Aliyekuwa mwenyekiti UVCCM Kilimanjaro kisha akahamia CHADEMA arudi tena CCM leo

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Moshi.

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, kimeanza kuvuna wanachama wake waliosombwa na mafuriko katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Madiwani, wabunge na Rais mwaka 2015, baada ya Frederick Mushi kurejesha kadi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kujiunga na chama hicho.

Frederick Mushi ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi kwa zaidi ya miaka Tisa kabla ya kuondoka katika chama hicho Agust 14 mwaka 2015 na kujiunga na Chadema,ametangaza kujiunga na CCM kwa mara nyingine jana katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kilimanjaro, kwa madai kuwa, kiu na matarajio aliyoyategemea kwenye upinzani hajayapata hivyo anaamua kurudi nyumbani kuunga mkono jitihada Rais John Magufuli za kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za nchi.

Akizungumza mara baada ya kutangaza kujiondoa Chadema na kujiunga na CCM, Mushi alisema mwaka 2015 alikubali kuachia nyadhifa zake alizokuwa nazo CCM kwa matumaini kuwa anakwenda kuendeleza mapambano ya kupinga ufisadi na Rushwa kupitia upinzani jambo ambalo halikufanikiwa kutokana na mfumo uliopo katika vyama hivyo.

“Kabla sijaondoka CCM nilikuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM), naomba nikiri leo kwamba nilikosea sana kuondoka na kujiunga na Chadema, kwani nilikuwa shimoni na sistahili kuendelea kukaa katika giza la shimo sasa narudi nyumbani kwangu CCM”alisema Mushi.

Mushi alieleza kuwa ameamua kurudi katika chama cha mapinduzi baada ya kuona jitihada kumbwa na mapambano ya kupiga vita rushwa, ufisadi pamoja na kutetea Rasilimali za nchi zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli.

“Kazi inayofanywa na Rais Magufuli ni kubwa sana na leo siwezi kuwa sehemu ya watu wanaomtukana Rais Magufuli, kwa kweli naona aibu, na ili kumuunga mkono kwa dhati nimeamua kurudi CCM ambako nakiri kwamba ndiko nyumbani kwangu”

Mushi alitumia pia nafasi hiyo, kuwataka vijana nchini kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais magufuli katika kutetea na kulinda rasilimali za taifa, hatua ambayo itasaidia kuongeza nguvu katika mapambano hayo.

“Nitoe wito kwa vijana kushikamana na kumuunga mkono Rais wetu Magufuli,kwani ametuamini na kutoa nafasi mbalimbali za uongozi kwa vijana, hivyo tunapaswa kutambua thamani yetu na tusimuangushe bali tutembee kifua mbele katika kumlinda na kumtetea pale anaposimama kutetea rasilimali za nchi yetu”alisema.

Akizungumza katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabihya, alisema chama hicho hakina mtaji wa kuwanunua watu ili wajiunge nacho, na kwamba wale wanaojiunga na CCM wanajiunga kwa matakwa yao bila ushawishi wowote.

“Leo mpinzani akiingia CCM wanadai kuwa amenunuliwa, lakini Mtu wa CCM akiingia upinzani wanadai kuwa amejitambua, hii sio sahihi kwani chama cha mapinduzi hatuna fedha wala mtaji wa kuwanunua watu na ni vyema watu wakaelewa kuwa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa ni matakwa yake mwenyewe”alisema.

Mabihya alitumia pia nafasi hiyo kumpongeza Mushi kwa kujitambua na kuamua kurudi katika chama cha mapinduzi ambako ndipo alikuwa awali na kuona matunda yake.

Mwisho.
 
a3637f91d5cb85cb35274a94c10ac4cc.jpg
 
Haya semeni na huyo siyo Mchaga? Kwa maana anaitwa Mushi au kagushi jina? Ukiona mpaka Wachaga wanaanza kuikimbia chadema ujue Meli inazama !
 
CHADEMA walilifuga li swala la porini wakafikiri ni mbuzi mee ona limerudi porini na kuona bora likaliwe na chui, simba, mamba fisi au mbwa mwitu. Ukizoea kukaa porini hata upewe nini utarudi tu.

Sawa na uchawi. Ukizoea kula nyama za watu hutaacha, utaendelea tu. Ukifika sehemu ambako hawali utaona kama umepotea
 
Moshi.

CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Kilimanjaro, kimeanza kuvuna wanachama wake waliosombwa na mafuriko katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Madiwani, wabunge na Rais mwaka 2015, baada ya Frederick Mushi kurejesha kadi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kujiunga na chama hicho.

Frederick Mushi ambaye alikuwa mwanachama wa chama cha Mapinduzi kwa zaidi ya miaka Tisa kabla ya kuondoka katika chama hicho Agust 14 mwaka 2015 na kujiunga na Chadema,ametangaza kujiunga na CCM kwa mara nyingine jana katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kilimanjaro, kwa madai kuwa, kiu na matarajio aliyoyategemea kwenye upinzani hajayapata hivyo anaamua kurudi nyumbani kuunga mkono jitihada Rais John Magufuli za kupambana na ufisadi na kutetea rasilimali za nchi.

Akizungumza mara baada ya kutangaza kujiondoa Chadema na kujiunga na CCM, Mushi alisema mwaka 2015 alikubali kuachia nyadhifa zake alizokuwa nazo CCM kwa matumaini kuwa anakwenda kuendeleza mapambano ya kupinga ufisadi na Rushwa kupitia upinzani jambo ambalo halikufanikiwa kutokana na mfumo uliopo katika vyama hivyo.

“Kabla sijaondoka CCM nilikuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana(UVCCM), naomba nikiri leo kwamba nilikosea sana kuondoka na kujiunga na Chadema, kwani nilikuwa shimoni na sistahili kuendelea kukaa katika giza la shimo sasa narudi nyumbani kwangu CCM”alisema Mushi.

Mushi alieleza kuwa ameamua kurudi katika chama cha mapinduzi baada ya kuona jitihada kumbwa na mapambano ya kupiga vita rushwa, ufisadi pamoja na kutetea Rasilimali za nchi zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli.

“Kazi inayofanywa na Rais Magufuli ni kubwa sana na leo siwezi kuwa sehemu ya watu wanaomtukana Rais Magufuli, kwa kweli naona aibu, na ili kumuunga mkono kwa dhati nimeamua kurudi CCM ambako nakiri kwamba ndiko nyumbani kwangu”

Mushi alitumia pia nafasi hiyo, kuwataka vijana nchini kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais magufuli katika kutetea na kulinda rasilimali za taifa, hatua ambayo itasaidia kuongeza nguvu katika mapambano hayo.

“Nitoe wito kwa vijana kushikamana na kumuunga mkono Rais wetu Magufuli,kwani ametuamini na kutoa nafasi mbalimbali za uongozi kwa vijana, hivyo tunapaswa kutambua thamani yetu na tusimuangushe bali tutembee kifua mbele katika kumlinda na kumtetea pale anaposimama kutetea rasilimali za nchi yetu”alisema.

Akizungumza katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Jonathan Mabihya, alisema chama hicho hakina mtaji wa kuwanunua watu ili wajiunge nacho, na kwamba wale wanaojiunga na CCM wanajiunga kwa matakwa yao bila ushawishi wowote.

“Leo mpinzani akiingia CCM wanadai kuwa amenunuliwa, lakini Mtu wa CCM akiingia upinzani wanadai kuwa amejitambua, hii sio sahihi kwani chama cha mapinduzi hatuna fedha wala mtaji wa kuwanunua watu na ni vyema watu wakaelewa kuwa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa ni matakwa yake mwenyewe”alisema.

Mabihya alitumia pia nafasi hiyo kumpongeza Mushi kwa kujitambua na kuamua kurudi katika chama cha mapinduzi ambako ndipo alikuwa awali na kuona matunda yake.

Mwisho.

Walishazoea vya kunyonga ccm hivyo vya kuchinja upinzani hawaviwezi!!! Hakuenda chadema kwa kuielewa na kuikubali bali alimfuata Lowassa! Lowassa wa chadema sio yule Lowassa wa ccm na maburungutu yake!!! Haishangazi hata kidogo, tena alichelewa sana!
 
Huyo arudi tu kwa sababu hakuwa hata na faida zaidi ya kutupiga mizinga ya bia mtaani!!!
 
Back
Top Bottom