Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Upendo Peneza, wakamatwa na Polisi Geita na kuachiwa

UMauti ya kisiwa cha amani umeshafika. Petroli tayari ipo, kinachohitajika ni kiberiti tu ambacho nacho kipo njiani kinakuja.

Vijana wanalia njaa, baada ya kutatua shida zao mnakimbilia kumkamata Lowasa.

Hivi ni Rais wa namna hii ndio tulimuhitaji Tanzania? Swali bado pevu, tunamiaka 4 imebaki ya kutafakari.
 
Nimekuuliza sheria ya makosa ya jinai imetungwa lini?

Kingereza hujui, tumia kiswahili utaeleweka
Kwa kujitambua kwako hata hujui unauliza nini! Kutungwa kwa sheria na kuletwa kwa sheria mpya ni vitu viwili tofauti! Nakuuliza unaongelea penal code or!?
 
UMauti ya kisiwa cha amani umeshafika. Petroli tayari ipo, kinachohitajika ni kiberiti tu ambacho nacho kipo njiani kinakuja.

Vijana wanalia njaa, baada ya kutatua shida zao mnakimbilia kumkamata Lowasa.

Hivi ni Rais wa namna hii ndio tulimuhitaji Tanzania? Swali bado pevu, tunamiaka 4 imebaki ya kutafakari.
Ni wewe mwingine? Ndiye huyo huyo mliemhitaji tena kwa kura za wizi
 
Ninachojua ufisadi ni uhujumu uchumi kwahiyo unaweza kutungiwa sheria wakati wowote itakayoendana na shitaka lako,uhujumu uchumi hauna mda hata kama ulitenda miaka kumi iliyopita utahukumiwa tu.
Kuna watu walishitakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao kitu ambacho hata huyu Mzee angeweza kushitakiwa kupitia sheria hiyo.

Mbona yupo mtaana na mnamwangalia tu,acheni unafiki uliopitiliza viwango.
Mkumbushane na wale mliosema Mwizi wa kuku anauawa Wakati fisadi anazunguka na fomu mitaani watusaidie kumshika maana ndio wanazunguka naye siku hizi!
 
Hivi nchi hii kuna fisadi kama Magufuli fisadi la kiuchumi kisiasa na kijamii alishaitia nchi hii hasara kwa bilioni n anaendelea huyo wa kufungwa bila kesi aise
Umeshaishiwa hoja sasa, huna adabu kama pichu yenye kiraka!
 
Nyie mataahira kweli! Hivi waliokuwa wanaropoka kwamba ushahidi wanao mbona huwaulizi! Akina Mnyika, Lissu, Msigwa, Mbowe na wenzake, waulize ule ushahidi waliosema wanao umeyeyukia wapi! After all, wao ndio waliopiga kelele sana ndani ya bunge mpaka mzee mamvi akatimuliwa uwaziri mkuu, leo mmebadilika as if ccm ndio iliyomsema pale Mwembeyanga! Nyie machadema Akili zenu sawa na za ng'ombe .
na nyie mlikaa kimya au mlikuwa na upande mnaoutetea?
 
Ni wewe mwingine? Ndiye huyo huyo mliemhitaji tena kwa kura za wizi
Yessssss ni mimi, tena yule yule mwenye idiolojia pevu iliyokomaa.

Ninachosema ni kwamba, watanzania tunastahili heshima kubwa kuliko tunayoipata katika serikali hii. Na kuwa serikali hii haina ufanisi ni maneno tu ya kejeli na kujikosha.

Miezi Nane ya mwanzo: Tulisikia lawama tele kwa serikali iliyopita (Rais, makamu na waziri mkuu). Kila kukicha ilikuwa ni Kikwete, Kikwete, Chikwete, Chikwete. Si ulikuwa katika serikali hiyo hiyo na ulijua unaomba urais ili utatue matatizo. wananchu wanataka utatuzi wa matatizo yao, sio rais anayelalamika. Hilo likachuja, halikuwa habari tena. Hatulisikii tena.

