Aliyemshushua Mkapa sasa kutuzwa

Msharika

JF-Expert Member
May 15, 2009
947
69
Mwandishi Wetu
Februari 24, 2010


bul2.gif
Ni Clare Short aliyeshupalia Tanzania kutoinunua


NYOTA ya Waziri wa zamani wa Uingereza wa ushirikiano wa kimaendeleo, Clare Short, aliyekuwa mstari wa mbele kupinga ununuzi wa rada ya Tanzania kiasi cha kutofautiana na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa inazidi kung’ara nchini na Raia Mwema imebaini kuwapo kwa maandalizi ya kumpatia tuzo mahsusi kama sehemu ya kutambua juhudi zake hizo ambazo zimebainika kuwa na maslahi kwa Watanzania.

short_1.jpg


Waziri wa zamani wa Uingereza, Clare Short

Kama tuzo hiyo itatolewa, basi, itakuwa ya kwanza kutolewa kwa Waziri kutoka Ulaya. Claire Short alifikia hatua ya kutishia kujiuzulu wadhifa wake katika Bunge la nchini kwake ili kuonyesha msimamo wa kutetea wananchi wa nchi masikini kama Tanzania.

Mama huyo ndiye Waziri aliyeanzisha mzozo wa kupinga ununuzi wa rada hiyo katika Bunge la Uingereza, nchi ambayo ni mfadhili wa maendeleo ya Tanzania, na hasa bajeti ya Taifa ambayo zaidi ya asilimia 30 hutegemea wafadhili.

Hoja zilizokuwa zikitumiwa na Short katika kupinga ununuzi huo ni pamoja na rada hiyo kuuzwa bei ghali tofauti na thamani halisi lakini pia ubora wake kuwa ulikuwa ni wa kutia shaka. Rada hiyo ilinunuliwa kutoka Kampuni ya utengenezaji na uuzaji vifaa vya kijeshi ya Serikali ya Uingereza ya BAE Systems.

Uchunguzi wa Raia Mwema kwa wiki kadhaa sasa umebaini kuwa maandalizi ya utoaji tuzo hiyo yanafanywa na Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), cha jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha wadau wengine kadhaa wakiwamo wasomi mashuhuri nchini.

Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa maandalizi hayo, Mkurugenzi wa LHRC Francis Kiwanga hakuwa tayari kuthibitisha wala kukanusha lakini akiweka bayana msimamo wa kituo hicho kwamba hakiridhishwi na kusuasua kwa Serikali katika kuwachukulia hatua wahusika wa kashfa hiyo ya rada, ambayo kwa maneno yake ni kuwa “chenji iliyorejeshwa ni ushahidi wa kutosha” kuwashughulikia wahusika.

“Kuhusu kutoa tuzo kwa Clare Short siwezi kuzungumzia hilo kwa sasa lakini nikwambie tu kwamba tumekuwa na mtandao rasmi wa kushughulikia masuala kama hayo ya rushwa. Sasa hilo la rada ni sehemu ya hayo, ni suala mahsusi ambalo linafanyiwa kazi ya uchambuzi wa kina ili baadaye tuamue kwa pamoja tunafanya nini…kama suala la tuzo litajitokeza sawa au mengine,” alisema Kiwanga.

Lakini Raia Mwema limebaini, mapema wiki hii, kwamba mazungumzo ya NGOs kadhaa kuhusu suala la kumtuza Claire Short yameshaanza na yanatarajiwa kuhitimishwa karibuni.

Katika hatua nyingine Kiwanga alisema; “unajua kwenye hii nchi kuna tatizo la impunity yaani watuhumiwa waliofanya hata makosa ya wazi ya ufisadi wanalindwa na system licha ya kuwapo kwa ushahidi wa wazi.”

Lakini alipoulizwa kama anaweza kuwa na mifano ya kuthibitisha hilo hakusita kutaja kashfa za Richmond, akihoji kuwa kwa nini Mramba (Basil, waziri wa zamani wa fedha) afikishwe mahakamani kwa kuitia hasara nchi lakini wengine katika Richmond na rada waachwe.

Alisisitiza kuwa licha ya mtandao maalumu wa LHRC kufuatilia suala la rada na kufanya uchambuzi wa kina wa kisheria wanashangaa Serikali kubaki katika kigugumizi cha kuwachukulia hatua watuhumiwa wa kashfa hiyo.

Kampuni ya BAE System iliyoiuzia rada Tanzania tayari imepigwa faini ya dola za Marekani milioni 450 (zaidi ya Sh bilioni 580) kwa makosa ya kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa bidhaa zake katika nchi za Tanzania (rada), Jamhuri ya Cheki, Hungary na Saudi Arabia.

