Aliyemtukana Rais Magufuli mtandaoni ana tofauti gani na Mkapa?

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,393
3,237
Mh sana Rais John Pombe Magufuli ni mtu mzima kidogo, kwa hiyo licha ya kutakiwa kumheshimu kama Rais wa nchi anayepaswa kuheshimiwa na kila raia tunapaswa kumheshimu kama mtu aliyetuzidi umri wengine ana umri sawa na wazee wetu!

Kama ambavyo hatuwezi kuwatukana na kuwaita wazee wetu mabwege hatupaswi kumuita Mh Rais bwege huu ni ukosefu wa maadili wa hali ya juu katika jamii yetu zaidi dhidi ya viongozi wetu. Hata kama watakuwa wamekosea ni lazima tutafute lugha ya staha ya kukosoa na kueleza kutokuridhika kwetu na mwenendo wa mambo.

Katika sakata hili sorry to say this, nimejifunza jambo moja kubwa sana. Kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili ndani ya jamii yetu na kwamba siasa zinatufanya watu tushindwe kuheshimiana na kuthaminiana yaani unamtoa mtu thamani kisa tu ana mtazamo tofauti na wewe katika jambo fulani jambo ambalo haliepukiki katika jamii iliyostaarabika lazima mtatofautiana.

Siwezi nikasema waziwazi kuwa neno BWEGE ni tusi kwa kiasi gani kama inavyoonekana kwenye kielelezo picha chenye tafsiri hapa chini ila nina uhakika hili neno ni neno linalotweza na kufisha au kushusha thamani ya utu wa mtu mbele ya wengine kifupi ni neno la kudharau na kudhalilisha pia! Kwani kama ilivyotamkwa kwamba fulani ni BWEGE unless mhusika athibitishe ubwege huo vinginevyo hiyo ni defamation(udhalilishaji).

Neno Bwege kisawe chake ni neno Mpumbavu kwa wale ambao si mahiri wa lugha ya kiswahili neno kisawe linamaanisha neno sawa na, kwa kifupi neno Bwege ni sawa na neno mpumbavu. BWEGE=MPUMBAVU, kwa maana hii utaona ukubwa wa tatizo la maadili kwa jamii yetu ya kitanzania kwani neno Mpumbavu kama tutakubaliana kuwa ni sawa na Bwege ambalo pia vyovyote vile tukikubaliana ni neno la kutweza liliwahi kutumika hadharani dhidi ya wananchi wasikiunga mkono chama cha mapinduzi na Rais Mstaafu Mheshimiwa Mkapa kipindi cha kampeni!

Hivyo basi kama ambavyo tunakubaliana kuwa Rais ametwezwa tunakubaliana pasi na shaka kuwa Mheshimiwa Mkapa aliwatweza wananchi wasiokiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwaita wapumbavu neno ambalo ni kisawe cha neno bwege.

Ndugu watanzania hii ni ishara kuwa jamii yetu imeoza si viongozi wala si wananchi wao wote wamekosa busara. Kama mtu aliyewahi kushika wadhifa wa Rais anaweza akatamka maneno hayo dhidi ya wengine itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida?

Kibaya zaidi jinsi maswala haya mawili yalivyoshughulikiwa inasikitisha zaidi na kujenga matabaka katika jamii, nakumbuka mbali na wananchi kulalamika kuwa wametukanwa si polisi wala kiongozi yeyote wa serikali aliyeinuka na kumkemea, kumuonya wala kumnyoshea kidole Mh Mkapa kwa kile alichokisema ilikuwa kama vile halijatokea jambo lolote kabisa, viongozi na polisi ama waliridhishwa ama walimuogopa muhusika!

Leo hii mwananchi wa kawaida, Kachupile, Masikini, Hohehahe, Masulupwete, malapulapu amethubutu kufata nyayo za role model wake Mkapa na kufanya kama alivyofanya anasakamwa, anaandamwa ananyanyasika, amebebwa msombemsombe na polisi kama vile gaidi wa alishababu!

Hii inasikitisha zaidi
 
Bwege ni mbaya zaidi ya kuitwa Lofa,

Tofautitisha KUTOSIMAMISHA kama tujuavyo neno bwege na kuitwa wewe ni maskini kama neno lofa lilivyo.
 
Tofauti zao;

1. Mmoja ni Rais mstaafu & ana KINGA ya kutoshitakiwa kwa kosa lolote.

2. Mmoja ni raia tu & ambaye hana kinga ya kutoshitakiwa.
 
unatafuta sifa ngoja wake wakutumbue maana na wewe umeshatukana.
 
