Aliyekuwa mstari wa mbele kupinga ununuzi wa rada ya Tanzania,kupatiwa Tuzo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Waziri wa zamani wa Uingereza wa ushirikiano wa kimaendeleo, Clare Short, aliyekuwa mstari wa mbele kupinga ununuzi wa rada ya Tanzania kiasi cha kutofautiana na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa inazidi kung’ara nchini na Raia Mwema imebaini kuwapo kwa maandalizi ya kumpatia tuzo mahsusi kama sehemu ya kutambua juhudi zake hizo ambazo zimebainika kuwa na maslahi kwa Watanzania.


Kama tuzo hiyo itatolewa, basi, itakuwa ya kwanza kutolewa kwa Waziri kutoka Ulaya. Claire Short alifikia hatua ya kutishia kujiuzulu wadhifa wake katika Bunge la nchini kwake ili kuonyesha msimamo wa kutetea wananchi wa nchi masikini kama Tanzania.
Mama huyo ndiye Waziri aliyeanzisha mzozo wa kupinga ununuzi wa rada hiyo katika Bunge la Uingereza, nchi ambayo ni mfadhili wa maendeleo ya Tanzania, na hasa bajeti ya Taifa ambayo zaidi ya asilimia 30 hutegemea wafadhili.
Hoja zilizokuwa zikitumiwa na Short katika kupinga ununuzi huo ni pamoja na rada hiyo kuuzwa bei ghali tofauti na thamani halisi lakini pia ubora wake kuwa ulikuwa ni wa kutia shaka. Rada hiyo ilinunuliwa kutoka Kampuni ya utengenezaji na uuzaji vifaa vya kijeshi ya Serikali ya Uingereza ya BAE Systems.
 
swali je watanzania lini tutagundua udhaifu wetu au mpaka mtu mwingine atugundulieeee
 
Majambazi walioshiriki katika ununuzi huo bado ni viongozi waheshimiwa wa Tazania, wako bungeni wanawawakilisha waliowaibia, loh!! Naona wakati Clare Short anapewa tunzo, viongozi wa kitanzania walioshinikiza ununuzi wa rada hiyo waalikwe na wapewe cheti cha kuwalaani kwa kuhujumu watanzania wenzao.
 
Back
Top Bottom