Kabla ya kufikia hatua hiyo ya kupigwa faini, Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai (SFO) ya Uingereza iliipa mwezi mmoja BAE Systems kukiri makosa yake au kufikishwa mahakamani. Katika uchunguzi wake, SFO iligundua kuwa mkataba wa ununuzi wa rada wa mwaka 1999, kati ya Serikali ya Tanzania na BAE Systems uligubikwa na mazingira tata yanayothibitisha kuwapo kwa rushwa.

vithlani_1.jpg


Shailesh Vithlani


Kwa niaba ya maofisa wa Serikali ya Tanzania, ununuzi wa rada hiyo ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani, ambaye anadaiwa alishawishi Tanzania itoe Sh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wa rada hiyo.

Vithlani inadaiwa alipewa dola za Marekani milioni 12 (zaidi ya Sh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha biashara hiyo na kwamba aligawana kitita hicho cha fedha na maofisa saba wa ngazi za juu katika Serikali ya Tanzania.

Vithlani aliripotiwa kutoroka Tanzania miaka mitatu iliyopita akiwa nje kwa dhamana baada ya kufunguliwa mashtaka na alikamatwa mwaka jana nchini Uswizi alikodaiwa kuwa amejificha.

Mbali na rushwa kutumika katika ununuzi wa rada ya Tanzania, BAE pia ilituhumiwa kutumia rushwa katika kukamilisha uuzaji wa ndege moja ya kijeshi nchini Afrika Kusini na uuzaji wa ndege nyingine ya kijeshi ambao haukufanikiwa kwa Jamhuri ya Cheki.

Lakini wakati Serikali ya Tanzania ikibaki kimya kama mtazamaji katika hatua hii mpya ya sakata hilo, Msemaji wa BAE, Dick Olver anasema; “Kampuni ya BAE inajutia yaliyotokea na inakubali kubeba mzigo kwa matatizo yaliyotokea.”

BAE ilikiri kuwapo malipo ya kamisheni kwa mtekelezaji wa biashara hiyo ya rada kwa Tanzania ambayo inaelezwa kuwa hayakuwekwa wazi kama ilivyotakiwa. Kutokana na kasoro hiyo, BAE imekubali kutoa pauni milioni 30 ambazo baadhi zinatarajiwa kuletwa Tanzania.

Mkurugenzi wa SFO, Richard Alderman ameripotiwa kufurahia makubaliano yaliyofikiwa (utoaji faini) na kuongeza kuwa huo ndio utakuwa mwisho wa uchunguzi wao kwa kampuni ya BAE.

Makachero wa SFO pia waliwahi kufika nchini na kuwahoji baadhi ya wahusika wa kashfa ya rada hiyo iliyogharimu Tanzania Sh billion 40. Inaelezwa kuwa baadhi ya vigogo waliohojiwa nchini ni wa kutoka Wizara ya Fedha na Wizara ya Miundombinu, ambao zamani walikuwa wakifanya kazi katika Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi. Wizara ya Miundombinu imetokana na kuunganishwa kwa iliyokuwa Wizara ya Ujenzi katika Serikali ya Awamu ya Tatu.

Taarifa hizo za maofisa kadhaa wa serikali kuhojiwa ziliwahi kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, kupitia baadhi ya vyombo vya habari nchini. Kamishna Manumba alithibitisha kwamba si wakala huyo pekee aliyehojiwa na makachero hao bali pia wengine waliodaiwa kuhusika nao pia walihojiwa.

"Ndiyo watu mbalimbali wamehojiwa, si wakala pekee, lakini walihojiwa watu wanaoelezwa kuhusika na ununuzi wa rada hiyo," alithibitisha Manumba akiongeza: “Unataka nikutajie majina, siwezi kutaja, wala idadi yao, ila ninachosema watu mbalimbali waliohusika katika ununuzi wa rada walihojiwa.”

Inadaiwa kuwa uchunguzi wa makachero wa Uingereza kutaka kubaini mchezo mchafu katika ununuzi wa rada hiyo unatokana na kamisheni ya asilimia 30 iliyolipwa kwa wakala, ikidaiwa kuwa ni kubwa kuliko kamisheni za asilimia 10 zinazotolewa katika ununuzi wa kawaida.
 
kweli "MiTanzania" hovyo kabisa watu ambao wala sio raia wanatupigania huko kwao huku wenye nchi na wenye hiyo fedha iliyoliwa wala habari hatuna, tunaona ni kama mchezo wa kuigiza, kama jamaa wameshakubali kuwa walifanya kitu fake, inashindikana nini kwa chenge at el kutiwa nguvuni? kama serikali inashindwa vipi kuhusu raia tukaamua kuweka maandamano ya kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua wahusika?
 
Na wengine tulioandika barua hadi ikasomwa kwenye House of Commons na MP Lamb tutatuzwa..? au ndiyo sadaka yenyewe ya kujitolea!?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom