Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,525
- 217,787
Kwa Mujibu wa Katiba ya Tanzania, Waziri wa Sheria ndiye Mshauri wa Rais wa Masuala yote ya kisheria na mambo ya Katiba ya Nchi, hivyo basi Rais anapokengeuka na kukanyaga Katiba ya Nchi, Waziri anapaswa kumshauri Bosi wake kwamba, hili unalotaka kulifanya kisheria si sawa, na amuambie kwa herufi kubwa ili mkubwa huyo ajue kweli ameboronga .
Sasa kwa vyovyote vile, yaliyotokea kwenye suala la CAG wa wakati ule, Profesa Assad kuondolewa ofisini kwa vile alikataa kutumikishwa kwenye uongo haliwezi kumuacha salama aliyekuwa Waziri wa Sheria (sikumbuki alikuwa nani), Huyu akikamatwa na kuburuzwa Mahakamani, Anaweza kutusaidia Mengi tunayojiuliza bila Majibu.
Ni vema akakamatwa haraka kabla hajakimbia nchi, Haiwezekani kuwaacha watu wanaoshiriki mambo ya kufedhehesha Taifa, ni lazima waadhibiwe ili iwe funzo kwa Wasiginaji wengine .
Mungu Ibariki Tanzania.