Huyu bwana hajafanya kosa lolote kisheria. Kwanye mtamshi yake hajamtaja jpm...ieleweke kwamba hili jambo halina maana mbele ya sheria. Watu wanafanya assumption kuwa bwge ni jpm kwakuwa kuna neno nyerere pale mwisho....huu ni ujuha...kwan jina nyerere linamilikiwa na mtu mmoja tu?! yaan siku ya kesi anaweza akaja mtu mahakaman akajitambulisha kwa jina la bwege...na mwingine akasema jina lake la utani ni nyerere....! Kesi inaishia hapo. Mie nadhan walioandaa mashitaka hayo ndo wanamtusi mheshimiwa kwa kutaka atambuliwe kama bwege
 
Mh sana Rais John Pombe Magufuli ni mtu mzima kidogo, kwa hiyo richa ya kutakiwa kumheshimu kama Rais wa nchi anayepaswa kuheshimiwa na kila raia tunapaswa kumheshimu kama mtu aliyetuzidi umri wengine ana umri sawa na wazee wetu! Kama ambavyo hatuwezi kuwatukana na kuwaita wazee wetu mabwege hatupaswi kumuita Mh Rais Bwege huu ni ukosefu wa maadili wa hali ya juu katika jamii yetu zaidi dhidi ya viongozi wetu. Hata kama watakuwa wamekosea ni lazima tutafute lugha ya staha ya kukosoa na kueleza kutokuridhika kwetu na mwenendo wa mambo.

Katika sakata hili sorry to say this, nimejifunza jambo moja kubwa sana. Kuwa kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili ndani ya jamii yetu na kwamba siasa zinatufanya watu tushindwe kuheshimiana na kuthaminiana yaani unamtoa mtu thamani kisa tu ana mtazamo tofauti na wewe katika jambo fulani jambo ambalo haliepukiki katika jamii iliyostaarabika lazima mtatofautiana.

Siwezi nikasema waziwazi kuwa neno BWEGE ni tusi kwa kiasi gani kama inavyoonekana kwenye kielelezo picha chenye tafsiri hapa chini ila nina uhakika hili neno ni neno linalotweza na kufisha au kushusha thamani ya utu wa mtu mbele ya wengine kifupi ni neno la kudharau na kudhalilisha pia! Kwani kama ilivyotamkwa kwamba fulani ni BWEGE unless mhusika athibitishe ubwege huo vinginevyo hiyo ni defamation(udhalilishaji). Neno Bwege kisawe chake ni neno Mpumbavu kwa wale ambao si mahiri wa lugha ya kiswahili neno kisawe linamaanisha neno sawa na, kwa kifupi neno Bwege ni sawa na neno mpumbavu. BWEGE=MPUMBAVU, kwa maana hii utaona ukubwa wa tatizo la maadili kwa jamii yetu ya kitanzania kwani neno Mpumbavu kama tutakubaliana kuwa ni sawa na Bwege ambalo pia vyovyote vile tukikubaliana ni neno la kutweza liliwahi kutumika hadharani dhidi ya wananchi wasikiunga mkono chama cha mapinduzi na Rais Mstaafu Mheshimiwa Mkapa kipindi cha kampeni! Hivyo basi kama ambavyo tunakubaliana kuwa Rais ametwezwa tunakubaliana pasi na shaka kuwa Mheshimiwa Mkapa aliwatweza wananchi wasiokiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwaita wapumbavu neno ambalo ni kisawe cha neno bwege. Ndugu watanzania hii ni ishara kuwa jamii yetu imeoza si viongozi wala si wananchi wao wote wamekosa busara. Kama mtu aliyewahi kushika wadhifa wa Rais anaweza akatamka maneno hayo dhidi ya wengine itakuwaje kwa mwananchi wa kawaida? Kibaya zaidi jinsi maswala haya mawili yalivyoshughulikiwa inasikitisha zaidi na kujenga matabaka katika jamii, nakumbuka mbali na wananchi kulalamika kuwa wametukanwa si polisi wala kiongozi yeyote wa serikali aliyeinuka na kumkemea, kumuonya wala kumnyoshea kidole Mh Mkapa kwa kile alichokisema ilikuwa kama vile halijatokea jambo lolote kabisa, viongozi na polisi ama waliridhishwa ama walimuogopa muhusika! Leo hii mwananchi wa kawaida, Kachupile, Masikini, Hohehahe, Masulupwete, malapulapu amethubutu kufata nyayo za role model wake Mkapa na kufanya kama alivyofanya anasakamwa, anaandamwa ananyanyasika, amebebwa msombemsombe na polisi kama vile gaidi wa alishababu! Hii inasikitisha zaidi
505a967d118c19f5dd9477fedf3baa73.jpg
[/IMG]
I do not buy you publication, unaandika kwa kujikomba na kudidimiza.mdogo aliyesema neno hilo. We ni mtu hatari sana
 
Back
Top Bottom