Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu TPA, Deusdedit Kakoko aachiwa kwa dhamana baada ya TAKUKURU kukamilisha Uchunguzi dhidi yake kwa 98%

Hivi kwa nini nyinyi wabongo mnafurahia sana wenzenu waliwazidi nafasi kidogo wafungwe tu hata kama haijathibitika kama tuhuma zinazowahusu ni za kweli?
Mnamtia hatiani mtu kabla haijathibitika bila shaka yoyote kwamba katenda jinai, hizo roho zenu mbaya zitawafikisha wapi?
Kuna tatizo kwenye mifumo, kuna mianya inayosababisha baadhi ya watu wasio waaminifu kushiriki vitendo vya wizi, mianya hiyo haina budi kuzibwa ili fedha ya umma ibaki salama.
 
Kesi ya uhujumu uchumi kwa wengine haina dhamana ila wengine dhamana ipo...double standard

Hii kesi imeshaisha tàyari wameona upigaji uliofanyika mpaka Hayati kapiga hiyo pesa
 
Mimi sikatai, kwa hao wawili kutokuwa tayari kwao kuwa marais; na hasa kwa huyu aliyepo sasa kwenye urais, kwa sababu hakutegemea kabisa kwamba angeshika cheo hicho.

Kwa mtu anayetafuta nafasi kama ya urais, labda tuseme kujiandaa kwake ni kuwa katika siasa na kushika nafasi za ngazi mbalimbali, huku akijijenga atambulike kwa wenzake na wananchi kwa kuwa na misimamo juu ya mambo yanayohusu serikali na nchi kwa ujumla.

Atakuwa ameshika nyadhifa na kufanya maamuzi muhimu juu ya mhimu yanayoihusu nchi.

Kiufupi niseme, mtu huyo atakuwa amejijengea historia inayomtambulisha kwa wenzake na kwa raia.

Mtu huyu pia atakuwa amekwishaonyesha sifa ya kuwa na maono ya nini kifanyike juu ya hatma ya nchi anayotaka kuiongoza.

Haya yote ndiyo yatakayomtambulisha kwa wenzake na wananchi kuwa yeye ni kiongozi na atakapofanya kampeni za uchaguzi atayasisitiza haya, na hatimaye wananchi wanampa ridhaa ya kuwaongoza.

Katika hawa wote tunaowazungumzia hapa, hakuna hata mmoja aliyepitia hatua hizo.

Kwa hiyo tunaweza kusema...Hawakujiandaa.
Swadakta kabisa mkuu, na hii ni issue ya kimfumo zaidi kwenye nchi zinazojitambua, ambapo utakuta hapa ndio idara za usalama hufanya kazi kubwa kwa maslahi mapana ya taifa. Na ili kuepusha nchi kuongozwa na mtu ambaye hakutarajia kuwa Rais, endapo Rais aliyepo atashindwa kuendelea na majukumu yake au kufariki, basi watarudi kwenye uchaguzi mkuu. Sijui kwanini Tz hatukurekebisha hii sheria!!!
 
Kwani DPP anashindwa nini kusema kesi ipo au hakuna? 2% inachukua miaka mingapi ? Wengi walio jela sasa wanasubiria DPP consent mbona hawapati dhamana ? Why Kakoko? Au Mama nae anaogopa akitoka watu wake kusumbuliwa bila msaada ? Mfumo wa kulindana ....kama nyuma kuna mtu mwenye kinga?
 
Magufuli aliupata uRais kwa Zali/hakujiandaa. Samia naye ameupata Urais kwa zali pia, hakujiandaa.
Tuendapo ni Mungu anajua.
Wanaojiandaa wanakuwa wabaya sana kwani ni wanasiasa wenye kutegemea kundi kubwa la watu. Huwa wameshatengeneza mgawanyiko kabla hata hawajaapishwa.
 
Wanaojiandaa wanakuwa wabaya sana kwani ni wanasiasa wenye kutegemea kundi kubwa la watu. Huwa wameshatengeneza mgawanyiko kabla hata hawajaapishwa.
Kikwete ni jibu sahihi(?)...; ni kama nauliza huku nikitoa mfano halisi!

Lakini niseme hapa, siyo wote; na hata kama wakiwa na "kundi kubwa la watu" kwamba viongozi hao hawawezi kuongoza vizuri kwa kutumia maono yao.
Kuwa na kundi/makundi ni lazima kwenye siasa, na sio lazima hayo makundi yawe ni kwa ubaya/upigaji tu.

Kiongozi mzuri ataunda kundi la watu wanaokubaliana na maono na matarajio yake juu ya anayotaka kuyafanya akiwa kiongozi.
 
Back
Top Bottom