Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Z’bar aibua mazito ya Katiba Mpya

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Z’bar aibua mazito ya Katiba Mpya

mazito+katiba_1.jpg

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Background (kwa kifupi)
Mh Othman alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uandishi wa Bunge la Katiba (a.k.a Bunge la Sitta (rip)). Tarehe 1 Oktoba 2014 aliibua mshangao mkubwa baada ya kupiga kura ya kukataa baadhi ya vipengele vya Rasimu ya Katiba ambayo tayari UKAWA walikuwa wameishaisusia baada ya kuchakachuliwa kwa Rasimu ya Katiba ya Wananchi (a.k.a Rasimu ya Warioba).
Baada ya uamuzi wake wa kujitoa kwenye Bunge la Katiba, Mh Othman anasema Rais Shein alimuita na kumtaka ajiuzulu, lakini akakataa akimweleza kuwa kwa sababu yeye (Rais) ndiye aliyemteua, na yeye (Othman) anaona hajatenda kosa lolote, basi Rais atengue uteuzi ule mwenyewe kama ataona inafaa. The rest is history.

Mh Othman afafanua kwa nini alipiga kura ya kukataa vipengele kadhaa kwenye Rasimu ya Katiba:

- Zanzibar haikwenda kwenye Bunge la Katiba ikiwa na msimamo wake na kwamba Dk Shein alishindwa kutetea visiwa hivyo.

- wajumbe kutoka Zanzibar hawakuwahi kukutana na kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kutetea masilahi yao, licha ya Rais Shein kushauriwa kuwakutanisha. Hivyo kila mtu alikwenda kivyake kwenye Bunge la Katiba. Walikwenda na misimamo yao ya vyama. "kwa bahati mbaya mimi sifungwi na misimamo ya vyama hivyo viwili. Watu waliomba si mara moja si mara mbili kwa Rais kwamba tukae. Makamu wa Kwanza (wakati huo Maalim Seif Sharif Hamad) alikwenda kumuomba, mawaziri walikwenda kumuomba kwamba tukae tujadili masilahi ya Zanzibar, lakini hatukukutana,” alisema.

- kilichomkera zaidi Mh Othman ni kuwekwa kwenye Kamati ya Uandishi wa Katiba ambayo alisema ilipewa maelekezo ya nini cha kuandika. “Nakumbuka kanuni ya 35 inasema kazi ya Kamati ya Uandishi ni kukusanya yale yaliyotoka kwenye Kamati za Bunge. Sasa ugomvi wangu ulikuwa ni mambo yaliyojadiliwa kwenye hizo kamati, yalitokana na waraka wa CCM uliotoa maelekezo ya mambo yaliyotakiwa kuandaliwa,” alisema

- anaendelea... “kwanza nilikuwa sikubaliani na mambo mengi yaliyojadiliwa kwenye hizo kamati. Pili, kwenye kuandaa hiyo ripoti ya chama, mimi sikushiriki ingawa kwa upande mwingine, Mwanasheria Mkuu wa wakati huo na wanasheria wengine walishirikishwa, akiwemo Jaji Fredrick Werema”

- sababu nyingine ni wajumbe walioteuliwa kuandika Katiba Inayopendekezwa kuandaliwa kila kitu na mchakato kukosa misingi ya uandishi. anasema “kwa hiyo sikutaka jina langu liwemo kwenye rasimu ambayo sikuiandaa, ndiyo maana nikajiondoa. Uzuri ni kwamba sikuteuliwa kwenye ile kamati kama Mwanasheria Mkuu (wa Zanzibar), bali niliteuliwa kama Othman, mjumbe wa Bunge la Katiba,” alisema.