Kwa mwaka mmoja: Natumbua majipu, natumbua majipu. Sasa ya utumbuaji wa majipu si habari tena.

Baada ya mwaka: Kejeli kwa watanzania na ukandamizaji wa wapinzani na vyombo vya habari. Weka ndani kila anayefungua kinywa chake. Hiki ni kipindi cha kutapatapa na ndio mwisho wa ufalme.

Sababu hizo ndizo zinazonitenga mimi na huyu Bwana mkubwa. Sioni kwanini nimuunge mkono?
 
Hongera sana kwa kuwa mkweli, endelea kuwaelimisha na wenzako ambao bado hawataki kuukubali ukweli!
 
Hongera

Wakati mnafanya makosa kuhusu huyu bwana hamkutuamini hata kwa hoja ya kuwa na uzoefu naye kazini wa miaka zaidi ya 20. Ni janga

Kosa siyo kosa hadi ukose unachotarajia

Naamini sasa mtakuwa na vigezo na viashiria thabiti vya kuteuana.

Kwa sisi wakulima lije jua, ukame, mvua kunakucha kama hakukuchi kwa kudra ya Mola.
 
Wote ukweli wanaufahamu sasa hivi. Tofauti iliyokuwepo kati yao nasi ni kwamba wao wanaogopa kusekwa rumande pindi wakimnyooshea kidole mkuu kwa ubabe wake. Wameamua kukaa kimya au kuzungumzia vyumbani tu. Kuna ambao wanaogopa hata kufungua JF eti wataripotiwa, maana polisi wanawahitaje wote wasiomsifia bwana mkubwa.

Yakikufika kama yale ya Bukoba na Geita hutoweza kuutambua ukweli. Na wote wamekaa kimya. Kwa ninavyowafahamu watani zangu wa Bukoba kukaa kimya basi kweli Simba aka Mungu kapita na anatawala nchi. Hawa huwa hawavumilii hata Nyerere aliwanyooshea mikono.
 
Hongera

Wakati mnafanya makosa kuhusu huyu bwana hamkutuamini hata kwa hoja ya kuwa na uzoefu naye kazini wa miaka zaidi ya 20. Ni janga

Kosa siyo kosa hadi ukose unachotarajia

Naamini sasa mtakuwa na vigezo na viashiria thabiti vya kuteuana.

Kwa sisi wakulima lije jua, ukame, mvua kunakucha kama hakukuchi kwa kudra ya Mola.

Uchaguzi wa Rais/mbunge ni sawa na mchezo wa bahati nasibu. Demokrasia ni nzuri lakini ina risk zake. Unajua kuwa Rais si sawa na kuwa waziri. Ni nafasi tofauti na zenye nguvu tofauti. Ni vigumu yule wa jana kuwa vile vile akiwa Rais.

Toka katika kujitangaza kuwa Mtu wa wanyonge uliyesoma bure mpaka kuwawekea ngumu wanafunzi, au kutowaskiliza wahanga wa Tetemeko ambao mpaka leo wanalala nje. Kutowasikiliza wahanga wa njaa.

Huyu amejieleza kuwa ni mtu wa Mungu nyakati zote za uchaguzi. Ni mtu gani wa Mungu asiyekuwa na huruma na wahanga? Hata hizo sekta za dini zinasaidia sasa huyu ni mtu wa Mungu yupi?

Narudia kumpata rais mzuri ni bahati na ni sawa na kamali au kucheza bahati nasibu. Tunachojua na cha uhakika ni kuwa katika bahati nasibu hii tumepoteza. Kinachompa furaha mcheza bahati nasibu ni mategemeo/hope kwa kesho, kwani mchezo huu tumepoteza na tunasubiri 2020 ili tucheze tena. Hiyo nakuaminisha bado ipo hata kwa wale wasiosema.

Haluta kontinuaaaaaa!
 
Back
Top Bottom