wa sayansi kutoka chuo kikuu cha DSM na chuo kikuu na sayansi cha Norwegian wakatoa ripoti iliyothibitisha kuwa maji ya mto Tigithe yana Sumu,lakini bunge na Serikali walikataa na kuwaona viongozi wa dini wachochezi wanawafukuza wawekezaji. leo Mkinga anasema Viongozi wa dini walikaa kimya.
Binafsi nilikuwa miongoni mwa waandishi walioandika sana kuhusu madini,mwaka 2009,viongozi wa dini hawa wanaobezwa nilikutana nao nikawapatia makala zangu za video kuhusu madini(nakumbuka nilimpatia Mchungaji Blandina),Viongozi hawa walikwenda na video hizo mpaka CANADA,walionesha video za uhalisia wa maisha ya watu wa pembezoni mwa madini na kusababishabaadhi ya watu huko Toronto kuandamana kuoinga unyama uliokuwa unafanyika,lakini Mzee Mkinga hayaoni hayo,na wakati yanafanyika Serikali ilikuwa kimya.
Mbali na ripoti ya Masha na Mark Bomani,ripoti nyingine iliyoainisha wizi katika sekta ya madini ni ya viongozi wa dini waliyoitoa mwaka 2009 na ilionesha kila kiti,kilichoandikwa na akina Prof Mruma kilikuwa ni marudio tu.
Nimeambatanisha ripoti ya viongozi wa dini ya mwaka 2009 ambayo ilithibitisha kuwa Mto Tigithe uliharibika kwa sumu kutoka mgodini lakini akina MKINGA hili hawalioni na serikali ilikuwa kimya,haikuwahi kiri wala ilazimisha Barrick kuwalipa fidia walioungua na sumu za mto Tigithe.
Tunapowashambulia viongozi wa dini,tuwashambulie kwa kutenda haki,.
Wasalaam