rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 15,189
- 20,156
Hawa makocha wa Burundi waliojazana huku wamefundisha top timu gani kwao.Kwanza kujiendeleza wenyewe bila support ya government ni ngumu. Kumbuka licences za uefa can cost up to 30million. Tuwe wakweli makocha wangapi wazawa wanaweza kulipa that amout ukizingatia wakati wao wanacheza pay ilikuwa magumashi?
Kuhusu kufundisha simba na yanga hapo wala hamna tatizo. Ni nadra sana mtu kwenda kufundisha nje ya nchi kama hajaweza fundisha top team kwenye nchi yake. Mfano hai tunao hapa tanzania. Kayuni pekee alienda fundisha kenya akitokea yanga. Leo hii tunamuona mosimane al ahly kwa sababu alifundisha mamelodi ambayo kupitia champions league ndio akaonekana. Chukulia italia pia..ancelotti, conte, capello wote walifundisha timu kubwa nchini kwao ndio wakatoka nje. Hiyo ndio trend kwenye mpira.
Ofcoz timu ya taifa sio ya majaribio. Kwa kupitia mikakati mizuri unakuwa umeshamuandaa kocha wakuja kurithi national team. Huyo kocha wa wapinzani wetu jana amefundisha u20 women national team na ndio kapewa timu ya wakubwa. Ni mchakato mrefu na mipango ya muda mrefu sio kwamba unakurupuka tuu.
Baraza alikuwa anafundisha top timu gani kwao.
Kaseja pamoja na kuwa bado anacheza tayari ameshaanza kusomea ukocha, kwa mshahara na marupurupu anayolipwa Matola ni wazi ana uwezo wa kulipa miliono 30.