- Mh Othman anaongezea kusema kabla ya kujitoa Kamati ya Uandishi, wajumbe wenzake kutoka Zanzibar, wakiwamo mawaziri wa Zanzibar walikutana na kuweka msimamo wa mambo manane kati ya 17 waliyotaka yaingizwe kwenye Katiba hiyo, lakini baadaye yalikataliwa.
- Baadhi ya mambo hayo muhimu ni:
(a) uwezo wa Rais wa Muungano kugawa mipaka ya Zanzibar, akisema walitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1982.
(b) Katiba ya Jamhuri ya Muungano isiguse mambo yasiyo ya Muungano ambayo yatakuwa chini ya Katiba ya Zanzibar.
(c) suala la ardhi ambalo awali lilikuwa chini ya Muungano, akisema lilipaswa kuwa chini ya Zanzibar
(d) jinsi ya kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kutumia wingi wa kura, jambo ambalo alisema haliwezekani, akipendekeza Rais apate japo asilimia 20 ya kura za Wazanzibari ndipo ahesabike kuwa mshindi. Mh Othman ametolea mfano Kenya na Marekani ambako minority (geographically) wanapewa appropriate leverage jinsi ya kumchagua mkuu wa nchi
(e) mambo mengine aliyataja kuwa kuwa ni mfumo wa kodi, suala la kupiga kura ndani ya Bunge na kubadilisha mfumo wa Serikali. Alitaja pia kero ya wabunge wa Zanzibar kutokuwa na nguvu ya uamuzi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, akisema ndiyo kubwa aliyoipigania
Mh Othman anaonyesha mshangao “sisi tunajiuliza, wabunge wa Zanzibar kama hawana sauti kwenye mambo ya Muungano, wanakwenda kufanya nini pale? Kuna haja ya kuwa na wabunge wa Zanzibar kama hawana sauti?"
Mh Othman anamalizia kwa kusema waliyajadili mambo hayo wakiwa na mawaziri wa Zanzibar, lakini baadaye wakabadilika.
Anaongeza hapa “Baadaye wakasema jamani tumeshakaa hapa tumekula pesa ya watu, tupitisheni tu kwa sababu hayataingia kwenye Rasimu ya Katiba. Waliponifuata nilikataa kwa sababu kumbukumbu inayobaki hapo ni Katiba Inayopendekezwa.”

Chanzo: MWANANCHI 14 Novemba 2016

my take:
kuna umuhimu wa serekali hii ya awamu ya 5 (with or without mchakato wa katiba) wa kuunda tume maalumu ya mapatano kule Zanzibar halafu ku-harmonize na mahitaji ya muungano.

sijui, labda ni mimi peke yangu.....lakini mbona mimi naona hili suala ni rahisi sana kupata suluhisho kwa kutumia diplomacy bila ya mihemko, ubabe na kutunishiana misuli kama ilivyo sasa?
 
Alafu hivi nani anaurudisha huu mjadala wa katiba mpya kwa kasi hivi ebu tujibuni kuhusu pesa za wahanga Kagera hili la katiba lije badae msitutoe katika hoja ya msingi ya hivi sasa hii katiba Mh alisema siyo ahadi yake sasa mnataka nini tunataka pesa za wahanga zirudi alafu Mh asije na majibu yake ya dharau dharau as is sisi watoto wadogo
 
Dunia haijawah mahala salama pa kuishi mimi naamin hvyo

Na hii inatokana na hawa wanasiasa wanaohisi wao waliutengeneza ulimwengu

Aisee !!
 
Alafu hivi nani anaurudisha huu mjadala wa katiba mpya kwa kasi hivi ebu tujibuni kuhusu pesa za wahanga Kagera hili la katiba lije badae msitutoe katika hoja ya msingi ya hivi sasa hii katiba Mh alisema siyo ahadi yake sasa mnataka nini tunataka pesa za wahanga zirudi alafu Mh asije na majibu yake ya dharau dharau as is sisi watoto wadogo
Hongera gazeti la Mwana halisi kwa kuurudisha huu mjadala kwa wananchi. Huwezi kuteka wananchi kwa misingi ya kuibeba CCM, Nilimdharau shein kama alivyokwisha dharaulika na wanzanzibari wengine, lakini hii imeonyesha jinsi gani wana CCM wa zanzibar walivyo mabwelele except for huyu bwana. CUF walionya kuwa ni vema waenda kama nchi moja, na sisi wabara tulio na akili, tofauti na mambumbumbu ya chama tawala tulifurahia sana na kutegemea sana kura ya zanzibar, very stupid people of my country. Leo hela za michango ya waathirika eti serikali imeamua zijengewe miundo mbinu, na bado watanzania tumekaa majumbani kwetu badala ya kukutana barabararan, we are worse than animals ambao leo ukitaka kumchukua kifaranga, kuku wote watasimama upande wake, sisi hatuna mwenyewe
 
Apite hivi, tupo bize na kusaka maendeleo
Hongera mkuu.wengine tumekomaa maofisin hamna hata wateja.mwezi Wa sita huu hata kodi la pango litatushinda.hela hamna.tukiongea wakasema tufanye kazi.bottom line HAli MBaya
 
Hayo mambo nane muhimu kwake ndio wananchi walivyomweleza au mawazo yao; naona kesha sahau alitumwa kufanya kazi ya kukusanya mawazo ya wa Tanzania na kufanya summary ya mawazo ya watanzania sio kuongeza wazimu uliokuwa kichwani mwake kama sehemu ya katiba itakayowaongoza takribani watu millioni 50.
 
