Uchaguzi 2020 Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi achukua fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM

maDC njaa zinawaua na wanatembeza sana bakuri kuomba mafuta ya gari na hela za matengenezo ya magari. Ndio maana wengi wanajaribu kukimbilia Bungeni kwenye neema tele
 
Hivi hawa waliojitoa mhanga vipi kama watamuudhi Mkuu alafu 'washughulikiwe' kwenye mchujo wakose yote?.
 
Nimekaa kidogo shinyanga Ila Masele anakubalika Sana shinyanga Mjini.Huyu hatoboi kwenye kura za maoni
 
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patribas Katambi amechukuwa form kuwania kiti cha ubunge shinyanga mjini , patrobas katambi amekuwa mtiania wa 49 shinyanga mjini huku wanaitajwa kuwa na nguvu ndani ya chama wakitajwa ni gasper kileo na Steven masele.

=======
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi leo Jumatano Julai 15,2020 amechukua Fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwaka 2015 akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi aligombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA,hata hivyo Stephen Masele (CCM) aliibuka mshindi kiti cha Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na mwaka 2017 Katambi alijiunga CCM na baadaye kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma.

Hizi nguvu zinazoongelewa ni nguvu za kiume ama?
 
Huyo si alitoka CDM?
Kumbuka apo yule GAK ( Gaspar Kileo),Phantom na Fresho ndiyo wafanya nani awe mbunge
GAK naye anagombe safari hii, hivyo wale wa mbereko safari hii watajijua wenyewe! Ila hata akisimama huyo GAK kwa Makamba anakaa!
 
maDC njaa zinawaua na wanatembeza sana bakuri kuomba mafuta ya gari na hela za matengenezo ya magari. Ndio maana wengi wanajaribu kukimbilia Bungeni kwenye neema tele
Ni Upuuzi Tu Huwa Hawaelewi; Kazi kama hizo ni za Kutengeneza Connection na kupata Publicity; Huku ukiandaa Miradi binafsi
Yuko DC Fulani ivi wa Kikwete Awamu ya Kwanza; Tuko nae Ughaibuni Very Smart, na Shule Huko Kigamboni an Vituo Vya watoto Yatima; yeye ni kutuma Kufanya Fundraising tu kutoka kwa Donors; na kurusha Tz kwa aajili ya mradi yake;
niliongea nae Alinambia kwamba yeye hakuwa na attention ya moja kwa moja na Siasa; Lengo lake lilikuwa Hilo tu.
 
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patribas Katambi amechukuwa form kuwania kiti cha ubunge shinyanga mjini , patrobas katambi amekuwa mtiania wa 49 shinyanga mjini huku wanaitajwa kuwa na nguvu ndani ya chama wakitajwa ni gasper kileo na Steven masele.

=======
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi leo Jumatano Julai 15,2020 amechukua Fomu kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwaka 2015 akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Patrobas Katambi aligombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA,hata hivyo Stephen Masele (CCM) aliibuka mshindi kiti cha Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na mwaka 2017 Katambi alijiunga CCM na baadaye kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma.

Huyu mwenye sura mbaya na meno kama ya popo lazima atapigwa chini
 
Hujui watu wewe kaa kimya

Watu wapo kazini

Unadhani alikuwa CDM huyu, ndio makosa mnafanya CDM

Watu wapo kazini,endeleeni kuvamia watu,nchi hii ilijengwa na Nyerere.

Period
Acha kujiaminishanujinga Wewe poyoyo sasa kama nchi ilijengwa na nyerere huyo nyerere yuko wapi by the way huyo boys wako asubir moto wa kura za maoni ndo atajua kuwa kununuliwa ukiwa na umri huo ni majuto kwanza mshaur akafanye sup zake pale law school maana miaka na miaka ameshindwa kuzichomoa pili yeye na ccm wenzake wasubir moto wa cdm kwa Salome makamba.
 
Nilizaliwa miaka mingi iliyopita. Nikakutana na amani, furaha na upendo. Mbona kadri siku zinasogea hivi vitu adimu vinapotea? Ninasikitika sana. Halafu ukiwa mkweli watakuita mpinzani. Haya yalinikuta mwaka 2015 nilichukia sana wizi na ufisadi ulioimaliza nchi kiasi kwamba nilitamani upinzani uchukue nchi. Ni kwa vile sina influence ya siasa na kwenye chama changu nami ningehama kama walivyohama vingunge. Nilibaki tu kushabikia kama wenzangu walivyokuwa wanashabikia. Nikashtukia naitwa mpinzani tena Chadema wakati hata sijawahi kuwa hata na ukaribu na wanachadema wenyewe na isitoshe toka nizaliwe sijawahi hata kuhudhuria mkutano wachama chochote japo nina kadi ya chama tokaJuly 1990. Mimi nikiona mambo ya uonevu na wizi huwa ninachukizwa sana. Na nikuhakikishie kitendo cha kudhamiria kabisa kumuua Lissu kilinisikitisha sana. Hatakama angekuwa na kosa gani lakini hiyo ni mtanzania mwenzetu. Na huwa mimi siyo mpiga kura na kura ya kwanza nilipiga 2015 na ya pili nitapiga 2020 baada ya hapo nitaendelea na UTARATIBU wangu wa kutopiga kura. Nitaendelea kutumikia watanzania wote popote pale nitakapokuwa. Naumia sana moyoni mwangu.
 
Back
Top Bottom