Aliyekuwa Rais wa Misri Ahukumiwa Kwenda Jela Maisha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
6449162.jpg

Aliyekuwa Rais wa Misri Ahukumiwa Kwenda Jela Maisha




Aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak amehukumiwa kwenda jela maisha Saturday, June 02, 2012 8:39 PM
Aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak amepatikana na hatia ya mauaji ya raia wasio na hatia waliouliwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yake, amenusurika kuhukumiwa kunyongwa lakini atanyea debe maisha yake yote yaliyobaki.
Mitaa ya nchini Misri asubuhi hii imekumbwa na kelele za furaha kushangilia kuhukumiwa kifungo cha maisha aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak.


Mubarak mwenye umri wa miaka 84, amepatikana na hatia ya mauaji ya watu 850 waliouliwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali yake iliyokaa madarakani kwa miaka 30.


Maandamano ya kumng'oa Mubarak yalianza mwanzoni mwa mwaka jana na hatimaye utawala wa Mubarak uling'oka baada ya miaka 30 ambayo jaji alisema kuwa Misri ilikuwa kwenye giza nene la ukatili wa rais huyo.


Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani wa Misri, Habib al-Adly naye amehukumiwa kwenda jela maisha.

Aliyekuwa Rais wa Misri Ahukumiwa Kwenda Jela Maisha
 
Back
Top Bottom