Aliyemrushia Bush Viatu Kuachiwa Huru Mwezi Ujao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyemrushia Bush Viatu Kuachiwa Huru Mwezi Ujao

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Sep 8, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Bush akikwepa kiatu alichorushiwa na mwandishi wa habari wa Iraq Saturday, August 29, 2009 4:03 PM
  Mtangazaji wa televisheni ya Iraq ambaye alitupwa jela baada ya kumrushia viatu vyake rais wa zamani wa Marekani George W. Bush atatoka jela mwezi ujao baada ya adhabu yake kupunguzwa. Muntadhar al-Zeidi mtangazaji wa televisheni ya Iraq alimkosa kosa Bush na viatu vyake namba tisa ambavyo alijaribu kumpiga navyo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye ziara yake ya mwisho nchini humo.

  Mwanasheria wa Zeidi, Karim al-Shujairi alisema kwamba Zeidi ambaye alitimiza umri wa miaka 30 mwezi disemba ataachiwa huru mwezi ujao baada ya adhabu yake kupunguzwa.

  Awali Zeidi alihukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kukanusha kosa la kumshambulia kiongozi wa kigeni lakini mahakama baadae iliipunguza adhabu hiyo kuwa mwaka mmoja kwakuwa Zeidi alikuwa hana historia ya uhalifu.

  Al-Shujairi aliliambia shirika la habari la AP kuwa amepata ripoti kutoka mahakamani kuwa Zeidi ataachiwa huru septemba 14 ikiwa ni miezi mitatu kabla ya tarehe yake ya kuachiwa huru.

  Katika tukio hilo lilitokea mwezi disemba mwaka jana, Rais Bush wa Marekani alifanikiwa kuvikwepa viatu viwili alivyorushiwa na Zeidi wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ziara yake ya siri ya mwisho nchini Iraq kabla ya kuachia ngazi urais wa Marekani.

  Zeidi alimrushia Bush viatu vyake baada ya kukasirishwa na uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka 2003 na kufuatia kauli ya Bush kwenye mkutano huo na waandishi wa habari kuwa vita ya Marekani nchini Iraq bado haijaisha.

  Wakati serikali ya Irak ikisema kuwa Zeidi ameitia aibu nchi hiyo na kumtaka mwajiri wake mwenye makazi yake nchini Misri aombe msamaha, mwajiri wake alimpongeza Zeidi na kutaka kuachiliwa kwake haraka iwezekanavyo.

  Zeidi alipongezwa na mataifa ya kiarabu na kuchukuliwa kama shujaa kiasi cha kutengenezewa sanamu la ukumbusho la kiatu chake alichomrushia Bush.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2946950&&Cat=2
   
Loading...