Aliyekuwa Mpenzi wangu anataka Kurudi kwangu Nimkubalie?

Mungu alivyokua habagui hata ukimuomba akusaidie katika uzinzi anakupa unachotaka.

Sasa muombe akunyooshee mipango.
 
Mungu alivyokua habagui hata ukimuomba akusaidie katika uzinzi anakupa unachotaka.

Sasa muombe akunyooshee mipango.
Ahahaha.. Zama zishapita Mkuu.. we busy! We Focused!
 
Habari za Asubuhi wanaJF ni tumaini langu Mwenyezi Mungu anazidi kuwabariki katika maisha yenu kwa kadri mnavyostahili na kwa kadri ya mapenzi yake!

Majuzi nilikuja na uzi hapa JF, link hii hapa Ushuhuda: Hii ni ishara tosha kuwa wanaume kamwe hatutakiwi kuwa na mwanamke mmoja!

Katika uzi huo nilijaribu kuelezea changamoto za Kimapenzi nilizopata hasa kwa Mpenzi wangu E na kwa mchepuko wangu F .., then nikaja kumuacha F yaani nilimwambia kuwa sikuhitaji na sitaki kukuchezea aheri utafte mwanaume wako, sijui F akafanya nini baada ya hapo kwa Maelezo Mazuri unaweza ukarefer kwenye link hapo Juu..

Kufupisha story ndefu E alitaka kuachana na mimi baada ya kuona anamkosea Mungu na Wazazi wake (Kwa kadri ya maelezo yake, Uasherati na kudanganya wazazi akitaka kuja kwangu).. alinambia A nataka niwe mwenyewe, nataka nifocus vizuri katika masomo yangu, E ni Mwanafunzi wa Kidato cha sita katika shule moja ya serikali hapa Nchini, Hakuwa na simu bali huazima simu ya rafiki yake kila alipotaka kuwasiliana, aliniambia hataki mahusiano, anataka kumtumikia Mungu.. niliumia kutokana na nilivyompenda ila nikakubali, Alikuwa na Hoja ya Msingi sana, kweli Nilikuwa nampenda E..

Katika aya hii Nimpe Heshima Kubwa Mkuu Kikulacho Chako kwa ushauri mmoja alionipa ya kuwa sio kila kuachana ni mapenzi ya Mungu, Mengine ni ya Mwanadamu, kweli sikuwahi kupata hili wazo kabla, ni Jumanne tu ya wiki iliyopita wakati tumejadili kuhusu hili swala, nikafuata ushauri wa mkuu hapo juu.. nikamuingia F kisaikolojia kama kuna kitu alifanya (Ushirikina labda), Huku nikimtishia kuwa Babu yangu ni Mtaalamu, F alinywea sana..

Mwezi Mmoja uliopita baada ya kuachana na huyo Mpenzi wangu E, nilimwombea sana kwa Mungu, Nikimuomba kama nastahili kuwa na E na iwe hivyo kama sistahili na asimrudishe maishani Mwangu, nikasali Rosary na sala zingine nilizoona zinafaa.. Baada ya Kupita Mwezi Nilikata tamaa na kukosa matumaini ya E kurudi (ukizingatia ndio Mwanamke niliyepanga Kumuoa).. nikajisemea labda si stahili yangu, MAPENZI YA MUNGU YATIMIZWE..

Usiku huo wa Jumanne ya last week nilipomchimba Mkwara F, nilishtushwa na sms ikiingia kwenye simu yangu ikisomeka I REALLY MISS YOU A, I AM TRYING TO HIDE IT BUT I CANT, ikiwa na maana ya Nimekukumbuka sana A, Najaribu kuficha ila siwezi, alikuwa ni E (Hakuwahi kunitafta kwa hiari yake kipindi chote hicho mpaka nimtafte mimi), Mwanamke wangu wa Pekee..sikumjibu zaidi ya kumtakia usiku mwema..

