Uchaguzi 2020 Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi achukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM

Nilizaliwa miaka mingi iliyopita. Nikakutana na amani, furaha na upendo. Mbona kadri siku zinasogea hivi vitu adimu vinapotea? Ninasikitika sana. Halafu ukiwa mkweli watakuita mpinzani. Haya yalinikuta mwaka 2015 nilichukia sana wizi na ufisadi ulioimaliza nchi kiasi kwamba nilitamani upinzani uchukue nchi. Ni kwa vile sina influence ya siasa na kwenye chama changu nami ningehama kama walivyohama vingunge. Nilibaki tu kushabikia kama wenzangu walivyokuwa wanashabikia. Nikashtukia naitwa mpinzani tena Chadema wakati hata sijawahi kuwa hata na ukaribu na wanachadema wenyewe na isitoshe toka nizaliwe sijawahi hata kuhudhuria mkutano wachama chochote japo nina kadi ya chama tokaJuly 1990. Mimi nikiona mambo ya uonevu na wizi huwa ninachukizwa sana. Na nikuhakikishie kitendo cha kudhamiria kabisa kumuua Lissu kilinisikitisha sana. Hatakama angekuwa na kosa gani lakini hiyo ni mtanzania mwenzetu. Na huwa mimi siyo mpiga kura na kura ya kwanza nilipiga 2015 na ya pili nitapiga 2020 baada ya hapo nitaendelea na UTARATIBU wangu wa kutopiga kura. Nitaendelea kutumikia watanzania wote popote pale nitakapokuwa. Naumia sana moyoni mwangu.
Usipopiga kura 2020 utaacha WAJINGA wakuongoze, unawajua kwa matendo yao, sitaji jina.
 
Back
Top Bottom