aliyelaaniwa na Dr Slaa na watu wa Ismani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

aliyelaaniwa na Dr Slaa na watu wa Ismani

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by kweleakwelea, Dec 30, 2010.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  jana mchana nilikuwa ninaendesha gari yangu nikapita meneo ya mvumi misheni kule kule mjia ya kwenda kwa mzee malecela aka tinga tinga. nikiwa ninapumzika kidogo na kunywa soda ndani ya hoteli moja kijana mmoja aliyeonekana mtanashati alikuja pale hotelini na kudadisi gari iliyokuwa pale nje ni ya nani. akajibiwa ni ya yule pale bwana. ndio akaja pale na kuomba kama inawezekana apate lifti. nlimkubalia na nikamwambia tutapomaliza shughuli pale mjini tutaondoka naye. hivyo akae stand by. awali alidai kuwa basi limechelewa.

  masaa mawli baadae nikawa tayari kuondoka pale na ndipo kijana yule alitokeza kwa mbele na kunisimamisha. nilishangaa kwani nilitegemea angekuwa ameishaondoka kwani mabasi yaliishakatiza. nikajua lazima iko shida.

  njiani wakati tunakuja mjini dodoma, nikamdadisi shughuli zake, akaniambia ni mhitimu wa UDOM, na huku amekuja kutafuta kazi ya kufundisha. amepigwa dana mara tatu. nikamuuliza kumbe wewe ni graduate. kumdodosa kuhusu wabunge wake akasema anawafahamu wengi wa iringa (ambako ni kwao) na huwa alikuwa anahudhuria shughuli zenye upuche wakiwa hapa dodoma.

  nilipomuuliza mchango wa mafuta nikagundua kuwa hakuwa hata na nauli ya kumtosha kufika mjini ambayo ni shilingi 3000. kwamba amebakiwa na shilingi 2000 tu! akadai kuwa jk aliwahi kuwadanganya udom kuwa graduates watapata ajira as soon as wakiigraduate!!! tena kabla wale wa vyuo vingine kuajiriwa???

  nikamuuliza kama graduate anadhani kuwa Tanzania kuna future na ccm? mwanzo akajikanyaga lakini akakiri future haipo! hakuamini kuwa huku mtaani kuna mateso makali sana chini ya ccm. akadai kuwa hapo alipo hana tena nauli wala chochote... tena anasubiri kiama cha bei za umeme kimmalize kodi zikipanda!

  yeye akadai ni muumini wa cdm ila alikuwa anafuata ubwabwa kweny pati za ccm... katiak hili alinitolea ushuhuda jinsi aliyelaaniwa na wanaismani anapata shida! kwamba mgombea wa chadema kule ismani bwana kapwani aliyekuwa na uwezo wa kushinda alipewa 13 million na lukuvi ili aachie kugombea. wakatui wa kampeni Dr SLaa alitamka katima mkutano kuwa kama wewe umewasaliti watu wa ismani kwa kujitoa kwenye kinyang'anyiro basi na damu ya watu hawa itakuwa juu yako!!

  kilichotokea baada ya hapo ni kuwa muda mfupi baadae yule mtu alipooza hata kabla ya uchaguzi na akawa kama zezeta. kijana yule akiwa ndani ya gari langu alipiga simu iringa kutumia simu yangu kujua hatima ya mtu yule! taarifa ikaja kuwa kwa sasa anatembelea magongo!!!

  hata leo naamini kuwa damu ya masikini na watanzania watesekao kwa ajili ya ccm, rostam, werema, el na wote iko juu ya watoto wa wanaccm na wanaoifagilia iendelee na ujambazi!! itawapata hata kabla jua halijatuwa. ni dhambi zaidi kwani masikini hawa walimchagua Dr Slaa lakini wao kwa misuli yao wakapindisha!!!

  haya sasa wanajf..... je kupooza huku ni hiyo laana au mtaalamu lkv alituma kipapai lakini kilichelewa kurindima?

  nawasilisha  do you see any future
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Wakati mwingine huwa nafurahia Mateso ya watu hasa waliokua wakiipigia debe ccm, Mfano Juzi binamu yangu , shabiki mkubwa wa ccm huko Dar, alinitumia email akilalamika juu ya kuongezeka kwa gharama za umeme, wakati huo mtoto wake anaesoma chuo cha IFM akinyimwa mkopo, kufuatia ongezeko la ada chuoni pale, na bodi imekataa kulipa ongezeko.
  Niliacha hata kujibu email yake, na moyoni nikajisemea na akome, maana lengo lake lilikua ni kunitaka nimchangie ada ya mtoto wake huyo.
  Na bado ninatamani apate mateso zaidi , ili 2015 aweze kuelewa somo, kuwa ccm ni chama Mufilisi, kinachoongozwa na mijitu isiyo na staha wala maadili. watu wasio na haya hata chembe, mabingwa wa fitina na wazandiki kabisa.
  Na ninatamani laana zaidi iwaangukie manazi, wasaliti na kila alieisaidia ccm kushinda.
   
