Aliyempiga Kofi Mwinyi Alazwa Wodi ya Vichaa Muhimbili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aliyempiga Kofi Mwinyi Alazwa Wodi ya Vichaa Muhimbili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Mar 27, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  IBRAHIMU Saidi [26] kijana aliyempiga kibao Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, amelazwa wodi ya watu wenye matatizo ya akili Muhimbili.

  Ibrahimu amelazwa Muhimbili kutokana na uongozi wa Magereza kuamua kumpima kutokana na vitendo vya ajabu ambavyo alivyokuwa anavifanya Gerezani vya kushangaza na si vya kawaida.

  Hatua hiyo ya kulazwa imekuja baada ya kuonekana kuwa ana matatizo ya akili kutokana na vipimo vilivyochukuliwa na madaktari kuonyesha kuwa ana matatizo hayo.

  Wiki mbili zilizopita Ibrahimu alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja na Hakimu Neema Chusi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kosa lake hilo alilolifanya la kumpiga Rais huyo mstaafu.

  Source: Nifahamishe.com
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haya wale watetea haki za binadamu, kazi hiyo. Kamteteeni chizi, yaani huyu kijana afungwe kwa ajili ya kumchapa kofi Mwinyi hali ya kuwa ni chizi? haki iko wapi? Au sheria zetu zinaruhusu chizi kufungwa?
   
 3. Kamjingijingi

  Kamjingijingi JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Haa!!!! hiyo tena nikulindana huyu siyo chizi,mbona alijua haram kutetea condom? akajitolea kwaajili ya mungu tena.anaogopa nini mwaka moja? kama yeye mcha mungu?! wasituharibie amani tz!!
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kama ameingia uchizi basi wale usalama waliochukua sheria mikononi mwao ndio waliomsababishia uchizi huo,kushindwa usalama wale kudhibiti ulinzi ni kosa ambalo wanatakiwa kufikishwa mahakamani ,lakini nani atawafikisha ?
   
 5. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi unadhani kuwa chizi kuna vitu huvifahamu. Mfano machizi tunaowaona barabarani hupisha magari. Ama wakati mwingine chizi akiona mbwa huogopa. Suala la huu ugonjwa ni kuwa kuna wakati unaweza kutulia, na kuna wakati hulipuka, tena hulipuka hasa unapokuwa na matatizo (kama hasira, ugonjwa, mawazo nk). Hivyo huyu jamaa huenda alilipuliwa kwa Mzee Mwinyi kuhalalisha Kondomu tena kwenye hafla ya Dini.

  Kamanda wa Polisi wa Dar es Salaam baada ya tukio aliripotiwa akisema kabla ya mtuhumiwa kupelekwa mahakamani atapelekwa polisi kuchunguzwa akili. Hii ni haki yake, lakini hakupelekwa japo waliahidi. Yote hii ni kuonyesha jinsi gani haki za wanyonge hazilindwi. Hata kama mtu amefanya kosa, ni haki yake kufanyiwa ubinadamu.
   
 6. Z

  Zion Train JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 503
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mama yake mzazi amekwishaomba samaha kwa mzee ruksa, naye amemsamehe, lakini haiwezekani akaachiwa tu hivi hivi, vinatafutwa vijisababu tu, nchi yetu kwani amuijui, mgao wa umeme na vijisababu tu vya kutaka kununua hayo majenereta.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nadhani hospitali ndizo huchunguza akili wagonjwa na si polisi!
   
 8. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Nadhani kuna uchizi wa aina nyingi mimi si Daktari. Wale mashehe walipomuomba radhi Rais Mstaafu juu ya kile kitendo cha huyu bwana mdogo, walitamka wazi kuwa huyo kijana hakuwa na akili timamu (itakuwa from their own sources). Nadhani chizi pia huwa anafikiria na anajuwa anafanya nini isipokuwa kuna wakati fulani anazidiwa nguvu na uchizi na ndipo anapofanya mambo yasiyokuwa na busara kama kusababisha vurugu, kuvua nguo, wengine hukaa na kulia tu na kadhalika.
   
 9. Kamjingijingi

  Kamjingijingi JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Haki za binaadamu ni zakila mtu .tena hazimruhusu kichaa kumpiga mzima .wala mzima kumpiga kichaa.kama imethibitika ni kichaa!, apelekwe mirembe asije akatuumiza njiani buree!!maana watu wote wana haki za binaadamu .tena mwnyi anapaswa kua nahaki zaidi tulimchagua kua kiongozi wetu. na tena nikioo cha jamii .tena kichaa huyo kuwekwa ndani ni usalama wake pia.vinginevyo saa hii mngemsahau kwajinsi wanainchi walio mchagua walivyo lipokea kwa uzito mkubwa .
   
 10. Wun

  Wun JF-Expert Member

  #10
  Mar 27, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 353
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  IBRAHIMU Saidi siyo kichaa kwa habari zilizo patikana kutoka gerezani bali anateswa sana na magereza pamoja na maofisa wa usalama kwa kitebdo huku wakimuita mfano mbaya kwa taifa mateso anayoyapata ni pamoja na kunyimwa chakula.
   
 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Hakuna mtu mwenye haki zaidi ya mwenzie mbele ya sheria. Ni kweli kwamba kuna watu wanao pendelewa na jamii au watendaji zaidi ya wengine kinyume cha sheria, na kuna wale wanao nyanyaswa na jamii na watendaji kinyume cha sheria. Vitendo hivyo ndiyo hupelekea watu wengi kudhani kwamba kuna kundi la wenye haki zaidi ya wengine.

  Mbele ya sheria,Watu wote ni sawa.
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kwa ujinga wa magereza na kutaka sifa wanaweza wakaisababishia serikali hasara ya mabilioni,yaani wakili anaejiamini anaweza kabisa kuitafuta kesi hiyo na kuinunua kisha akatiwe chake baada ya malipo.
   
 13. K

  Karandinga Member

  #13
  Mar 27, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 66
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  The more things change the more they remain the same! Hii technique ya kuwa commit kwenye mental institutions watu waliofanya vitendo vya namna hii dhidi ya viongozi wa kitaifa ilikua inatumika sana Soviet Union enzi za Stalin. In a way it is a dissent stifling technique. Kwamba kijana huyu kafanya kitendo kama hicho ni laazima awe na matatizo ya akili!! They did the same thing kwa yule jamaa aliyemrushia Bush viatu. Huko ughaibuni viongozi wa kisiasa na kibiashara huwa wanakumbana na kash kash kama hizi na husikii mtu kapelekwa mental institution...It's a "face saving" ploy in my opinion. Having said that, I disagree with what the young man did to Mzee Mwinyi..
   
 14. Kamjingijingi

  Kamjingijingi JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  I fully agree with karandinga, personally I feel that its a face-saving exercise, if the accussed was not sane then one would not expect him to be allowed to partcipate in the function and have easy access to the high table, asingekuwa ustadhi, mwenye sifa ya upole na mcha mungu kama walivyosema baadhi ya waumini, walikubaliana na msimamo wake ! Nionavyo mimi, huyu si mwendawazimu, bali kitendo hicho kilikusudiwa na ambacho ni cha kusikitisha sana ! Alitumia dini atimize lengo lake !
   
 15. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaaaaaaaaaaaaa!!!!. Kweli Mkuu Masanilo, nilikuwa namaanisha kupelekwa Hospitali kuchunguzwa akili lakini nikakosea na kuandika Polisi.
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Mar 28, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh,
  Ama kweli nchi yetu inachekesha.. Huyu kijana kafungwa jela mwaka, leo ndani ya kifungo anaonekana ana matatizo ya akili?...haikuchukunguzwa toka mwanzo wakati kesi ikiwakilishwa mahakamani!
  Nina hakika kapelekwa Hospitali ya vichaa kuongeza adhabu kwa kijana huyo ndio mtindo wa nchi za Kijamaa..
   
Loading...