Alafu hivi nani anaurudisha huu mjadala wa katiba mpya kwa kasi hivi ebu tujibuni kuhusu pesa za wahanga Kagera hili la katiba lije badae msitutoe katika hoja ya msingi ya hivi sasa hii katiba Mh alisema siyo ahadi yake sasa mnataka nini tunataka pesa za wahanga zirudi alafu Mh asije na majibu yake ya dharau dharau as is sisi watoto wadogo
kwanza ukawa warudishe hela ya katiba waliyokula kisha kuhujumu mchakato baada ya kususia vikao.
 
Hongera gazeti la Mwana halisi kwa kuurudisha huu mjadala kwa wananchi. Huwezi kuteka wananchi kwa misingi ya kuibeba CCM, Nilimdharau shein kama alivyokwisha dharaulika na wanzanzibari wengine, lakini hii imeonyesha jinsi gani wana CCM wa zanzibar walivyo mabwelele except for huyu bwana. CUF walionya kuwa ni vema waenda kama nchi moja, na sisi wabara tulio na akili, tofauti na mambumbumbu ya chama tawala tulifurahia sana na kutegemea sana kura ya zanzibar, very stupid people of my country. Leo hela za michango ya waathirika eti serikali imeamua zijengewe miundo mbinu, na bado watanzania tumekaa majumbani kwetu badala ya kukutana barabararan, we are worse than animals ambao leo ukitaka kumchukua kifaranga, kuku wote watasimama upande wake, sisi hatuna mwenyewe

Kwani hy hela ya wahanga ni ya kujitajirisha ama kuwarudisha ktk hali yao ya zamani!! Km wameshafanya hvy kwa nn isitumike kwa kazi engine!! Wa Tz jamani!!
 
Hayo mambo nane muhimu kwake ndio wananchi walivyomweleza au mawazo yao; naona kesha sahau alitumwa kufanya kazi ya kukusanya mawazo ya wa Tanzania na kufanya summary ya mawazo ya watanzania sio kuongeza wazimu uliokuwa kichwani mwake kama sehemu ya katiba itakayowaongoza takribani watu millioni 50.

Kati ya huyu aliekuwa mwanasheria wa Zanzibar mh Othman Masoud na wewe nani mwenye wazimu!!!!!! Nadhani wewe ndio hasa maana hata haujui nini unachokiongea!!!! Niwapi na nani aliemtuma Mh. Othman Masoud kukusanya maoni ya wananchi!!!!!!!!???

Pamoja na kichaa chako ulichonacho basi mtofautishe kabisa Mh. Othman Masoud na wasomi wenu wa kidanganyika!!!!! Wafoji vyeti wengi wa kidanganyika akili zao hazina tofauti na akili za VUNJAJUNGU DUME, akili za wafoji vyeti wa kidanganyika ziko TUMBONI sawa na vunjajungu DUME.

Ninani katika hao Wafoji vyeti wa kidanganyika angeweza kupingana na mwajiri wake tena akiwa katika nafasi ya juu ya uongozi na kuwa tayari kuikosa hiyo nafasi ilimradi anasimamia anachokiamini!!!!!!???? VUNJAJUNGU DUME yuko tayari kukatwa kichwa na JIKE ilimradi astarehe nae. AKILI ZAKE ZIKO TUMBONI.
 
Waipe uhuru Zanzibar ya watu au kama hawataki tuifanye koloni la tanganyika haswa na tuinyonye kwelikweli mpaka wawe kitu kimoja kujipigania wenyewe.
 
Kati ya huyu aliekuwa mwanasheria wa Zanzibar mh Othman Masoud na wewe nani mwenye wazimu!!!!!! Nadhani wewe ndio hasa maana hata haujui nini unachokiongea!!!! Niwapi na nani aliemtuma Mh. Othman Masoud kukusanya maoni ya wananchi!!!!!!!!???

Pamoja na kichaa chako ulichonacho basi mtofautishe kabisa Mh. Othman Masoud na wasomi wenu wa kidanganyika!!!!! Wafoji vyeti wengi wa kidanganyika akili zao hazina tofauti na akili za VUNJAJUNGU DUME, akili za wafoji vyeti wa kidanganyika ziko TUMBONI sawa na vunjajungu DUME.