Usiku huo nililala kwa Amani sana nikiwa na matumaini makubwa ya kuwa Mwenyezi Mungu kajibu Maombi yangu hata kama ni kwa Muda Mrefu ila Ameyajibu..Nikalala usingizi wa Kipekee sana, Mungu si Athumani asubuhi ikafika kukiwa na baridi ya wastani iliyochangamana na upepo mwanana wenye kuvutia ikiwa ni ishara ya siku nyingine ya kupendeza sana..

Ghafla simu yangu aina ya nokia ya Torch iliita toka mfukoni ikiwa ni ishara ujumbe wa maneno, niliusoma ujumbe ule ulikuwa ukitoka miongoni mwa Ndugu zake Mpenzi wangu E, nilisisimka mno, ikiwa ni faraja kubwa kwangu kutafutwa na ndugu za mwanamke nimpendae, hakika ilikuwa ni ishara njema sana kwangu.. Haikupita lisaa nikatafutwa na ndugu zake wengine wawili wote wakinambia wamenimiss, na nikiwa na uhakika hawakuwasiliana na E wala E hakuwasihi wafanye hivyo..nilijiona mwenye Bahati..

E akawa na utaratibu wa kunitafta kila usiku apatapo nafasi kwa wiki yote hii iliyopita, Jana jumatatu usiku baada ya kumaliza kupata chakula cha jioni kama kawaida yangu nilijikalia kitandani nikiwa napitia baadhi ya kurasa za katekisimu ya kanisa Katoliki..ndipo ulipoingia ujumbe wa maneno uliosomeka A im not fine, alikuwa ni E, kumuuliza akaniambia A toka nimeachana na wewe nimekuwa kama nipo kwenye jehanam, focus niliyoitaraji si ya kweli, siwezi kufocus bila wewe..NISAMEHE A, NAKUPENDA A, PLEASE NIPOKEE.. SIWEZI BILA WEWE,.. Najua hapo ni hisia gani unazipata hasa pale Mwanamke unayempenda anakutamkia hayo maneno hasa katika kipindi ambacho hukutarajia...inafariji sana..

Ndugu zangu ni hakika na imani yangu E Ananipenda hili nalifahamu toka mwanzo labda pia ndio sababu kubwa ya kumngangania na kuendelea kumpenda na pia nina uhakika hakudate na Mwanaume katika kipindi hiki cha miezi miwili ambacho hakuwa na mimi (Anasoma shule ya wasichana Peke yake, pia kutokana na maelezo ya watu wa karibu nilioweka wamchunguze).. sasa kama Mlivyonishauri vema katika uzi uliopita naombeni mnipe tena nasaha je Huu uhusiani utafaaa tena? yaani utafanya kazi kama ule wa kwanza?.. Nimkubalie? kwa maana bado sijajmjibu.

Na pia kutokana na maelezo katika Nyuzi zote hizo Mbili Assume uhusiano utatiki na utafanya kazi..Je nifanye Marekebisho yapi ambayo unaona yanafaa ili kuboesha uhusiano wangu?

Asanteni sana, JF (MMU) imekuwa wigo mzuri wa kutatua changamoto za kimahusiano kwa wale ambao wameamua kuitumia jukwaa hili kwa manufaa halisia.

Mbarikiwe sana na Muwe na Jumanne Njema!

Architectus
Yan huelewek kabisa!
Mara E
Mara F.
Sasa hatujui hiyo E ni girly or Boy
F ni female or Male
Eg. Emmanuel, EmacUlata
F- fransi, Florence or what?
Aaargghhhh?
 
Yan huelewek kabisa!
Mara E
Mara F.
Sasa hatujui hiyo E ni girly or Boy
F ni female or Male
Eg. Emmanuel, EmacUlata
F- fransi, Florence or what?
Aaargghhhh?
Not meant for you.. Bro.. Sio lazima uelewe!
 
Back
Top Bottom