Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha akamatwa na Polisi

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Aliyekuwa waziri wa Mashauri ya Ndani ambae sasa ni mwanachama wa CHADEMA Mh Laurance Masha amekamatwa jioni ya leo na jeshi la polisi nchini.

Tukio la kukamatwa Masha limefuatia kukamatwa kwa wanachama 18 waliokuwa kwenye harakati za kawaida za uenezi wa chama chao katika kampeni ya kawaida ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu ambayo haizuiwi na sheria yoyote ile nchini.

Baada ya kukamatwa vijana hao na kufikishwa kituo cha Oysterbay, Mh Masha aliamua kwenda kufuatilia sababu za kukamatwa kwa wanaukombozi hao, ajabu alipofika tu nae akatiwa mbaroni.
 
Duuuh,Duuuh,Duuuh,Kikwete asijewasha moto wa mabua ukamshinda kuzima-asicheze na roho za watu kwenye nyakati hizi za ukombozi
 
Jeshi la polisi wana double standard sana..leo nimeona shein akiandama kwenda kuchukua fomu au Zanzibar sii sehemu ya Muungano?
 
Back
Top Bottom