Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak Afariki Dunia

Status
Not open for further replies.

lutayega

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
1,288
552


Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak
Wednesday, June 20, 2012 1:08 AM
Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak ambaye serikali yake ilipinduliwa mwaka jana baada ya kuitawala Misri kwa miaka 30 amefariki dunia baada ya kukumbwa na shambulio la moyo akiwa jela.

Televisheni ya taifa ya Misri imetangaza kuwa aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak amefariki dunia kutokana na shambulio la moyo lililomkumba akiwa jela.

Hosni Mubarak ambaye alikuwa na umri wa miaka 84, alihukumiwa kifungo cha maisha mwanzoni mwa mwezi huu.

Televisheni ya taifa ya Misri imesema kuwa Mubarak alikumbwa na shambulio la moyo jumanne akiwa jela na alikimbizwa hospitali ya jeshi ambako madaktari wamethibitisha kuwa kwa kitabibu ni ameishafariki dunia.

Wakati ripoti nyingi zikitolewa kuwa Mubarak amefariki dunia, mawakili wake walikanusha habari za kufariki kwake wakisema kuwa Mubarak yuko kwenye chumba cha watu mahututi bado hajafariki dunia ingawa anapumua kwa kutumia mashine.

 
Duh!Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi....
 
kuna meseji very clear anaipata mtu flani hii hapa Tanzania...na alivo na ugonjwa wa kuanguka mbona anaweza kukata roho akiona mlango wa segerea
 
kuna meseji very clear anaipata mtu flani hii hapa Tanzania...na alivo na ugonjwa wa kuanguka mbona anaweza kukata roho akiona mlango wa segerea

Nimeipenda hii.....
Mkuu Kigogo, shikamoo.....habari za siku nyingi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom