Aliyempiga misumali Kichuya na Mavugo inatosha, mtatuua mashabiki

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,053
114,521
Uzi unajieleza.

Kama kuna mtu amempiga misumari kijana wetu mahiri Shiza Kichuya na Muvugo, basi inatosha jamani, mashabiki tunaumia sana. Tunakwenda kwenye mabanda ya kutizama mpira tukiwa hatuna raha kabisa. Mkishinda kagoli kamoja mnamshukuru Mungu.

Hawa vijana wako vizuri sana, ukiwaona uwanjani wanavyohaha kurudisha imani kwa sisi mashabiki unaona kabisa kwamba wamefungwa miguu.

Tuacheni na sisi tufurahi kidogo katika kipindi hiki kilichobaki, wewe mpiga misumari fikiria toka mwaka gani hatujachukua kombe hili

INAUMA
 
Uzi unajieleza.....Kama kuna mtu amempiga misumari kijana wetu mahiri Shiza Kichuya na Muvugo, basi inatosha jamani, mashabiki tunaumia sana. Tunakwenda kwenye mabanda ya kutizama mpira tukiwa hatuna raha kabisa. Mkishinda kagoli kamoja mnamshukuru Mungu.

Hawa vijana wako vizuri sana, ukiwaona uwanjani wanavyohaha kurudisha imani kwa sisi mashabiki unaona kabisa kwamba wamefungwa miguu.

Tuacheni na sisi tufurahi kidogo katika kipindi hiki kilichobaki, wewe mpiga misumari fikiria toka mwaka gani hatujachukua kombe hili

INAUMA
....umenikumbusha timu yangu ya Liverpool.

aisee unaweza kusema sasa hivi wachezaji wote wamepigwa misumari aisee!!
 
Ndo uwezo wao ulipoishia kwani Kichuya VPL kaanza kucheza akiwa na Simba??Mtibwa liipa nini??
 
Hawana uwezo sema mliwakuza mwisho wa siku wamefeli...wanalambalamba tunazibua palipoziba bado kandambili ya Jangwani lazima mjini heshima iwepo
 
Mabeki wameishajua ujanja wa Kichuya. Hakuna cha misumari hapo. Sasa inabidi ajiongeze ili aje kivingine. Ndivyo mpira ulivyo.
Zaidi ya hapo, kila timu imeishajua mbinu za Omog. Lazima aje na plan B wakati mwingine.
 
Aisee ni kweli wamewapiga misumiri kabisa na sijui hizo misumiri kama watawaregezea..!!??

Aliye wapiga misumari hao vijana wawili ni yule kijana aliyetolewa kwa Mkopo.

Halafu kwa bahati mbaya ameondoka na wamesahau kumkumbusha achomoe misumari yake! lol
 
Mabeki wameishajua ujanja wa Kichuya. Hakuna cha misumari hapo. Sasa inabidi ajiongeze ili aje kivingine. Ndivyo mpira ulivyo.
Zaidi ya hapo, kila timu imeishajua mbinu za Omog. Lazima aje na plan B wakati mwingine.
Huu uzi unani kumbusha baadhi ya vijana wangu wa pale Jangwani....

Masahbiki wa Yanga SC wangekuwa wenye kuamini sana masuala ya ushirikina basi uzi kama huu ungekuwa umeanzishwa kuhusu Uwezo wa Ngoma na Kamusoko kipindi anawasili ..

Kwenye Ligi hii kuna tabia moja! Ukija msimu wa kwanza ukashindwa kuonyesha makucha yako basi huwezi kuonyesha makucha yako hata kama ukicheza misimu 10....(ndio hayo kama ya Mavugo)...

Endapo ukifanikiwa kuonyesha cheche msimu wa kwanza, basi ujue msimu wa pili hauto kuwa kama wa kwanza...
(Kwenye hii ligi kuna tabia ya kusomana kwa wachezaji)...

Ni nadra sana mchezaji kuingia VPL na Ku-click kwa misimu kadhaa mfululizo (nadhani hili ameliweza Tambwe kwa kiasi kidogo mno),
 
Back
Top Bottom