Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza auwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,200
4,991
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndg CLEMENT MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kisesa jijini Mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM ndg Joyce Masunga (maarufu kama Maziwa Fresh) ni kweli kuwa tukio hili limetokea na tunaendelea kufuatilia kupata habari zaidi.

============

Mwananchi Dec 16, 2013:
Mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina ameuawa na wananchi wenye hasira baada ya kuzuka mgogoro wa ardhi baina yao. Mabina aliuawa katika Kata ya Kisesa, baada ya wananchi wenye hasira kumtuhumu kumuua kwa kumpiga risasi mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

Jina la mkazi aliyepigwa risasi halikupatikana na kwamba alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali kwa matibabu.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga alithibitisha kuuawa kwa Mabina, ambaye miezi ya karibuni alikuwa ni mwenyekiti wake.

Jinsi alivyouawa:

Masunga alisema taarifa zilizomfikia zinaeleza kuwa Mabina alijikuta anaingia kwenye mgogoro na wananchi hao saa 11:00 asubuhi.

Alisema mgogoro huo ulianza wakati kundi la watu waliotumwa na Mabina walipoanza kuweka alama za mipaka kwenye shamba linalodaiwa kumegwa kwenye eneo la wakazi hao.

Wakazi hao walipopata taarifa hizo, walijitokeza kuzuia kundi hilo lisitekeleze kazi hiyo.

Kundi hilo lilipopata upinzani huo, liliwasiliana na Mabina kumweleza kwamba wamezuiwa kufanya kazi aliyowaagiza.

Inadaiwa kuwa Mabina kusikia hivyo, aliharakisha kwenda eneo hilo ili kujaribu kusuluhisha mgogoro huo ili maelekezo yake yafanyike kama alivyopanga.

Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye eneo hilo, alisema wakati wanajibizana na wananchi hao, Mabina alimpiga risasi mmoja wa wakazi hao na kuanguka chini.

Walieleza kuwa tukio hilo liliwapandisha hasira wakazi hao na kusababisha wamshambulie kwa kumrushia mawe, vipande vya miti na silaha mbalimbali kwa kadri kila mmoja alivyoweza.

Hali hiyo, wanaielezea ilisababisha kuanguka chini na wakazidi kumshambulia hadi wakahakikisha amekufa huku vijana wake wa kazi wakiingia mitini.

Ofisa wa Polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa yeye si msemaji wa jeshi hilo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Taarifa hiyo ya polisi ilieleza kwamba, mgogoro huo ulizuka baada ya wananchi hao kumtuhumu Mabina kuwa ana mpango wa kuuza eneo lao la kijiji kwa mwekezaji.

“Ni mapema mno kuelezea tukio hili kwa undani hasa ikizingatiwa kuwa mimi siyo msemaji. Subiri msemaji wa jeshi atawapa taarifa kwa undani,” alisema ofisa huyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Christopher Fuime alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema wanaendelea kufanya uchunguzi.”

“Tulipata taarifa ya kuwepo kwa tukio hilo na kutuma vijana wetu kwenda kutuliza vurugu,” alisema Fuime. Alisema Mabina hakuwa na dhamira ya kuua, ila alijaribu kufyatua risasi hewani kwa lengo la kuwatuliza na ndipo ilipompata mmoja wao.

Kutoka kwa wanaomfahamu kwa karibu:

Clement Mabina:

- Alikuwa miongoni mwa watu ambao wamejijengea umaarufu mkubwa sana katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa hususani ndani ya ziwa Victoria!

- Ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakituhumiwa na ujambazi wa kutumia silaha hasa katika miaka ya 90!

- Ni miongoni mwa watu ambao wanadaiwa kuua wavuvi ndani ya Ziwa Victoria na kuwapora fedha na mali zao nyingine!

- Ni miongoni mwa watu wanaodaiwa kufanya mauaji ndani ya Ziwa yeye na wenzake kadhaa akiwemo DC na Diwani Mmoja!

- Kifo chake pengine ni malipo ya mauaji aliyokuwa akifanya dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.

- Ni mtu ambaye alikuwa anaogopwa hadi na maofisa wa Jeshi la Polisi, alitumia vibaya sana madaraka yake ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza!

- Alijaribu kupigana sana kwenye uchaguzi wa CCM mkoa mwaka huu, na ni miongoni mwa mambo yaliyomfanya achanganyikiwe!
=============
PICHA kwa wasiomfahamu:


RaisKikwete.jpg

Clement Mabina akiwa na Rais Kikwete (enzi za uhai wake) CCM Kirumba katika sherehe za kutimiza miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCMsherehe hizo za kutimiza miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM

=========

Mwili wa Marehemu

attachment.php
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndg CLEMENT MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kisesa jijini Mwanza.

Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana Mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani?

Mabina akaanza kutoa lugha chafu na
 
Inaendelea.........
Risasi zilipomuishia na kufanikiwa kumuua raia m1 kwa risasi ndipo wananchi wenye hasira kali wakamrudia kumpiga wakiwa na mapanga, mawe na kila dhana ya kijadi, jambo lililopelekea umauti kumkuta. Mauaji yametokea mchana huu majira ya saa 7.
 
Kama ni kweli, basi hii ni mbaya sana! Wangempeleka katika vyombo vya sheria jamani.
 
Mh!!! kwa kuwa ni TETESI ngoja nisubiri uhakika ndio niseme ninachotarajia kusema
 
what is the indication? ukihusisha na utoaji na usimamiaji wa haki
 
Inakuwaje kiongozi wa umma anaamua kutumia mabavu kuhalalisha mambo; na kivipi wananchi wakachukua uamuzi huo. Utawala wa sheria ulikuwa wapi? Any way hata Mvomero wafugaji na wakulima wanatoana roho bila serikali kuchukua initiatives. RIP Mabina
 
Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza MABINA ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa mawe huko maeneo ya Kiseke jijini mwanza. Chanzo cha kuuwawa ni kwamba mabina aliwanyang'anya ardhi wananchi hao na kesi ikawa mahakamani na leo mchana mabina bila kibali cha mahakama alikuwa anapanda miti na kujenga msingi wa nyumba ndipo wanachi wakaenda kumhoji iweje anapanda miti na kuweka msingi kwenye viwanja hivyo ilhali kesi ipo mahakamani.? Mabina akaanza kutoa lugha chafu na kurusha risasi hewani.
Mhh...kumbe pana chezea Sukumaland veve. Tusubiri propaganda kutoka Lumumba maana sasa wako kwenye foleni kupokea buku 7 za kula mchana pale Lumumba.
 
Back
Top Bottom