Ninani katika hao Wafoji vyeti wa kidanganyika angeweza kupingana na mwajiri wake tena akiwa katika nafasi ya juu ya uongozi na kuwa tayari kuikosa hiyo nafasi ilimradi anasimamia anachokiamini!!!!!!???? VUNJAJUNGU DUME yuko tayari kukatwa kichwa na JIKE ilimradi astarehe nae. AKILI ZAKE ZIKO TUMBONI.
We sasa unataka kubisha hakuwa kwenye tume ya katiba ama?

Halafu unadhani kazi ya tume ilikuwa nini kuja na mawazo yao kama huyu bwana anavyotaka au kuwakilisha maoni ya wananchi.

Mfa maji tu huyo kilichobaki ni kutapa tu, halafu mtu analalamika vitu ambavyo walau basi angesema maoni yalitoa twasira hiyo. Kwakuwa anajoropokea tu na kutoa maelezo tofauti ya kazi yao kama tume kwa mujibu wa sheria husika; huu kama sio wazimu tuuite nini.
 
Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu Z’bar aibua mazito ya Katiba Mpya

mazito+katiba_1.jpg

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Background (kwa kifupi)
Mh Othman alikuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Uandishi wa Bunge la Katiba (a.k.a Bunge la Sitta (rip)). Tarehe 1 Oktoba 2014 aliibua mshangao mkubwa baada ya kupiga kura ya kukataa baadhi ya vipengele vya Rasimu ya Katiba ambayo tayari UKAWA walikuwa wameishaisusia baada ya kuchakachuliwa kwa Rasimu ya Katiba ya Wananchi (a.k.a Rasimu ya Warioba).
Baada ya uamuzi wake wa kujitoa kwenye Bunge la Katiba, Mh Othman anasema Rais Shein alimuita na kumtaka ajiuzulu, lakini akakataa akimweleza kuwa kwa sababu yeye (Rais) ndiye aliyemteua, na yeye (Othman) anaona hajatenda kosa lolote, basi Rais atengue uteuzi ule mwenyewe kama ataona inafaa. The rest is history.

Mh Othman afafanua kwa nini alipiga kura ya kukataa vipengele kadhaa kwenye Rasimu ya Katiba:

- Zanzibar haikwenda kwenye Bunge la Katiba ikiwa na msimamo wake na kwamba Dk Shein alishindwa kutetea visiwa hivyo.

- wajumbe kutoka Zanzibar hawakuwahi kukutana na kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kutetea masilahi yao, licha ya Rais Shein kushauriwa kuwakutanisha. Hivyo kila mtu alikwenda kivyake kwenye Bunge la Katiba. Walikwenda na misimamo yao ya vyama. "kwa bahati mbaya mimi sifungwi na misimamo ya vyama hivyo viwili. Watu waliomba si mara moja si mara mbili kwa Rais kwamba tukae. Makamu wa Kwanza (wakati huo Maalim Seif Sharif Hamad) alikwenda kumuomba, mawaziri walikwenda kumuomba kwamba tukae tujadili masilahi ya Zanzibar, lakini hatukukutana,” alisema.

- kilichomkera zaidi Mh Othman ni kuwekwa kwenye Kamati ya Uandishi wa Katiba ambayo alisema ilipewa maelekezo ya nini cha kuandika. “Nakumbuka kanuni ya 35 inasema kazi ya Kamati ya Uandishi ni kukusanya yale yaliyotoka kwenye Kamati za Bunge. Sasa ugomvi wangu ulikuwa ni mambo yaliyojadiliwa kwenye hizo kamati, yalitokana na waraka wa CCM uliotoa maelekezo ya mambo yaliyotakiwa kuandaliwa,” alisema

- anaendelea... “kwanza nilikuwa sikubaliani na mambo mengi yaliyojadiliwa kwenye hizo kamati. Pili, kwenye kuandaa hiyo ripoti ya chama, mimi sikushiriki ingawa kwa upande mwingine, Mwanasheria Mkuu wa wakati huo na wanasheria wengine walishirikishwa, akiwemo Jaji Fredrick Werema”

- sababu nyingine ni wajumbe walioteuliwa kuandika Katiba Inayopendekezwa kuandaliwa kila kitu na mchakato kukosa misingi ya uandishi. anasema “kwa hiyo sikutaka jina langu liwemo kwenye rasimu ambayo sikuiandaa, ndiyo maana nikajiondoa. Uzuri ni kwamba sikuteuliwa kwenye ile kamati kama Mwanasheria Mkuu (wa Zanzibar), bali niliteuliwa kama Othman, mjumbe wa Bunge la Katiba,” alisema.

