Uchaguzi 2020 Aliyemshauri Lissu baada ya kuadhibiwa na NEC anaweza kuendelea na shughuli za chama amemshauri vibaya

Bekiri

Member
Jun 30, 2013
14
63
Imeandikwa, kiburi si maungwana na mtoto mkaidi hawezi kufaidi hadi siku ya Iddi. Tundu Lissu anaingia katika kundi hili kwa kushauriwa vibaya au kukaidi ushauri mzuri.

1. Aliemshauri Lissu kuwa baada ya kuadhibiwa na Kamati ya Maadili ya NEC anaweza kuendelea na shughuli za Chama kama Makam Mwenyekiti wa Chama amemshauri vibaya.

Tundu Lissu ni mmoja, hakuna nafsi mbili ktk mtu mmoja. Popote atakapokuwa Tundu Lissu ndipo alipo Mgombea wa Urais wa Chadema na Makam wa Mwenyekiti wa Chadema. Hakuna mstari wowote wa kutenganisha kati ya Lissu Mgombea na Lissu M/Mwenyekiti.

Kukosekana kwa tofauti hiyo ndio maana popote alipo mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli ndipo alipo Rais wa JMT. Huwezi kuutofautisha ugombea wa John Pombe Joseph Magufuli na Urais wake au Uenyekiti wake wa CCM. Hivyo hivyo huwezi kuutofautisha ugombea wa Tundu Lissu na Umakam Mwenyekiti wake vinginevyo ni kujidanganya tu.

Aliemshauri Lissu kuwa baada ya kuadhibiwa anaweza kuendelea na kazi za kisiasa amemdanganya, amemshauri vibaya na amempotosha bure. Anachagiza vurumai za bila sababu. Lissu ashauriwe vizuri, ugombea wake na Umakam Mwenyekiti wake ni alfa na Omega, huwezi kuvitenganisha. Kimoja kinaathiri kingine!

2. Aliemshauri Lissu kuwa, kufungua matawi ya Chama au kutembelea masoko sio shughuli za Kampeni amemshauri vibaya, amemdanganya. Ni bahati mbaya kuwa Lissu licha ya kuwa Mwanasheria amedanganyika kirahisi mno. Mazingira na wakati vinanguvu zaidi ktk kuamua kesi, Lissu anafahamu hilo. Hakuna mstari wowote unaotenganisha kufungua matawi ya chama, kutembelea masoko na shughuli za Kampeni kwa wakati huu. Wakati uliopo sasa na mazingira anayokwenda kutembelea Tundu Lissu ni ushahidi wa wazi kuwa ameamua kufanya kampeni kwa mlango mwingine. Ni kosa, ni ukaidi.

Kampeni ni hamasa, kampeni ni ushawishi. Kufungua matawi ya vyama ni hamasa na ushawishi kuwa Chama kipo hai, hii ni kampeni zaidi kuliko kufanya mkutano wa hadhara.

Kuwatembelea watu ktk soko na maeneo ya wazi ni hamasa na ushawishi pia. Watu waliosoma elimu maalumu watanielewa vzr hapa kwamba kuna lugha ya picha na alama. Unaweza kufika mahala bila kuongea jambo lolote, ukasabahi kwa ishara na kuondoka lkn mavazi yako na muda vika-deliver ujumbe uliokusudiwa kwa watu. Kwenda Kibaha, kukutana na Wanachama au Wananchi hata bila kuongea jambo lolote ni kampeni kwa Lissu. Kati ya nafasi ya Umakam Mwenyekiti na nafasi ya Ugombea Urais kwa Lissu inayotangulia kwa sasa ni ya Ugombea. Hii ni principle ya wakati!!

Ushauri:

1. Mwambieni Tundu Lissu akili nyingi mbele ni giza. Awasikilize wenzake, aachane na mpango huu hauna faida. Polisi watamzuia kwa sababu hawawezi kutofautisha Ugombea wake na Umakam Mwenyekiti wake. Sio Polisi tu, hata wewe huwezi kwa sababu hakuna tofauti hiyo.

Polisi ndicho chombo chenye dhamana ya kusimamia na kushurutisha utekelezaji wa sheria. Ninahisi wataendelea na kusimamia utaratibu huu bila kujali kwa sababu ni wajibu wao, tusiwalaumu.

2. Mwambieni Tundu Lissu aache kukifanya kichwa chake kigumu, kitavunjika na asipate dawa. Aache kutukana watu kila kukicha, binadamu tumeumbwa na vinyongo. Siku Polisi wakikinai kuitwa wajinga au siku wakitamani kuufanya ujinga hadharani itakua hatari kwa nchi yetu. Hii ni nchi yetu sote, tuilinde

3. Mwambieni Lissu, walio nyuma yake ni ndugu zake ktk Chama, ndugu zake ktk damu na ni Watanzania wenzetu. Asiwatumie vibaya, majuto ni mjukuu. Likitokea la kutokea hasara ya kwanza ni kwetu sisi kama nchi, aachane na mzaha huo. Ni kosa kutumia njia haramu kuutafuta mwisho halali, Ikulu mtu hawezi kwenda kwa kupita ktk mifereji ya damu za watu. Aache mara moja!!
#MitanoTenaKwaJPM.
 
Inaonekana unaijua vizuri sheria. Pia maamuzi ya kamati.
Amezuiwa kufanya kampeni au shughuli zote za siasa?

Halafu, mbona kama hii ni kuumizwa na vitu vidogo ambavyo ukivipotezea vinakuwa kama havipo na madhara yake hayataonekana?

Nakumbuka, Shibuda aliwahi kufungiwa kufanya kampeni kwa muda fulani, lakini athari yake ikawa upande wa waliofurahia kufungiwa kwake
 
Ushauri wako ni mzuri ila ameshachelewa... leo nimepita sokoni mabibo wafanya biashara wana wanamchekaaaa wanasema kajawa dharau yule

Nikawaambia wazee wangu hayo maneno msubirini akija mmwambie🤗🤗
 
Mkuu hata bodyguard wa Rais akiwa kwenye shughuli za chama anavaa gwanda za kijeshi(bakabaka)... na akiwa kama Rais anavaa sare ya officer wa jeshi hata hilo uelekezwe.
 
Lisu ana kiburi, makusudi na ujuaji

Dawa ya wakaidi mithili ya Lisu ni kuchukuliwa hatua zaidi na zaidi
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom