TANZIA Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga afariki Dunia

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,059
23,929
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga amefariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Milambo Mkoani Tabora usiku huu.

Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga alistaafu mwezi Julai, mwaka 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Bw. Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya Brig. Gen. (Rtd) Emmanuel Maganga.

Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga alilitumikia jeshi la wananchi wa Tanzania kwa muda wa miaka 37, akiwa kitengi cha ugakuzi wa Ulinzi jeshini (Defense Inspection Unit). Aliagwa rasmi pamoja na maafisa wenzake wa ngazi za juu mnamo tahere 04 Machi 2016 katika gwaride maalum lilioandaliwa katika kambi ya Jenerali Abdallah Twalipo, Temeke Dar Es Salaam. Aliteuliwa mwaka huo huo kuwa mkuu wa mkoa wa Kigoma.

_MG_4783.JPG

Brig. Jen Mstaafu Emmanuel Maganga enzi za uhai wake
#RIPMaganga
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia leo Usiku huu.

Taarifa za awali zinasema kuwa Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi mkoani Tabora.
 
Zamani ukuu Wa mkoa ilkuwa cheo cha hatari,ilkuwa ni lazima uwajue wakuu Wa mikoa yote Tanzania.

Maana wakati mwingine unaweza kuulizwa swali kwenye mtihani,mf taja mkuu Wa mkoa Wa Mwanza?,unataja chapu.

Ila toka wameanza kuwekwa vijanavijana hawa mwendo kasi ka kina Gambo,Makonda,Hapi nk,wameharibu hicho cheo tokana na matendo yao hasa hicho cheo kuwa cha kisiasa zaidi.

Mi nilikuwa hata sijui mkuu Wa mkoa huo JIna ndo naskia Leo baada ya Ku RIP,hata ukiniuliza sa hii mkuu Wa mkoa nilioko saa jina lake sijui mpaka niingie Google.
 
Huyu Brig nilimfahamu baada ya hii video, nimeshtushwa na taarifa kwamba ameaga dunia wakati anapata matibabu, RIP

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia leo Alhamis usiku Januari 21,2021.

Taarifa za awali zinasema kuwa Brigedia Jenerali mstaafu, Emmanuel Maganga amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Jeshi mkoani Tabora.

Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga alistaafu mwezi Julai, mwaka 2020 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Bw. Thobias Andengenye (aliyewahi kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji) kuwa Mkuu wa mkoa wa Kigoma kuchukua nafasi ya Brig. Gen. (Rtd) Emmanuel Maganga.
 
Doh rip nilimfahamu sana muda mwingi anavaa mashati yake ya Mandela na bastola kiunoni kwao Turiani, Morogoro.
 
RIP Brigadier Maganga. Hii video itakua ilichukuliwa kabla ya maombi ya siku tatu kuikomesha COVID.
 
Back
Top Bottom