Tetesi: Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu akamatwa na TAKUKURU

Status
Not open for further replies.
Kweli moyo ni mdanganyifu kuliko vyote, tena una ugonjwa wa kufisha. Mtu unalamba mshahara halali wa zaidi ya 20m kwa mwezi lkn bado haiutoshi!

Mimi nikipata mshahara wa usd 5,000/ = kwa mwezi sina sababu ya kufanya ufisadi.

Vv
Hivi huyu alikuwa hausiki na ile maximum 15m ya mkuu??
 
Sasa bila shaka mtaelewa kwa nini Rais wetu anaomba tumwombee.Kwa dhati ya moyo wake ameamua kusafisha nchi anapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania mwenye nia njema na nchi hii.Nataka niwambie kwa mwendo huu Tanzania mpya yenye maendeleo haiepukiki.viva Magufuli viva Tanzania tuendelee kumwombea apambane na wale wote walikwisha ibia nchi hii kwa muda mrefu
Safi kabisa kama kwa mwendo huu tutaenda mpaka kwenye kivuko kilee, mabilioni ya ujenzi,vichwa vya treni na kandarasi fake za Kiwanja.
Kama tunachagua miongoni mwa wezi nani ashughulikiwe na nani tumbebe haitakuwa nia njema bali ovu
 
Tatizo lako unashangilia watu wawe na hali ya umaskini kama ulivyo ww,pole sana jitahd kutafuta na uwaombee walionazo waendelee kuwa nazo ili kuna siku na wwutapitia hapo.
Bila shaka hunifahamu ndio maana umeandika hivyo.mimi sio masikini na sio fisadi.ila penye ukweli tuseme ukweli nchi hii ni kwetu sisi Leo na kesho ni watoto wetu na wajukuu.ikiwa ufisadi ulioanza kujengeka ungeachwa utamalaki tena kwa miaka kumi nchi ingeweza kuanguka kabisa.tumshukuru sana Mungu kumwinua Magufuli kwa wakati wake na kwa majira yake ili atuokoe.kazi hii anayofanya Magufuli si yeye bali Mungu anayofanya kupitia kwa Magufuli na akisha kumaliza kazi ya Mungu aliyotumwa kuifanya atapumzika ila kwa sasa tumpe support yote ili atimize utume wake kwa watanzania
 
Mm kwa maoni yangu hili limechelewa sana, mchechu, kule nssf na maliasili katika utawala ule waliwekwa watu kwa maslah ya watawala(utatu mtakatifu)na wamekula kweli kweli huku wakihakikishiwa usalama. Ni bahati mbaya tu watawala wao wako juu sheria hawaguswi.

NHC contract zote za miradi mikubwa tender zote zake na marafiki wenzake, viwanja vinanunuliwa 10mil vinauziwa NHC bilioni. Wame- manipulate price vya kutosha kwa wizi tu.
 
Siwezi kumuunga mkono rais wa visasi, anayekumbatia mabashite, anayevunja nyumba za wanyonge, anyesigina demokrasia, ameweka kapuni katiba mpya, anayefurahia watu wake kula msoto, asiyetaka wengine waombewe, asiyehudhuria misiba, anayekula rambirambi, anayesema wazi hakuna kuchagua wapinzani kama vile siasa imekuwa uadui, anayezalisha wake za watu, anayehubiri amani wakati kaficha panga mgongoni. Anayetafuta kiki kwa vitu ambavyo ni vya kawaida, nini Msechu, tuliona akina Mramba wakiingia jela. Anayetufanya kwa kutudanganya dollar bilioni moja zimekamatwa, kama vile dollar hizo ni hela ya kukaa kwenye handbag, asiyetimiza ahadi zake, wapi millioni 50 kwa kila kijiji. NIKISEMA NTAMWOMBEA NTAKUWA MNAFIKI KAMA YEYE, AKINILAZIMISHA KUMWOMBEA NTAOMBA KINYUME
Who cares?

Kwani umelazimishwa kumuunga mkono?

Unaweza kumuunga mguu kama ukipenda!

Sidhani kama unapiga hata kura lakini hiyo kura yako moja ni uchafu tu katika sanduku la kura.

Love him or loathe him, Rais Magufuli is here to stay.
 
Mara baada ya kusimamishwa kazi Jana, Nehemia Mchechu kakamatwa na TAKUKURU kwa mahojiano zaidi.

Taarifa zinasema Junanne atapandishwa mahakamini kwa makosa kadhaa yakiwemo uhujumu uchumi, uchepushaji na matumizi mabaya ya madaraka

Mytake:
Kwa kweli Rais Magufuli Mungu azidi kukubariki sana sana. Unafanya kazi iliyotukuta hasa kwa wanyonge. Mungu akubariki sana Rais Magufuli


Mbn dau wa nssf hakamatwi, hii ni double std analeta jpm
 
Kusema ukweli Nehemiah nimekuwa namuona tu kwenye TV akiongea sijui Kuhusu maisha ni nyuma na miradi kibao kibao ya NHC.

Ila moyo wangu Haujawai kukataa kuwa Nehemiah ni jizi...nimekuwa najaribu sana kuuhaminisha moyo wangu kuwa huyu jamaa sio jizi ila nimeshindwa.

Inawezekana yao takukuru wasipate ushahidi wa kumtia hatiani ila narudia Nehemiah ni JIZI....moyo wangu Haujawai kunidanganya
 
Bila shaka hunifahamu ndio maana umeandika hivyo.mimi sio masikini na sio fisadi.ila penye ukweli tuseme ukweli nchi hii ni kwetu sisi Leo na kesho ni watoto wetu na wajukuu.ikiwa ufisadi ulioanza kujengeka ungeachwa utamalaki tena kwa miaka kumi nchi ingeweza kuanguka kabisa.tumshukuru sana Mungu kumwinua Magufuli kwa wakati wake na kwa majira yake ili atuokoe.kazi hii anayofanya Magufuli si yeye bali Mungu anayofanya kupitia kwa Magufuli na akisha kumaliza kazi ya Mungu aliyotumwa kuifanya atapumzika ila kwa sasa tumpe support yote ili atimize utume wake kwa watanzania
Hata huyo unaye mzungumzia mtume wa mungu unamfaham vzuri?au unasema tu ili watu wasome?kwann husemi juu ya maonevu wanayofanyiwa watu ni kweli skujui lkn pia nadhani hunijui fanya uchunguzi umjue mtume vzuri.
 
Mytake:
Kwa kweli Rais Magufuli Mungu azidi kukubariki sana sana. Unafanya kazi iliyotukuta hasa kwa wanyonge. Mungu akubariki sana Rais Magufuli

Wanyonge ni kina nani hao chifu?

Secondly, why Magufuli is so selective in dealing with ufisadi na uhujumu uchumi? Lini, atajipeleka TAKUKURU kuhojiwa juu ya uhujumu uchumi na ufisadi wake? Lini TAKUKURU itafanyia kazi tuhuma za Mnyeti, mtuhumiwa aliyekuwa promoted?

[HASHTAG]#magufuliisaphony[/HASHTAG]
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom