Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola adaiwa kuwa chini ya ulinzi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
236
500
kangi.jpg

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola hivi sasa yupo chini ya ulinzi unaomfanya asiweze kusafiri sehemu yoyote bila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa na taarifa.

Lugola alitenguliwa wadhifa wake baada ya kuhusishwa na mkataba wa kifisadi wa zaidi ya shilingi trilioni 1 wa ununuzi wa vifaa vuya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Hata hivyo, siku chache zilizopita wakati Rais Magufuli akiwaapisha mawaziri na mabalozi aliowateua alikabidhi suala hilo kwa TAKUKURU kwa hatua zaidi na kuisihi mamlaka hiyo kutowaonea huruma waliohusika.

Imeelezwa kuwa maagizo hayo yamekuwa mwiba zaidi kwa Lugola ambaye inaelezwa kuwa kwa sasa anafuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama.

“Lugola yupo kwenye wakati mgumu sana, kwanza hajui hatma yake, yaani wale aliokuwa akiwapa amri hivi sasa ndiyo wanampa amri na kumchunguza”

“Yupo chini ya ulinzi kila anapokwenda na anachofanya ni lazima kijulikane, yale maisha ya kujimwambafai hayapo tena, sina hakika kama hata vikao vya bunge vilivyoanza jana atashiriki kikamilifu” chanzo kimoja kimelieleza Tanzania Daima.

Hata hivyo imeelezwa kuwa Kangi Lugola hakuonekana jana katika ufunguzi wa vikao vya bunge, jambo lililozua maswali kadhaa, mojawapo likiwa ni kama amekwenda Dodoma au yupo Dar kwa mahojiano na vyombo vya dola.

Siku chache zilizopita Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen. John Mbung’o alisema uchunguzi huo umeanza kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli.

Mbung’o alisema wataanza kupata nyaraka zinazohusu mkataba huo na kuhoji kila anayejua na aliyeshiriki katika mchakato wa mkataba huo, ikifuatiwa na kuwahoji watuhumiwa.

Chanzo: Tanzania Daima
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom