Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono afariki usingizini

stan

Senior Member
Apr 23, 2010
149
180
160405081353_meghan_wren_512x288_bbc_nocredit.jpg

Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono​

Aliyekuwa nyota wa filamu za ngono Amber Rayne amefariki nyumbani kwake mjini Los Angeles ,maafisa wamethibitisha.

Marafiki na waliokuwa wafanyikazi wenzake walituma ujumbe katika mtandao wa Twitter wakimuenzi mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31 ambaye alifariki usingizi wikendi iliopita.

Amber alikuwa nyota wa filamu za ngono kwa muongo mmoja kabla ya kujiuzulu mwaka 2015.

Alikuwa miongoni ,mwa kundi moja la wanawake ambao walidai kwamba James Deen,ambaye pia ni nyota wa filamu za ngono alimshambulia.

Hatahivyo Deen amekana madai hayo.

Mkaguzi wa matibabu katika kaunti ya Los Angeles ameiambia Newsbeat kwamba hakuna sababu rasmi ya kifo chake iliothibitishwa.

Hatahivyo wamesema kuwa familia yake imearifiwa.Bi Rayne ,ambaye jina lake rasmi ni Meghan Wren,alitangaza kujiuzlu kutoka kazi hiyo mwaka uliopita.

Wafanyikazi wenza katika soko la filamu za ngono walituma ujumbe wa kushtushwa na kifo chake.

CHANZO: BBC
 
Kumbe wenzetu wana nyota (legend) wa filamu za ngono! Ingawa tunaonekana tuko nyuma kwenye hii tasnia ya filamu za ngono, ila kuchelewa kwetu ni mpango wa Mungu, sio fursa njema ya kuichangamkia. Acha watutangulie kwenye hili!
 
image.jpeg

Msanii nguli wa filamu za Ngono nchini Marekani Amber Rayne amefariki dunia.Rayne ambaye jina lake lingine ni Meghan Wren amefariki akiwa usingizini nyumbani kwake Los Angeles.Sababu za kifo chake bado hazijawekwa wazi,japo kuna taarifa kuwa alikuwa "overdosed" na madawa ya kulevya.

Nje ya maisha ya "Adult films" Amber alikuwa na maisha yake ya kijamii,rafiki wa watu wengi na kipenzi cha wanafamilia yake.Msimu huu wa pasaka Amber alijumuika na wanafamilia wenzake kusherekea sikukuu hiyo pamoja nao.Alisifika kwa kupenda sana kumiliki farasi na michezo yake.

Siku chache zilizopita Amber alinukuliwa na vyombo vya habari akimlalamikia muigizaji mwenzake wa kiume wa "Adults Film" kuwa alimbaka na kumpiga wakati wa kuigiza,kitu kilichomfanya kusema kuwa hatakuwa tayari tena kuigiza na mwanaume huyo.

Katika ulimwengu wa "Adults films" Ambar Rayne alijinyakulia tuzo kadhaa na kujizolea umaarufu sana wa kuwa miugizaji bora na mwenye kubeba uhalisia.Mara zote familia na ndugu zake walikuwa nyuma yake katika kazi yake hiyo aliyoipenda toka akiwa binti aliyemaliza kuvunja ungo.

Marafiki zake kadhaa ktk mtandao wa Twitter wametuma salamu za rambirambi wakimtakia pumziko la amani na kuomba malaika wampokee
 
Back
Top Bottom