 3. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  nilichofanya ni kuchukua shilingi 1500 kati 2000 yake na kumwandikisha kadi ya chadema ikiwa ni bei ya kadi na ada ya mwaka! nikamwambia enenda zako na ufumbuke macho!
   
 4. d

  dotto JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  KAziiiii ipo inakuja. Tutakoma na Ujinga wetu. '' Naa-----pa nahidi mbele ya Chama ----------"
   
 5. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ngoja maisha yawe magumu tujifunze kutumia hata akili alizotupa Mungu. Rushwa ktk chaguzi za CCM ilikuwa wake up call kwamba chama hiki kimepoteza mwelekeo. It doesn't take a prophet to know that CCM is no longer interested in Tanzania nor Tanzanian. Sorry for patriots who still cling to CCM but you have no voice and I wonder what you are doing their!

  I feel pity for all who still think CCM is political party!
   
 6. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Nilisikia alipewa milioni 40, akaumiza sana matarajio ya wazee waliokua wamemuandaa kumtoa mbunge wa sasa...
   
 7. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Watu wanaoumia zaidi ni wale waliokuwa wanavaa kofia na jezi za yanga wanajuta
   
 8. mchillo

  mchillo JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 433
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwa hakika kipindi hiki cha awamu ya pili cha walaghai hawa (CCM) kitakuwa cha maumivu makubwa na matokeo ya maumivu haya yanaweza kudumu miaka mingi hata baada ya utawala wao kumalizika. Inasikitisha sana kuona chama hiki kilichokuwa tegemeo la wakulima na wafanyakazi masikini sasa kimetekwa na majambazi wakitumia jina la chama kilekile (CCM), kuvaa nembo zao na kuzungumza lugha inayofanana na CCM iliyouliwa nao. Si siri kwamba CCM ya sasa ni tofauti na ile ya Nyerere ambayo mwenyewe aliikosoa ya sasa akiishangaa kwa kuwakumbatia matajiri na kuwasahau walengwa wa msingi , ndiyo wakulima, wavuvi na wafanyakazi. CCM ya sasa inazungumza lugha ya fedha tu bila kujali zinavyopatikana, inazungumzia ubaguzi baina ya wanachama wake na kuwakana baadhi yao kwamba "Si raia" wa nchi hii; jambo lililoamsha laana ya jumla kwa chama kizima kadiri ya utabiri ya mwasisi wa CCM Hayati Mzee Nyerere aliyewaasa kabla ya kifo kwamba hakuna dhambi mbaya zaidi ya ile ya ubaguzi. Nyerere alinena waziwazi kwamba dhambi ya ubaguzi "Haiishi", kwani baada ya kuwabagua watu kikabila itafuata kidini, kijimbo, kirangi n.k.
  Kwa hiyo sishangai kumsikia Kikwete na wana CCM wenzake kuhubiri juu ya kinachoitwa "Udini" kwani ni sehemu ya laana hiyo waliyoianzia kwa kada wao Dr. Salim na baadae kusambaa kwa wanachama wao kadhaa na sasa, baada ya "Kufilisika" kisera wamedandia hoja ya "Udini". Kikwete na CCM yake sasa wana "Display" characteristics zote za kufilisika kisiasa kulikotabiriwa kwa uhakika kabisa na mwasisi wa Chama wanachodai chao yaani CCM ambayo kwa kweli si CCM bali ni genge la wahuni na wahalifu waliojiunga pamoja na kutumia jina, alama, nembo na hata lugha na miisamiati ya ki-CCM ambayo kwa hakika si CCM bali ni mafisadi na manyang'au waliojivika ngozi ya "mwanakondoo". Ni jukumu letu sasa sisi Great thinkers kupuuza "Porojo" zote za wanasiasa waliofilisika hawa na kusonga mbele katika juhudi za kuleta mabadiliko kwa nchi yetu. Tumeanza na Katiba ambayo sasa mwitikio wake unaelekea kuisomba CCM kwa dhoruba kali ya kimbunga, naona hata shoga zao CUF wamegundua hilo na kudandia gari kabla halijawaacha (Maana juzi tu wamefanya maandamano) ambayo naamini yangekuwa yamefanywa na CHADEMA; haohao CUF wangeshirikiana na CCM kuyabeza na kuyalaani.
  Ni muhimu wa JK na CCM wenzake kufahamu kuwa mbegu wanayoipanda sasa ya ubaguzi wa asili, rangi na udini inawezakuliletea taifa hili hasara kubwa ya uwezekano wa kuzuka hali kama iliyotokea Rwanda, Kenya, inayotokea Nigeria na Ivory Coast sasa. Hayo yakitokea JK na CCM yake hawataepuka kusutwa na jumuia ya kimataifa na hata kufikishwa The Hague.
   
 9. t

  tumpale JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kweli wadu mmenena, haya mateso yaendelee, kofia, kanga na elfu tano zinawatokea puani. umeme umepanda, sasa hivi mchakato wa kupandisha nauli unaendelea. Hata miezi mwili haijatimia hali namna hii.
   
 10. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kijana mmoja anayefanya kazi katika kampuni ambayo ninaiongoza alikuja kwangu kuomba nyongeza ya mshahara eti maisha yamekuwa ghali. Yeye hufanya shughuli zinazoitwa staff duties. Lakini katika kampeni yeye alikuwa mpiga debe ( kama katibu mwenezi wa tawi ccm). Analipwa juu kidogo ya kima cha chini. Nikamwambia kusema ukweli hatutakuongeza chochote. Akamaka kwa nini? Ni kamwambia tunatekeleza ilani ya ccm. Wewe uliitangaza sana. Chadema walisema watafikisha kima cha chini 320,000.= hapo hata kampuni yetu tusingekuwa na udhuru ingetulazimu kuilipa. Sisiemu wakasema hiyo haiwezekani (Wewe ukakubaliana na ccm tena ukawashawishi na wengine. Sasa mmeshinda hivyo sisi tunatekeleza tu) Kijana akaondoka ameinama, amesema mzee nitakuona tena Januari. Sasa tena na hizi bei za umeme sijui nimjibu nini.
   
 11. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini tuendelee na kampeni za kuitoa CCM madarakani hata kama uchaguzi bado miaka 5. Kuna wajinga bado hawajui kwa nini tunateseka mno. Nguvu ya umma ni kubwa kuliko FFU.

  Tuendelee kupiga kelele mpaka watashindwa kula hizo pesa.
   
 12. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #12
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Namsikitikia kwa ujinga wake...but well done Omulangi!
  Nadhani ameelewa vema na next time hatakurupuka ka vijihela visivyo na msingi!
  I love that :thumb:
   
 13. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  They are our relatived and beloved...but let them learn the hard way!
   
 14. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #14
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmmh na maisha yamekuwa magumu kweli, halafu hawa watu wa ccm wa mtaani kuweni sana macho nao, wakija kukukopa hawalipi, ziliwalevya tshet, na pilau sasa wameanza kulalama mapema, na wale waliokuwa wanawapigia debe wanaomba tena bungeni kuongezewa mshahara, hawawakumbuki hawa wapiga debe kuwa waliota nundu mikononi kupiga hilo debe
   
 15. Kagemro

  Kagemro JF-Expert Member

  #15
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  sijapenda heading kidogo imekaa kushoto,aliyelaaniwa na Dr wetu wa ukweli?navyomjua huwa hajui kulipa kisasi wala kutukana. wananchi inawezekana maana watu wa huko wanahasira sana.
   
 16. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #16
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Maandiko yana mstari unasema, Watu wangu wanapotea kwa kukosa maarifa!!
  Wafanyakazi ambao TUCTA ilikuwa inawapigania walisahau yote pale T-shirt,na kfia za kijani zilipogawiwa, wakasahau huyuhuyu ndo alisema kura zenu
  sizitaki! wakasahau kima chao cha mshahara.
  Tesekeni mpate akili, Nyangau nyie.
   
 17. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii ni hatari, mbona mimi nilisikia kwapwani amehamia ccm
   
Loading...