- Mh Othman anaongezea kusema kabla ya kujitoa Kamati ya Uandishi, wajumbe wenzake kutoka Zanzibar, wakiwamo mawaziri wa Zanzibar walikutana na kuweka msimamo wa mambo manane kati ya 17 waliyotaka yaingizwe kwenye Katiba hiyo, lakini baadaye yalikataliwa.
- Baadhi ya mambo hayo muhimu ni:
(a) uwezo wa Rais wa Muungano kugawa mipaka ya Zanzibar, akisema walitaka Rais wa Zanzibar awe na mamlaka hayo kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1982.
(b) Katiba ya Jamhuri ya Muungano isiguse mambo yasiyo ya Muungano ambayo yatakuwa chini ya Katiba ya Zanzibar.
(c) suala la ardhi ambalo awali lilikuwa chini ya Muungano, akisema lilipaswa kuwa chini ya Zanzibar
(d) jinsi ya kumpata Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa kutumia wingi wa kura, jambo ambalo alisema haliwezekani, akipendekeza Rais apate japo asilimia 20 ya kura za Wazanzibari ndipo ahesabike kuwa mshindi. Mh Othman ametolea mfano Kenya na Marekani ambako minority (geographically) wanapewa appropriate leverage jinsi ya kumchagua mkuu wa nchi
(e) mambo mengine aliyataja kuwa kuwa ni mfumo wa kodi, suala la kupiga kura ndani ya Bunge na kubadilisha mfumo wa Serikali. Alitaja pia kero ya wabunge wa Zanzibar kutokuwa na nguvu ya uamuzi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano, akisema ndiyo kubwa aliyoipigania
Mh Othman anaonyesha mshangao “sisi tunajiuliza, wabunge wa Zanzibar kama hawana sauti kwenye mambo ya Muungano, wanakwenda kufanya nini pale? Kuna haja ya kuwa na wabunge wa Zanzibar kama hawana sauti?"
Mh Othman anamalizia kwa kusema waliyajadili mambo hayo wakiwa na mawaziri wa Zanzibar, lakini baadaye wakabadilika.
Anaongeza hapa “Baadaye wakasema jamani tumeshakaa hapa tumekula pesa ya watu, tupitisheni tu kwa sababu hayataingia kwenye Rasimu ya Katiba. Waliponifuata nilikataa kwa sababu kumbukumbu inayobaki hapo ni Katiba Inayopendekezwa.”

Chanzo: MWANANCHI 14 Novemba 2016

my take:
kuna umuhimu wa serekali hii ya awamu ya 5 (with or without mchakato wa katiba) wa kuunda tume maalumu ya mapatano kule Zanzibar halafu ku-harmonize na mahitaji ya muungano.

sijui, labda ni mimi peke yangu.....lakini mbona mimi naona hili suala ni rahisi sana kupata suluhisho kwa kutumia diplomacy bila ya mihemko, ubabe na kutunishiana misuli kama ilivyo sasa?
Hofu yangu ni kuwa je, siri hiyo aliyoitoboa na hali ya kisiasa ya Zbar ilivyo sasa hivi kimalipizi, atasalimika?
 
We sasa unataka kubisha hakuwa kwenye tume ya katiba ama?

Halafu unadhani kazi ya tume ilikuwa nini kuja na mawazo yao kama huyu bwana anavyotaka au kuwakilisha maoni ya wananchi.

Mfa maji tu huyo kilichobaki ni kutapa tu, halafu mtu analalamika vitu ambavyo walau basi angesema maoni yalitoa twasira hiyo. Kwakuwa anajoropokea tu na kutoa maelezo tofauti ya kazi yao kama tume kwa mujibu wa sheria husika; huu kama sio wazimu tuuite nini.

Sasa kama alikuwa katika tume ya warioba jee katika hivyo vifungu alivyovikataa na alivyovipendekeza vilitoka katika rasimu ya Katiba au au rasimu ya ccm ambayo iliwasilishwa baada ya kuikataa ya warioba!!!!????

Kama kweli wewe sio miongoni mwa VUNJAJUNGU DUME unaweza ukaniambia bunge la katiba jee lilijadili rasimu ya warioba au ya ccm!? Kwa kuwa anajitambua ndio maana akakataa kuwa miongoni mwa waandishi wa waliondika uvundo unaosubiri kupigiwa kura ya maoni.

Tena alivyokuwa jasiri aliukataa mchana kweupe bila ya kujali nini kitakachojiri juu ya hatma ya nafasi alivyokiwa nayo. NARUDIA TENA HAKUNA MFOJI VYETI WA KIDANGANYIKA MWENYE UJASIRI KAMA ULE!!!!! Unajua kwanini!!!?? Akili zao ziko TUMBONI.
 
Back
Top Bottom