Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima (44) na wenzake wawili wafikishwa mahakamani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima (44) na wenzake wawili leo Juni 22, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita ikiwemo mawili ya utakatishaji fedha.

Wengine ni Mariam Mshana (40), aliyekuwa mkuu wa idara ya fedha ya halmashauri hiyo na Innocent Maduhu (40) aliyekuwa mkuu wa idara ya mipango ya uchumi.

Mbali na watuhumiwa hao, wengine ni Nuru Ginana na Alex Daniel ambao walikuwa wachumi katika jiji hilo, nao walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha dhamana ambapo kupitia mawakili wao waliieleza mahakama hiyo kuwa hawajakamilisha masharti ya dhamana.

Katika kesi hiyo Jamhuri inawakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule, Wakili wa Serikali, Charles Kagilwa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Richard Jacopiyo huku washtakiwa hao wakiwakilishwa na Mawakili Valentino Nyalu na Sabato Ngogo.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5/2022, washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ambapo kosa la kwanza linalowakabili ni ufujaji na ubadhirifu wa Sh103 milioni, kosa la pili na la tatu ni kutumia nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri.

Kosa la tano linalomkabili Maduhu ni utakatishaji fedha huku la sita likiwa utakatishaji ambalo linawakabili wote watatu.

Wote walikana kutenda makosa hayo ambapo upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na hakimu

Mwakisu aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5, 2022.

Chanzo: Mwananchi
 
Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima (44) na wenzake wawili leo Juni 22, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita ikiwemo mawili ya utakatishaji fedha...
hizo kesi hazina mashiko ni zuga tu kwa watanzania.sasa kama upelelezi haujakamilika wanakamatwa kwa kosa lipi linalowakabili?
 
Wema ni Akiba na Ubaya ni akiba....mnalo la kujifunza 2025
 
hizo kesi hazina mashiko ni zuga tu kwa watanzania.sasa kama upelelezi haujakamilika wanakamatwa kwa kosa lipi linalowakabili?
Wenzio wanapelekwa Lupango wewe unabwabwaja tu
 
Ukibambikiwa utakatishaji fedha ujue unalo!! Hiyo tuhuma huwa haina dhamana!! Ni maumivu makali sana!!
 
Wangapi wametoka nchi hii
Hakuna kesi hapo
Sisi tunataka kuona mtu akipatikana na hatia anyolewe miaka kadhaaa

Ova
 
Aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha, Dk John Pima (44) na wenzake wawili leo Juni 22, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakikabiliwa na kesi nyingine ya uhujumu uchumi yenye mashtaka sita ikiwemo mawili ya utakatishaji fedha.

Wengine ni Mariam Mshana (40), aliyekuwa mkuu wa idara ya fedha ya halmashauri hiyo na Innocent Maduhu (40) aliyekuwa mkuu wa idara ya mipango ya uchumi.

Mbali na watuhumiwa hao, wengine ni Nuru Ginana na Alex Daniel ambao walikuwa wachumi katika jiji hilo, nao walifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kukamilisha dhamana ambapo kupitia mawakili wao waliieleza mahakama hiyo kuwa hawajakamilisha masharti ya dhamana.

Katika kesi hiyo Jamhuri inawakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Janeth Sekule, Wakili wa Serikali, Charles Kagilwa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Richard Jacopiyo huku washtakiwa hao wakiwakilishwa na Mawakili Valentino Nyalu na Sabato Ngogo.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 5/2022, washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa sita ambapo kosa la kwanza linalowakabili ni ufujaji na ubadhirifu wa Sh103 milioni, kosa la pili na la tatu ni kutumia nyaraka kwa malengo ya kumdanganya mwajiri.

Kosa la tano linalomkabili Maduhu ni utakatishaji fedha huku la sita likiwa utakatishaji ambalo linawakabili wote watatu.

Wote walikana kutenda makosa hayo ambapo upande wa Jamhuri ulieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na hakimu

Mwakisu aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5, 2022.

Chanzo: Mwananchi
Uyu maduu wakati wa uchaguzi 2020 ndo alikua msimazi wa uchaguzi wilaya ya ukerewe,aloyafanya mungu ndo anamlipa Leo
 
Uyaivuruga kesi kwa kuweka tarehe ambayo si sahihi.
 
hizo kesi hazina mashiko ni zuga tu kwa watanzania.sasa kama upelelezi haujakamilika wanakamatwa kwa kosa lipi linalowakabili?

Kabisa yaani ni usanii wa wazi. Na hizo mahakama zilivyoshuka kiwango ni kupotezeana tu muda.
 
Umesababisha niangalie kalenda mara mbili mbili ujue... leo tarehe 22? Wakati hata mshahara bado!
 
Daaah hii nchi ngumu kila mtu anapiga dili tena hela ndefu sana
Wafanyakaz wa serikali hawaogopi tena
Vikao hewa
Mara kisima kimahama yaan uongo tupu
Wizi wizi wizi wizi wizi
Daaah hatariiii Sana
 
Kwenye nchi ya MBILIKIMO HATA WALIMU WAKE HUONEKANA NI MBILIKIMO, CCM ni waizi watupu wanaomsifia mama Yao ni wezi wajao 2026
 
Back
Top Bottom